• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
Ubungo Municipal Council
Ubungo Municipal Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Malengo na dhamira
    • Maadili ya Msingi
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Elimu Sekondari
      • Agriculture, Livestock and Fisheries
      • Industry,Trade and Investments
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure, Rural and Urban Development
      • Pre-Primary and Primary Education
      • Human Resources Management and administration
      • Health, Social Welfare and Nutrition Services
      • Communit Development
    • Vitengo
      • Legal Services
      • Ukaguzi wa ndani
      • TEHAMA
      • Procument Management
      • Government Communication
      • Finance and Accounts
      • Sports, Culture and Arts
      • Waste Management and Sanitation
      • Natural Resources and Environment Conservation
    • Sheria ndogo ndogo za Manispaa
      • Sheria ndogo ndogo za Manispaa
      • Other Laws
  • Fursa za Uwekezaji
    • Ufugaji
    • Kilimo
    • Masoko
    • Vituo vya Basi
    • Viwanda
  • Huduma zetu
    • Afya
      • iCHF
      • Lishe
      • Social welfare
    • Elimu
      • Pre and Primary Education
      • Elimu Sekondari
    • Biashara
      • Ushuru wa Huduma
      • Usajili wa Tax
      • Leseni za Biashara
      • Ushuru wa Hoteli
    • Ujasiliamali
      • Ten Percent Loans
    • Kilimo
    • Uvuvi
    • Ufugaji
      • UJUWA
  • Madiwani
    • Orodha za Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za kudumu
    • Ratiba za vikao vya kisheria
    • Ratiba ya Kumuona Meya
  • Miradi
    • Miradi iliyopangwa
    • Miradi endelevu
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Fomu za Maombi
    • Ripoti
    • Sheria
    • Bronchures
    • Zabuni iliyotangazwa
    • Mpango Mkakati
    • Newsletter
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Hotuba

CWT UBUNGO YAWAPIGA MSASA WALIMU NA WARATIBU WA ELIMU KATA

Posted on: February 10th, 2022


Chama cha walimu Ubungo kwa kushirikiana na Manispaa ya Ubungo leo tarehe 10/02/2022 kimekutana na maafisa elimu kata na walimu wakuu wa shule za msingi na sekondari lengo ikiwa ni kuwapa mafunzo ya kuwa viongozi bora kwa maana ya kuboresha na kuongeza ufaulu mashuleni.


Katibu wa chama cha walimu Ubungo, Maisa Joseph amewataka walimu hao kuwa na uongozi bora na mawasiliano mazuri baina yao na wanaowasimamia ili kuongeza ufaulu kwa wanafunzi na kuiwezesha kuwa katika ufaulu wa kumi bora Nchini.


Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo, Selemani Kateti (Mkuu wa Idara ya Utumishi na Utawala) amekipongeza chama cha walimu kwa namna wanavyoweza  kushirikiana vyema na serikali katika kuhakikisha maslahi ya walimu wanafuatwa na amewaomba wawe na ofisi ndani ya Manispaa ili kuendelea kushirikiana vizuri zaidi.


Kateti amewasisitiza walimu na waratibu hao wa elimu kuwajibika ipaswavyo katika kutekeleza majukumu yao na kuwajibika katika kusimamia miradi mbalimbali ya maendeleo katika shule zao kwa kushirikisha walimu na wadau wengine shuleni hapo. Na kuwasimamia walimu wanaowasimamia kutimiza majukumu yao ipaswavyo.


“Kunawajibu kama kiongozi katika kusimamia majukumu yako ukiwa kama kiongozi wa serikali wa eneo Fulani.”


Aidha Kateti ameeleza kwamba katika kuhakikisha maslahi ya walimu yanafuatwa atahakikisha kila mtumishi mwenye sifa za kupanda daraja, kubadilishwa muundo yote yatafanyika sambamba na ubadilishwaji wa mishahara ili kuepuka malimbikizo kwa watumishi, na kuwaondolea mlolongo mrefu wa kupitishiwa fomu za mikopo.


Kateti amewataka walimu hao kuhakikisha taaluma inapanda kwa kuhakikisha ufaulu unaongezeka mashuleni na hicho ni kipimo cha kupima uwajibikaji wao katika kutekeleza majukumu yao, Pia amewataka walimu hao kuipa nguvu benki ya walimu ambayo ni kama wameisahau.


 Naye Mjumbe wa Kamati ya Utendaji Taifa ya chama cha walimu Mwalimu Nelson Mabula amempongeza Mkuu wa Idara ya Utumishi na Utawala kwa namna anavyojali maslahi ya watumishi na ameeleza kuwa walimu wote ambao walinyang’anywa vyeo serikali inaangalia namna ya kuwarudishia vyeo hivyo na amewataka walimu kufanya kazi kwa weledi kwa maslahi ya Umma.


Nae mwakilishi wa Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC) ya Wilaya Fides G Tairo ameeleza kuwa tume imejikita katika kusimamia nidhamu kwa walimu, na kwamba ameeleza mwalimu Mkuu ana mamlaka ya kumpa mwalimu anaemsimamia adhabu kwa kuzingatia kanuni, sheria na taratibu za Nchi, ili kuimarisha utaendaji kazi wao kwa maslahi ya Taifa.



Taarifa

  • KIBALI CHA KUANZA KUTOZA USHURU WA KUSHUSHA NA KUPAKIA MIZIGO July 17, 2023
  • KUKANUSHA TAARIFA YA UWEPO WA HARAFU MBAYA STENDI YA MABASI MAGUFULI July 06, 2023
  • MATOKEO YA SENSA YA WATU NA MAKAZI 2022 Ubungo September 06, 2023
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI NAFASI YA DEREVA NA KATIBU MAHSUSI July 21, 2022
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MAAFISA HABARI HAKIKISHENI MNATANGAZA UTEKELEZAJI WA MIRADI KWA WANANCHI

    May 24, 2025
  • CRDB WAMKARIBISHA DC MSANDO KWA KUTOA MADAWATI 30 NA VIFAA VYA MICHEZO

    May 22, 2025
  • MAFUNZO KWA WATENDAJI NGAZI YA KATA KUHUSU UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA AWAMU YA PILI.

    May 14, 2025
  • NI LAZIMA UJENZI WA UKUTA UANZE NA KUKAMILIKA" DC MSANDO

    May 12, 2025
  • Tazama zote

Video

KIWANJA CHAKO KINA HATI? | UMEKUWA UKISUMBULIWA NA MIGOGORO YA ARDHI? | KARIBU KWENYE ARDHI CLINIC
More Videos

Viunganishi vya haraka

  • Leseni za biashara
  • Ushuru wa Hoteli
  • Kibali cha ujenzi
  • Sheria ndogondogo
  • Malengo na Dira
  • Muundo wa Uongozi
  • zabuni

Viunganishi linganifu

  • The National Examinations Council of Tanzania
  • TAMISEMI
  • Ministry of Education
  • President office State House
  • National Council for Technical Education
  • Ministry of Finace and Planning

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya wanaoingia

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Luguruni Area, Morogoro Road

    Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam

    Telephone: +255 22 2926341

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: md@ubungomc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa