Maendeleo ya Jamii.
Maendeleo ya Jamii na vijana ni miongoni mwa idara katika Manispaa ya Ubungo idara ina vitengo viwili ambavyo ni vijana jinsia na watoto.
Idara inatoa huduma kwa jamii ili kuwezesha kupanga, kubuni, kutekeleza na kusimamia shughuli zao za kiuchumi na kuwa na maendeleo endelevu.
Halmashauri kupitia Idara ya Maendeleo ya jamii ina jukumu kubwa la kuwezesha jamii yake katika kutambua uwezo wao katika kutatua matatizo ya Maendeleo.
Hili limefanyika kwa kushirikiana na sekta binafsi kwa lengo la kuboresha maisha ya jamii kwa matumizi ya rasilimali zilizopo , idara ya Maendeleo ya jamii ina mamlaka ya kutambua na kuandikisha vikundi vya kijamii na kiuchumi ,mashirika yasiyo ya kiserikali na kuwaratibu.
Kwa sasa idara inatekeleza mipango mbalimbali kama vile VVU,na UKIMWI ,Mfuko wa maendeleo ya jamii TASAF, Mfuko wa mikopo ya wanawake na vijana, kamati ya uwezeshaji wanawake kiuchumi ya wilaya na mpango wa usimamizi wa maafa.
Idara ya Maendeleo ya Jamii inawajibika kutekeleza sera zifuatazo, sera ya maendeleo ya watoto-2008,sera ya Maendeleo ya Jensia -2000, sera ya Taifa ya VVU na UKIMWI -2001, Sera ya maendeleo ya Vijana-2007 na sera ya uwezeshaji wa Taifa.
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa