• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
Ubungo Municipal Council
Ubungo Municipal Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Malengo na dhamira
    • Maadili ya Msingi
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Elimu Sekondari
      • Agriculture, Livestock and Fisheries
      • Industry,Trade and Investments
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure, Rural and Urban Development
      • Pre-Primary and Primary Education
      • Human Resources Management and administration
      • Health, Social Welfare and Nutrition Services
      • Communit Development
    • Vitengo
      • Legal Services
      • Ukaguzi wa ndani
      • TEHAMA
      • Procument Management
      • Government Communication
      • Finance and Accounts
      • Sports, Culture and Arts
      • Waste Management and Sanitation
      • Natural Resources and Environment Conservation
    • Sheria ndogo ndogo za Manispaa
      • Sheria ndogo ndogo za Manispaa
      • Other Laws
  • Fursa za Uwekezaji
    • Ufugaji
    • Kilimo
    • Masoko
    • Vituo vya Basi
    • Viwanda
  • Huduma zetu
    • Afya
      • iCHF
      • Lishe
      • Social welfare
    • Elimu
      • Pre and Primary Education
      • Elimu Sekondari
    • Biashara
      • Ushuru wa Huduma
      • Usajili wa Tax
      • Leseni za Biashara
      • Ushuru wa Hoteli
    • Ujasiliamali
      • Ten Percent Loans
    • Kilimo
    • Uvuvi
    • Ufugaji
      • UJUWA
  • Madiwani
    • Orodha za Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za kudumu
    • Ratiba za vikao vya kisheria
    • Ratiba ya Kumuona Meya
  • Miradi
    • Miradi iliyopangwa
    • Miradi endelevu
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Fomu za Maombi
    • Ripoti
    • Sheria
    • Bronchures
    • Zabuni iliyotangazwa
    • Mpango Mkakati
    • Newsletter
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Hotuba

BARAZA LA MADIWANI UBUNGO LAVUNJWA, DC MSANDO AWAMWAGIA SIFA

Posted on: June 20th, 2025

Mkuu wa wilaya ya Ubungo Mh. Albert Gasper Msando ameipongeza Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo kwa mafanikio iliyoyapata katika kusimamia na kutekeleza miradi yake kwa kiwango kikubwa.

DC Msando amesema Manispaa hiyo ni ya mfano kutokana na kusimamia vema miradi yake na kuitekeleza kwa kiwango kikubwa jambo ambalo ni tofauti na Manispaa nyingine nchini.

Alisema kuwa kwa uongozi madhubuti wa Mstahiki Meya na Baraza lake wameongeza makusanyo kutoka shilingi bilioni 18.1 mwaka 2020/21 hadi shilingi Bilioni 41.3 Mwaka 2024/25 sawa na ongezeko la shilingi bilioni 23.2 mwaka 2024/25 ambapo imesaidia kuweza kusimamia miradi yake kwa fedha zake katika miradi ya Barabara, Maji na Shule.

DC Msando aliyasema hayo wakati wa Mkutano wa kuliahirisha Baraza la Madiwani wa Manispaa ya Ubungo iliyofanyika kwenye ofisi za Manispaa ya Ubungo Juni 20, 2025.

Kwa upande wake Mstahiki Meya aliyemaliza muda wake Mh. Jaffar Nyaigesha aliwaahidi wananchi wa Manispaa yake kuendelea kushirikiana nao katika kuyaendeleza yale yote waliyoyafanya kwa kushirikiana na Madiwani na Watendaji wa Manispaa hiyo hata pale itakapotokea hawatarudi tena kwenye nafasi zao.

Aidha alisema kuwa anajivunia mafanikio makubwa yaliyoipata Manispaa katika kipindi cha uongozi wake ikiwemo sekta ya Elimu Msingi na Sekondari,  Sekta ya Afya, Uwezeshaji wananchi kiuchumi, Ukusanyaji wa Mapato, Kuongeza sekta ya Biashara, Viwanda na Uwekezaji. 

Hata hivyo Meya huyo aliwataka wananchi kuendeleza kampeni ya uwekaji safi mazingira ya Manispaa hiyo ili kupuka maradhi mbalimbali yanayosababishwa na uchafu.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo Dkt. Aron Kagurumujuli akisoma taarifa ya utekelezaji wa shughuli za Maendeleo katika kipindi cha Miaka mitano (2020/21 -2024/25) pamoja na mapendekezo ya uendeshaji wa shughuli za Halmashauri kipindi cha Mpito, amesema katika kipindi cha miaka 5 baraza limepata mafanikio makubwa ambapo jumla ya shule mpya saba (8) za awali na Msingi zimejengwa na kusajiliwa na kufanya jumla ya shule 69 za awali na Msingi kutoka shule 65 za awali na 64 za Msingi  zilizokuwepo mwaka 2020/2021.





Taarifa

  • KIBALI CHA KUANZA KUTOZA USHURU WA KUSHUSHA NA KUPAKIA MIZIGO July 17, 2023
  • KUKANUSHA TAARIFA YA UWEPO WA HARAFU MBAYA STENDI YA MABASI MAGUFULI July 06, 2023
  • MATOKEO YA SENSA YA WATU NA MAKAZI 2022 Ubungo September 06, 2023
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI NAFASI YA DEREVA NA KATIBU MAHSUSI July 21, 2022
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • WANANCHI ZAIDI YA 200,000 WANUFAIKA NA KAMPENI YA MSAADA WA KISHERIA YA MAMA SAMIA

    June 21, 2025
  • BARAZA LA MADIWANI UBUNGO LAVUNJWA, DC MSANDO AWAMWAGIA SIFA

    June 20, 2025
  • VIONGOZI WA WAFANYABIASHARA SOKO LA MANZESE WALA KIAPO CHA UADILIFU

    June 19, 2025
  • KIKAO CHA TATHMINI YA LISHE KWA ROBO YA TATU MWAKA WA FEDHA 2024/25 (JANUARI - MACHI 2025)

    June 20, 2025
  • Tazama zote

Video

KIWANJA CHAKO KINA HATI? | UMEKUWA UKISUMBULIWA NA MIGOGORO YA ARDHI? | KARIBU KWENYE ARDHI CLINIC
More Videos

Viunganishi vya haraka

  • Leseni za biashara
  • Ushuru wa Hoteli
  • Kibali cha ujenzi
  • Sheria ndogondogo
  • Malengo na Dira
  • Muundo wa Uongozi
  • zabuni

Viunganishi linganifu

  • The National Examinations Council of Tanzania
  • TAMISEMI
  • Ministry of Education
  • President office State House
  • National Council for Technical Education
  • Ministry of Finace and Planning

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya wanaoingia

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Luguruni Area, Morogoro Road

    Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam

    Telephone: +255 22 2926341

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: md@ubungomc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa