Kitengo Cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano kina lengo la kutoa huduma za kitaalamu juu ya matumizi ya teknolojia ya habari na mawasiliano katika Manispaa.
Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) ni nyenzo muhimu, ambayo mchango wake ni mkubwa katika kuharakisha kufikiwa kwa Malengo ya Milenia ifikapo mwaka 2025. Kukua kwa teknolojia katika Manispaa ya Ubungo, kuna mchango muhimu katika kuhakikisha kuwa wananchi wanapata taarifa kuhusu shughuli mbalimbali za utawala, sera na mipango kwa wakati mwafaka, hivyo kuwashirikisha wananchi moja kwa moja katika maamuzi yanayoathiri maisha yao. TEHAMA inatumika kila mahali na katika utoaji wa huduma za aina yoyote ile ikiwemo Elimu (Distant Learning, eLibrary), matibabu (telemedine), biashara (eCommerce, eBanking, nk),Ukusanyaji wa mapato, uongozi/utawala (eGovernace) n.k.
Kutokana na kuingia kwa utandawazi, dunia sasa imekuwa kama kijiji kimoja tena kidogo sana, kwani mawasiliano yamekuwa yakiboreshwa siku hadi siku na kuwa rahisi.
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa