• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
Ubungo Municipal Council
Ubungo Municipal Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Malengo na dhamira
    • Maadili ya Msingi
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Elimu Sekondari
      • Agriculture, Livestock and Fisheries
      • Industry,Trade and Investments
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure, Rural and Urban Development
      • Pre-Primary and Primary Education
      • Human Resources Management and administration
      • Health, Social Welfare and Nutrition Services
      • Communit Development
    • Vitengo
      • Legal Services
      • Ukaguzi wa ndani
      • TEHAMA
      • Procument Management
      • Government Communication
      • Finance and Accounts
      • Sports, Culture and Arts
      • Waste Management and Sanitation
      • Natural Resources and Environment Conservation
    • Sheria ndogo ndogo za Manispaa
      • Sheria ndogo ndogo za Manispaa
      • Other Laws
  • Fursa za Uwekezaji
    • Ufugaji
    • Kilimo
    • Masoko
    • Vituo vya Basi
    • Viwanda
  • Huduma zetu
    • Afya
      • iCHF
      • Lishe
      • Social welfare
    • Elimu
      • Pre and Primary Education
      • Elimu Sekondari
    • Biashara
      • Ushuru wa Huduma
      • Usajili wa Tax
      • Leseni za Biashara
      • Ushuru wa Hoteli
    • Ujasiliamali
      • Ten Percent Loans
    • Kilimo
    • Uvuvi
    • Ufugaji
      • UJUWA
  • Madiwani
    • Orodha za Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za kudumu
    • Ratiba za vikao vya kisheria
    • Ratiba ya Kumuona Meya
  • Miradi
    • Miradi iliyopangwa
    • Miradi endelevu
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Fomu za Maombi
    • Ripoti
    • Sheria
    • Bronchures
    • Zabuni iliyotangazwa
    • Mpango Mkakati
    • Newsletter
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Hotuba

BILIONI 2 KUJENGA MADARASA 100 UBUNGO

Posted on: August 14th, 2021

Ni maandalizi ya kuwapokea wanafunzi wa darasa la Kwanza na kidato cha kwanza mwaka 2022.

Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo inatarajia kutumia shilingi bilioni 2 fedha za mapato ya ndani kujenga na kukarabati vyumba vya madarasa 100 kwa shule za Msingi na Sekondari za Manispaa hiyo ikiwa ni maandalizi ya kuwapokea wananfunzi wa darasa la kwanza na kidato cha kwanza mwaka ujao wa 2022.

Ujenzi huo wa vyumba 100 vya madarasa unaotarajia kuanza Agosti mwaka huu na kukamilika Novemba 20, 2021, unalenga kuboresha miundombinu ya shule na hivyo kuwana mazingira bora ya kujifunza na kujifunzia.

Akizungumza na Walimu Wakuu na Wakuu wa Shule  kwenye kikao kazi kuhusu utekelezaji wa mpango huo kwa kwaka wa fedha 2021/2022, Mkurugenzi wa Manispaa hiyo Beatrice Dominic  amewataka wasimamizi wa miradi hiyo kufanya kazi kwa ushirikiano na umakini mkubwa huku wakifuata kanuni, taratibu na miongozo ya serikali katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

Beatrice amewaeleza wasimamizi wa miradi hiyo kuwa, Miradi hiyo inajengwa kwa kufuata mwongozo wa “Force account”  hivyo  wahakikishe wanauzingatia vizuri hususani kununua vifaa viwandani pamoja na kuwa na watoa huduma tofauti tofauti  wa vifaa ili kupunguza gharama ya mradi lakini kupata vifaa kwa wakati.

“hili zoezi ni la kimkakati hivyo tujipange kulitekeleza kwa wakati, uadilifu na kuzingatia taratibu na mwongozo ili ifikapo Novemba 2021 miradi yote iwe imekamilika”alisisitiza Beatrice

Akiwasilisha Mpango wa ujenzi wa miundombinu hiyo, Mkuu wa Idara ya Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji ndugu, Salvius F.  Nkwera ameeleza kuwa katika bajeti ya mwaka huu wa fedha, Manispaa imetenga jumla ya shilingi bilioni 3.5 kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya shule na huduma za afya ambapo bilioni 2 ni kwa ajili ya madarasa na bilioni 1.5 ni kwa ajili ya ujenzi wa vituo  3 vya afya.

Aliendelea kueleza kuwa, Ujenzi wa miundombinu ya shule ni kati ya vipaumbele kumi vitakavyotekelezwa kwenye bajeti ya mwaka fedha 2021/22 kwa kutumia fedha za mapato ya ndani kama sehemu ya kuboresha utoaji huduma kwa wananchi wake.

Taarifa

  • KIBALI CHA KUANZA KUTOZA USHURU WA KUSHUSHA NA KUPAKIA MIZIGO July 17, 2023
  • KUKANUSHA TAARIFA YA UWEPO WA HARAFU MBAYA STENDI YA MABASI MAGUFULI July 06, 2023
  • MATOKEO YA SENSA YA WATU NA MAKAZI 2022 Ubungo September 06, 2023
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI NAFASI YA DEREVA NA KATIBU MAHSUSI July 21, 2022
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MAAFISA HABARI HAKIKISHENI MNATANGAZA UTEKELEZAJI WA MIRADI KWA WANANCHI

    May 24, 2025
  • CRDB WAMKARIBISHA DC MSANDO KWA KUTOA MADAWATI 30 NA VIFAA VYA MICHEZO

    May 22, 2025
  • MAFUNZO KWA WATENDAJI NGAZI YA KATA KUHUSU UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA AWAMU YA PILI.

    May 14, 2025
  • NI LAZIMA UJENZI WA UKUTA UANZE NA KUKAMILIKA" DC MSANDO

    May 12, 2025
  • Tazama zote

Video

KIWANJA CHAKO KINA HATI? | UMEKUWA UKISUMBULIWA NA MIGOGORO YA ARDHI? | KARIBU KWENYE ARDHI CLINIC
More Videos

Viunganishi vya haraka

  • Leseni za biashara
  • Ushuru wa Hoteli
  • Kibali cha ujenzi
  • Sheria ndogondogo
  • Malengo na Dira
  • Muundo wa Uongozi
  • zabuni

Viunganishi linganifu

  • The National Examinations Council of Tanzania
  • TAMISEMI
  • Ministry of Education
  • President office State House
  • National Council for Technical Education
  • Ministry of Finace and Planning

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya wanaoingia

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Luguruni Area, Morogoro Road

    Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam

    Telephone: +255 22 2926341

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: md@ubungomc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa