Idara ya Maji ipo kwa mujibu wa muundo wa Utumishi. Idara ina vitengo vikuu vitatu.
• Kitengo cha mipango na usanifu
• Kitengo cha ujenzi
Kitengo cha uendeshaji wa miradi ya maji na matengezo vinavyotambuliwa kisheria.
Malengo/Majukumu ya Idara ya Maji
Kuandaa bajeti ya kutekeleza miradi ya maji na kusimamia utekelezaji wa miradi hiyo
Kutoa huduma ya maji safi na salama kwa wakazi wa Manispaa ya ubungo wasiopata huduma ya maji kutoka kwa mamlaka ya DAWASA na Kampuni ya DAWASCO.
Ø Kutoa huduma ya uzoaji maji taka kwenye sehemu ambayo magari makubwa ya kuzoa maji taka hayafiki kwa kutumia pikipiki yenye miguu mitatu na pampu maalumu ya kuvuta maji taka.Kutoa mafunzo, kusimamia mchakato wa kuunda vyombo vya kusimamia na kuendesha miradi ya maji pamoja na kuvisajili, kwa
Ø mujibu na taratibu wa Sheria ya Maji ya 2009.
Ø na kuendesha miradi ya maji kutunza fedha za matengezo na kuwa na nidhamu ya matumizi ya fedha za mfuko.
Ø Japo kwa kiwango kidogo, kuweza kuchangia kukusanya mapato ya Halmashauri kupitia ukusanyaji wa fedha zinazotokana na upimaji wa maji katika maabara ya Idara ya Maji na ukataji wa vibali kwa wachimbaji wa visima wanaofanya kazi ndani ya Manispaa yetu.
Ø Kupunguza na kuzuia milipuko ya magonjwa yanayosababishwa na ukosefu wa maji safi na salama
Ø Kusimamia vyema miradi inayofanya kazi kwa kusisitiza vyombo vya kusimamia
Vitengo vinaunda sehemu kumi na moja katika Idara. Idara ya Maji ina jukumu kubwa la kutoa huduma ya maji kwa wakazi wa Manispaa ya Ubungo. Pamoja na jukumu la kutoa huduma ya maji Idara inahusika na kupanga na kusanifu miradi ya maji, kupitia usanifu wa miradi ya maji unaofanywa na wataalam wa nje, kusimamia ujenzi na uendeshaji wa miradi ya maji pamoja na kukarabati miradi ya maji yenye hitilafu. Idara pia inahusika na kuunda na kusimamia vyombo vya watumiaji maji
Kibamba Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa