• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
Ubungo Municipal Council
Ubungo Municipal Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Malengo na dhamira
    • Maadili ya Msingi
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Elimu Sekondari
      • Agriculture, Livestock and Fisheries
      • Industry,Trade and Investments
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure, Rural and Urban Development
      • Pre-Primary and Primary Education
      • Human Resources Management and administration
      • Health, Social Welfare and Nutrition Services
      • Communit Development
    • Vitengo
      • Legal Services
      • Ukaguzi wa ndani
      • TEHAMA
      • Procument Management
      • Government Communication
      • Finance and Accounts
      • Sports, Culture and Arts
      • Waste Management and Sanitation
      • Natural Resources and Environment Conservation
    • Sheria ndogo ndogo za Manispaa
      • Sheria ndogo ndogo za Manispaa
      • Other Laws
  • Fursa za Uwekezaji
    • Ufugaji
    • Kilimo
    • Masoko
    • Vituo vya Basi
    • Viwanda
  • Huduma zetu
    • Afya
      • iCHF
      • Lishe
      • Social welfare
    • Elimu
      • Pre and Primary Education
      • Elimu Sekondari
    • Biashara
      • Ushuru wa Huduma
      • Usajili wa Tax
      • Leseni za Biashara
      • Ushuru wa Hoteli
    • Ujasiliamali
      • Ten Percent Loans
    • Kilimo
    • Uvuvi
    • Ufugaji
      • UJUWA
  • Madiwani
    • Orodha za Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za kudumu
    • Ratiba za vikao vya kisheria
    • Ratiba ya Kumuona Meya
  • Miradi
    • Miradi iliyopangwa
    • Miradi endelevu
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Fomu za Maombi
    • Ripoti
    • Sheria
    • Bronchures
    • Zabuni iliyotangazwa
    • Mpango Mkakati
    • Newsletter
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Hotuba

BARAZA LA MADIWANI UBUNGO LALIA NA UBOVU WA MIUNDOMBINU

Posted on: May 4th, 2021

Baraza la Madiwani la Manispaa ya Ubungo leo tarehe 4 Mei, 2021 limesema changamoto ya ubovu wa barabara, madaraja, vivuko na miundombinu ya shule imekuwa kero kubwa kwa wananchi wa manispaa hiyo hasa kipindi hiki cha mvua.

Kauli hiyo imetolewa na wajumbe wa mkutano Baraza hilo kwenye mkutano wa baraza wa kuwasilisha  taarifa za utekelezaji wa shughuli mbalimbali za maendeleo katika kata zao kwa kipindi cha  robo ya tatu kuanzia mwezi januari Hadi Machi mwaka huu ambapo changamoto ya  ubovu wa barabara na miundombinu ya shule imejitokeza katika kata nyingi.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti Madiwani hao wamesema kuwa hali ya miundombinu ya barabara hasa kipindi hiki cha mvua ni mbaya na hazipitiki,  wananchi wanapata shida sana hivyo " tunawaomba TARURA wafanye matengenezo ya barabara, madaraja na vivuko  kwa wakati ili kuwaondolea adha wananchi wetu"



Aidha kuhusu uchakavu wa miundombinu kwa baadhi ya shule, wajumbe wa Baraza hilo wameeleza kuwa pamoja na jitihada zinazofanywa na Manispaa pamoja na Serikali kuu ya kujenga na kukarabati Madarasa, vyoo na ununuzi wa madawati bado kuna kuna uhitaji wa Madarasa katika shule za Manispaa hiyo hivyo manipaa kwa kushirikiana na wadau iendelee kutenga bajeti ya ujenzi wa miundombinu hiyo.

Kata ya Goba na Saranga ni kati ya kata zilizoboreshawa miundombinu ya shule ikiwemo ujenzi wa Madarasa na kupelekewa madawati  katika shule zake kupitia fedha za mapato ya ndani, Diwani wa kata hiyo Ester Ndoha amemshukuru Mkurugenzi wa manispaa hiyo kwa ujenzi huo ambao umesaidia upunguza changamoto ya wanafunzi kukaa chini na ameomba juhudi hizo ziendee kwani changamoto hiyo bado ipo.

Kwa mwaka wa fedha 2020/2021 kwa upande wa Elimu Sekondari Halmashauri ya manispaa ya ubungo imeweza  kujenga Madarasa 42 yenye thamani ya shilingi milioni 675, madawati 1700 yenye thamani ya shilingi milioni 125 na matundu ya vyoo 24 yenye thamani ya shilingi milioni 24.2

Aidha Manispaa ilipokea madawati 340 kutoka Kwa wadau wa maendeleo NMB, CRDB na UNBOUND Community Tanzani.

Kwa upande wa  shule za msingi, Halmashauri ya manispaa ya ubungo kupitia fedha za mapato ya ndani imeweza kujenga madarasa 42  yenya thamani ya shilingi milioni 607, ukarabati wa madarasa 13 kwa gharama ya shilingi milioni 37, ujenzi wa vyoo matundu 22 kwa gharama ya shilingi milioni 33 na utengenezaji wa madawati 1707 yenye thamani ya shilingi milioni 87.

Akifunga mkutano wa baraza hilo, Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa hiyo Jaffary Juma Nyaigesha ameeleza kuwa ili kuboresha maisha ya wananchi baraza hilo lina wajibu wa kushirikiana na wadau wa maendeleo wakiwemo TARURA, DAWASA, TANESCO na wengine ili kuhakiksha kero hizo zinatatulika kwa wakati ili kujenga Imani kwa serikali yao ambayo iliahidi kutatua kero za zao.

Taarifa

  • KIBALI CHA KUANZA KUTOZA USHURU WA KUSHUSHA NA KUPAKIA MIZIGO July 17, 2023
  • KUKANUSHA TAARIFA YA UWEPO WA HARAFU MBAYA STENDI YA MABASI MAGUFULI July 06, 2023
  • MATOKEO YA SENSA YA WATU NA MAKAZI 2022 Ubungo September 06, 2023
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI NAFASI YA DEREVA NA KATIBU MAHSUSI July 21, 2022
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • KATA YA UBUNGO YAKABIDHI MKOPO WA TSH. 122,800,000/= KWA VIKUNDI SITA VYA ASILIMIA 10

    May 02, 2025
  • KAMPENI YA KATAA UCHAFU, SAFISHA, PENDESHA UBUNGO YAZINDULIWA, MITAA SAFI NA MICHAFU KUPEWA ZAWADI

    May 03, 2025
  • FANYENI KAZI, MSIJALI MASILAHI BINAFSI" ~ CHALAMILA

    May 01, 2025
  • HUDUMA YA KUJIFUNGUA KWA UPASUAJI YAANZA RASMI KITUO CHA AFYA GOBA,WANANCHI WAKARIBISHWA

    April 30, 2025
  • Tazama zote

Video

KIWANJA CHAKO KINA HATI? | UMEKUWA UKISUMBULIWA NA MIGOGORO YA ARDHI? | KARIBU KWENYE ARDHI CLINIC
More Videos

Viunganishi vya haraka

  • Leseni za biashara
  • Ushuru wa Hoteli
  • Kibali cha ujenzi
  • Sheria ndogondogo
  • Malengo na Dira
  • Muundo wa Uongozi
  • zabuni

Viunganishi linganifu

  • The National Examinations Council of Tanzania
  • TAMISEMI
  • Ministry of Education
  • President office State House
  • National Council for Technical Education
  • Ministry of Finace and Planning

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya wanaoingia

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Luguruni Area, Morogoro Road

    Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam

    Telephone: +255 22 2926341

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: md@ubungomc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa