Idara ya Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika inaundwa na sehemu tatu (3) ambazo ni:-
Ø Kilimo
Ø Umwagiliaji
Ø Ushirika
Majukumu ya idara
Jukumu kuu la Idara hii ni kuhamasisha, kuboresha na kusimamia utoaji wa huduma za maendeleo ya kilimo, Umwagiliaji na Ushirika katika jamii kwa kushirikiana na wadau mbalimbali.
Ø , usambazaji wa uuzaji wa pembejeo na zana za kilimo kutoka maduka ya watu binafsi.
Ø Usimamiaji wa matumizi ya pembejeo za kilimo katika Mitaa/Kata.
Ø Kutoa elimu/ushauri wa matumizi ya mbolea na madawa, kilimo mseto, usindikaji wa mazao, hifadhi ya udongo na matumizi bora ya ardhi, kilimo cha umwagiliaji na uzalishaji wa mazao mbalimbali ya nafaka, uyoga, mboga, matunda, miche ya matunda, miti ya kivuli na maua kwa kuzingatia kanuni bora kwa wakulima mmoja mmoja au vikundi.
Ø Kufanya tathmini kuhusu hali ya chakula na lishe katika Manispaa.
Ø Kusimamia, kufuatilia na kutathmini utekelezaji wa shughuli mbalimbali za Miradi ya Maendeleo ya Kilimo ya Wilaya (District Agriculture Development Projects – DADPs).
Ø Kuhamasisha na kusimamia shughuli za kilimo cha zao la korosho.
Ø Kufanya maandalizi na kushiriki maonesho ya sikukuu ya wakulima Nanenane.
Ø Kuboresha vyama vya ushirika vya aina mbalimbali.
Ø Kuimarisha ushirika wa akiba na mikopo.
Ø Kutoa mafunzo na elimu kuhusu vyama vya ushirika.
Ø wa fedha zinazotokana na upimaji wa maji katika maabara ya Idara ya Maji na ukataji wa vibali kwa wachimbaji wa visima wanaofanya kazi ndani ya Manispaa yetu.
Ø Kupunguza na kuzuia milipuko ya magonjwa yanayosababishwa na ukosefu wa maji safi na salama
Ø Kusimamia vyema miradi
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa