• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
Ubungo Municipal Council
Ubungo Municipal Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Malengo na dhamira
    • Maadili ya Msingi
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Elimu Sekondari
      • Kilimo umwagiliaji na ushirika
      • Fedha na Biashara
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Mipango miji na Ardhi
      • Elimu Msingi
      • Utumishi na Utawala
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Maendeleo ya Jamii na Vijana
      • Maji na Usafishaji
      • Ufugaji na Uvuvi
      • Ujenzi
      • Mazingira na udhibiti wa taka ngumu
    • Vitengo
      • Kitengo cha Sheria
      • Ukaguzi wa ndani
      • TEHAMA
        • Uhusiano
      • Uchaguzi
      • Manunuzi na Ugavi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Ufugaji
    • Kilimo
    • Masoko
    • Vituo vya Basi
    • Viwanda
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Biashara
      • Ushuru wa Huduma
      • Usajili wa Tax
      • Leseni za Biashara
      • Ushuru wa Hoteli
    • Ujasiliamali
    • Kilimo
    • Uvuvi
    • Ufugaji
      • UJUWA
  • Madiwani
    • Orodha za Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za kudumu
    • Ratiba za vikao vya kisheria
    • Ratiba ya Kumuona Meya
  • Miradi
    • Miradi iliyopangwa
    • Miradi endelevu
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Fomu
    • Ripoti
    • Sheria
    • Vipeperushi
    • Zabuni iliyotangazwa
    • Mpango Mkakati
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Hotuba

VIKUNDI VYA VICOBA KUSAJILIWA KIELEKTRONIKI

Posted on: March 29th, 2021

Maafisa Maendeleo ya Jamii kutoka kata 14 za Manispaa ya Ubungo wamepata mafunzo ya namna ya kusajili vikundi vya kijamii vya huduma dogo za fedha maarufu kama VIKOBA kwa njia ya kielektroniki  ili wakaelimishe vikundi vilivyopo kwenye maeneo yao na kuvisaidia katika usajili Mpya kama sheria inavyotaka

Akizungumza wakati wa kutoa mafunzo kwa maafisa hayo, Afisa Maendeleo wa Manispaa ya Ubungo,  Evelyne Mangwea alisema kuwa, usajili huu Mpya wa vikundi vya kijamii ni utekelezaji wa sheria ya huduma ndogo za fedha ya mwaka 2018 na kanuni zake za mwaka 2019.

Usajili wa vikundi hivyo kupitia mfumo huo  itarahisisha usajili, usimamizi na utoaji wa taarifa za vikundi Kwa lengo la kuimarisha usimamizi wa sekta ndogo ya fedha ili kukidhi mahitaji halisi ya wananchi wa kipato cha chini na hivyo kuongeza ukuaji wa uchumi na kupunguza umasikini kwa wananchi

Evelyne ameeleza usajili wa vikundi kupitia mfumo huo  mpya wa kielektroniki utasaidia kwa kiasi kikubwa  kupunguza wizi, udhulumaji, migogoro  pamoja na  kudhibiti upotevu wa fedha kwenye vikundi.

"Kuanzia tarehe mosi mei mwaka huu vikundi vyote vinatakiwa viwe vimejisajili kwenye mfumo wa kielektroniki ili ili viweze kutoa huduma za kifedha na usajili huu ni bure hivyo kila Afisa Maendeleo akahakikishe anatoa elimu ya usajili huu kwa vikundi vilivyopo kwenye kata yako" alieleza Evelyne.

Evelyne ameendelea kufafanua  kuwa,  Vikundi vitakavyohusika na usajili kupitia mfumo huo  Mpya unaosimamiwa na Benki Kuu ya Tanzania  (BoT) ni vile ambavyo havijasajiliwa kisheria   ili vitambuliwe  na mifumo ya kifedha ya Serikali na kuhakikisha usalama wa fedha zao.

Kwa mujibu wa muingozo huu kikundi kitaweza kusajili wanachama  kuanzia kumi (10) hadi hamsini  (50) na sio zaidi au chini ya hapo. Aidha vikundi hivyo vitajulikana kwa jina la  Community microfinance Groups  ( CMGs) badala ya  jina la VICOBA lililozoeleka.

Akielezea  namna ya kutumia mfumo huo  wa usajili, Afisa Tehama  wa Manispaa  hiyo Aziza ameeleza kuwa baada ya kupatiwa elimu ya namna ya usajili, wanachama watajisajili wenyewe  kwa kutumia  komputa au simu za rununu na Afisa Maendeleo ngazi ya kata  atapata  fursa kuvisaidia vikundi katika zoezi la usajili ikiwemo kuhakikisha nyaraka zinazotakiwa zinapakiwa kwenye mfumo pamoja na   kuona vikundi vinavyojisajili.

Akiongea kwa niaba ya maarifa maendeleo waliohudhuria mafunzo hayo, Ramla Mustafa Afisa Maendeleo wa kata ya Ubungo amesema watajitahidi kuwaelekeza wanavikundi  kujisajili kupitia mfumo you mpya ili waweze kuendelea na shughuli zao za kuwezeshana kiuchumi pamoja na kufuatia sheria za nchi.


Taarifa

  • HUDUMA YA KUKODI GARI LA MAJI TAKA June 12, 2019
  • TAARIFA KWA UMMA August 12, 2019
  • Tangazo la ukataji au kuhuisha leseni na Tozo mbalimbali. December 08, 2017
  • Uchangiaji Damu Hospitali ya Sinza June 14, 2018
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • WAMILIKI WA MABASI WAAGIZWA KUFUNGA OFISI ZILIZO NJE YA KITUO CHA MAGUFULI

    April 01, 2021
  • MAAFISA UGANI MANISPAA YA UBUNGO WAPIGWA MSASA KUHUSU MFUMO WA MOBILE KILIMO(M-KILIMO)

    March 26, 2021
  • TARI YAWAJENGEA UWEZO WATAALAMU WA KILIMO MANISPAA YA UBUNGO JUU YA KANUNI BORA ZA KILIMO

    March 29, 2021
  • VIKUNDI VYA VICOBA KUSAJILIWA KIELEKTRONIKI

    March 29, 2021
  • Tazama zote

Video

More Videos

Viunganishi vya haraka

  • Leseni za biashara
  • Ushuru wa Hoteli
  • Kibali cha ujenzi
  • Sheria ndogondogo
  • Malengo na Dira
  • Muundo wa Uongozi
  • zabuni

Viunganishi linganifu

  • The National Examinations Council of Tanzania
  • TAMISEMI
  • Ministry of Education
  • President office State House
  • National Council for Technical Education
  • Ministry of Finace and Planning

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya wanaoingia

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Kibamba Area, Morogoro Road

    Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam

    Telephone: +255 22 2926341

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: md@ubungomc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa