• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
Ubungo Municipal Council
Ubungo Municipal Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Malengo na dhamira
    • Maadili ya Msingi
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Elimu Sekondari
      • Agriculture, Livestock and Fisheries
      • Industry,Trade and Investments
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure, Rural and Urban Development
      • Pre-Primary and Primary Education
      • Human Resources Management and administration
      • Health, Social Welfare and Nutrition Services
      • Communit Development
    • Vitengo
      • Legal Services
      • Ukaguzi wa ndani
      • TEHAMA
      • Procument Management
      • Government Communication
      • Finance and Accounts
      • Sports, Culture and Arts
      • Waste Management and Sanitation
      • Natural Resources and Environment Conservation
    • Sheria ndogo ndogo za Manispaa
      • Sheria ndogo ndogo za Manispaa
      • Other Laws
  • Fursa za Uwekezaji
    • Ufugaji
    • Kilimo
    • Masoko
    • Vituo vya Basi
    • Viwanda
  • Huduma zetu
    • Afya
      • iCHF
      • Lishe
      • Social welfare
    • Elimu
      • Pre and Primary Education
      • Elimu Sekondari
    • Biashara
      • Ushuru wa Huduma
      • Usajili wa Tax
      • Leseni za Biashara
      • Ushuru wa Hoteli
    • Ujasiliamali
      • Ten Percent Loans
    • Kilimo
    • Uvuvi
    • Ufugaji
      • UJUWA
  • Madiwani
    • Orodha za Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za kudumu
    • Ratiba za vikao vya kisheria
    • Ratiba ya Kumuona Meya
  • Miradi
    • Miradi iliyopangwa
    • Miradi endelevu
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Fomu za Maombi
    • Ripoti
    • Sheria
    • Bronchures
    • Zabuni iliyotangazwa
    • Mpango Mkakati
    • Newsletter
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Hotuba

CLINIKI TEMBEZI YA UPIMAJI WA KIFUA KIKUU BURE UBUNGO, 29 WABAINIKA

Posted on: November 1st, 2023

Katika kuhakikisha Mpango wa Taifa wa  kutokomeza Kifua kikuu na ukoma,  Manispaa ya Ubungo kwa kushirikiana na Amref Afya shirikishi inaendesha zoezi la upimaji na utambuzi wa kifua kikuu katika Manispaa hiyo kupitia Klinik Tembezi lengo ikiwa ni kuwasogezea karibu huduma wananchi

Zoezi hilo linalofanyika kwa muda wa siku 4 lilianza oktoba 30,2023 katika kituo kikuu cha mabasi cha magufuli na litamalizika novemba 2, 2023 katika soko la ndizi Mabibo ambapo hadi sasa jumla ya watu 329 wamepimwa na kati ya hao 29 wamegundulika na TB na wameanzishiwa huduma ya matibabu

Mratibu wa zoezi hilo Dkt Sophia Kisoma ni mratibu wa Kifua kikuu na Ukoma katika Hospitali ya Sinza  Palestina, amesema kuwa mwitikio wa wananchi wa kutaka kupima Ugonjwa huo ni mzuri na wale wanaopatikana na ugonjwa wanaanzishiwa matibabu haraka sana.

Dkt Kisoma anasema "Mgonjwa anayepatikana na Kifua kikuu tunakaa nae muda mrefu ambapo muda wa chini kabisa ni miezi sita kwa maana ya matibabu lakini wengine wanapata matiba mpaka miaka miwili hivyo tunapenda watu wawe na utamaduni wa kucheki afya zao mara kwa mara ili kupata matibabu mapema"

Aidha, Dkt Kisoma anaeleza kuwa ugonjwa  wa Kifua kikuu unasambaa kwa njia ya hewa na upimaji wake unafanyika kwa kufanya uchunguzi kwa njia ya mionzi (x-ray) na  kupima sampuli ya mahohozi kwenye machine ya kupima vina saba ambapo katiza zoezi hili vipimo ni bure , hivyo wananchi wajitokeze kupata huduma hiyo.

Aliendelea kusema kuwa Manispaa ya Ubungo kupitia watoa huduma ngazi ya jamii imeendelea kutoa elimu kwa wananchi juu ya Ugonjwa huu na wagonjwa waliopatikana na mambukizi wamekuwa wakipelekwa kwenye vituo ambavyo viko karibu makazi yao ili wapate huduma kwa urahisi

Mtoa huduma ngazi ya jamii Ndg.Dickson Abdallah alisema kuwa katika kuhakikisha wananchi wanapata elimu kuhusiana na Kifua kikuu huwa tunatembelea  wananchi mtaani na kuwapa elimu na huduma ya upimaji bure na baada ya  upimaji huwa wanawapeleka hospitali au kituo cha afya kwa ajili ya kuanza kupatiwa dawa kwa wale wanakutwa na ugonjwa huo


Pichani ni wananchi waliojitokeza kupata huduma ya upimaji wa kifua kikuu katika Clinik tembezi

Taarifa

  • KIBALI CHA KUANZA KUTOZA USHURU WA KUSHUSHA NA KUPAKIA MIZIGO July 17, 2023
  • KUKANUSHA TAARIFA YA UWEPO WA HARAFU MBAYA STENDI YA MABASI MAGUFULI July 06, 2023
  • MATOKEO YA SENSA YA WATU NA MAKAZI 2022 Ubungo September 06, 2023
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI NAFASI YA DEREVA NA KATIBU MAHSUSI July 21, 2022
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • KATA YA UBUNGO YAKABIDHI MKOPO WA TSH. 122,800,000/= KWA VIKUNDI SITA VYA ASILIMIA 10

    May 02, 2025
  • KAMPENI YA KATAA UCHAFU, SAFISHA, PENDESHA UBUNGO YAZINDULIWA, MITAA SAFI NA MICHAFU KUPEWA ZAWADI

    May 03, 2025
  • FANYENI KAZI, MSIJALI MASILAHI BINAFSI" ~ CHALAMILA

    May 01, 2025
  • HUDUMA YA KUJIFUNGUA KWA UPASUAJI YAANZA RASMI KITUO CHA AFYA GOBA,WANANCHI WAKARIBISHWA

    April 30, 2025
  • Tazama zote

Video

KIWANJA CHAKO KINA HATI? | UMEKUWA UKISUMBULIWA NA MIGOGORO YA ARDHI? | KARIBU KWENYE ARDHI CLINIC
More Videos

Viunganishi vya haraka

  • Leseni za biashara
  • Ushuru wa Hoteli
  • Kibali cha ujenzi
  • Sheria ndogondogo
  • Malengo na Dira
  • Muundo wa Uongozi
  • zabuni

Viunganishi linganifu

  • The National Examinations Council of Tanzania
  • TAMISEMI
  • Ministry of Education
  • President office State House
  • National Council for Technical Education
  • Ministry of Finace and Planning

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya wanaoingia

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Luguruni Area, Morogoro Road

    Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam

    Telephone: +255 22 2926341

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: md@ubungomc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa