• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
Ubungo Municipal Council
Ubungo Municipal Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Malengo na dhamira
    • Maadili ya Msingi
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Elimu Sekondari
      • Agriculture, Livestock and Fisheries
      • Industry,Trade and Investments
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure, Rural and Urban Development
      • Pre-Primary and Primary Education
      • Human Resources Management and administration
      • Health, Social Welfare and Nutrition Services
      • Communit Development
    • Vitengo
      • Legal Services
      • Ukaguzi wa ndani
      • TEHAMA
      • Procument Management
      • Government Communication
      • Finance and Accounts
      • Sports, Culture and Arts
      • Waste Management and Sanitation
      • Natural Resources and Environment Conservation
    • Sheria ndogo ndogo za Manispaa
      • Sheria ndogo ndogo za Manispaa
      • Other Laws
  • Fursa za Uwekezaji
    • Ufugaji
    • Kilimo
    • Masoko
    • Vituo vya Basi
    • Viwanda
  • Huduma zetu
    • Afya
      • iCHF
      • Lishe
      • Social welfare
    • Elimu
      • Pre and Primary Education
      • Elimu Sekondari
    • Biashara
      • Ushuru wa Huduma
      • Usajili wa Tax
      • Leseni za Biashara
      • Ushuru wa Hoteli
    • Ujasiliamali
      • Ten Percent Loans
    • Kilimo
    • Uvuvi
    • Ufugaji
      • UJUWA
  • Madiwani
    • Orodha za Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za kudumu
    • Ratiba za vikao vya kisheria
    • Ratiba ya Kumuona Meya
  • Miradi
    • Miradi iliyopangwa
    • Miradi endelevu
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Fomu za Maombi
    • Ripoti
    • Sheria
    • Bronchures
    • Zabuni iliyotangazwa
    • Mpango Mkakati
    • Newsletter
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Hotuba

DC KOMBA AKABIDHI MADAWATI, VITI NA MEZA MASHULENI

Posted on: February 19th, 2024

Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Hashim Komba amezielekeza Kamati za Shule wilayani humo kuwa na Utamaduni wa kufanya ukarabati wa madawati yaliyochakaa ili kupunguza changamoto zinazoweza kujitokeza, ikiwemo wanafunzi kukaa chini kutokana na uchakavu wa Madawati hayo, badala ya kusubiri Ujenzi wa Madawati mapya yenye mchakato mrefu.

DC Komba ametoa maelekezo hayo wakati wa kukabidhi Madawati 100 Kwa Shule ya Msingi Makoka ambayo Ina Upungufu wa Madawati 140, hali iliyotokana na ongezeko kubwa la wanafunzi katika Shule nyingi za Msingi za Serikali, kutokana na Sera ya elimu bure.

"Nimepita leo kujiridhisha kuona kama maelekezo ya Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan yanafanyiwa kazi ya kutaka watoto wetu wasikae chini, wakati tunakagua maandalizi ya kupokea wanafunzi kwa mwaka 2024 tulikubaliana kwa upande wa Idara ya Elimu Sekondari kuchonga Viti na Meza 7,339, Kwa upande wa Idara ya Elimu Msingi tulikubaliana kuchonga Madawati 4,000," Alisema Mhe. Komba.

Mhe. Komba amekabidhi Madawati 100 Kwa Shule ya Msingi Makoka, Viti na Meza 200 kwa Shule ya Sekondari Mugabe iliyopo Sinza na kutembelea katika karakana zinazotengenezewa Viti hivyo na Madawati ambapo mkandarasi anaendelea na Ujenzi, huku akitoa maelekezo ya kwamba kasi ya ujenzi huo iongezeke.

Akizungumza baada ya kukabidhiwa Madawati hayo Afisa Elimu Msingi Manispaa ya Ubungo Dennis Nyoni amesema hadi Sasa Madawati 1,660 ya yameshasambazwa kwenye Shule mbalimbali za Msingi Kwa awamu ya kwanza Kwa kushirikiana na wadau mbalimbali na kwa awamu ya pili yatatengenezwa zaidi ya Madawati 7,000, huku Shilingi Milioni 500 zikiwa zimetengwa kwa awamu hiyo ya kwanza, na mwaka wa Fedha ujao imetengwa Milioni 700 itakayosaidia zaidi ya wanafunzi 16,000 walioandikishwa kupata mazingira bora ya kusomea.

Kwa upande wake, Afisa Elimu Sekondari Manispaa ya Ubungo Voster Mgina amesema jumla ya Shule 36 ambazo Zina wanafunzi 41,200 katika Manispaa hiyo, zilikuwa na Upungufu wa Viti na Meza 17,000, lakini Manispaa kwa awamu ya kwanza imetengua Milioni 700 kwa ajili ya Viti na Meza 7,339, na Hadi Sasa Viti na Meza 2,700 Vimekamilika na kusambazwa.















Taarifa

  • KIBALI CHA KUANZA KUTOZA USHURU WA KUSHUSHA NA KUPAKIA MIZIGO July 17, 2023
  • KUKANUSHA TAARIFA YA UWEPO WA HARAFU MBAYA STENDI YA MABASI MAGUFULI July 06, 2023
  • MATOKEO YA SENSA YA WATU NA MAKAZI 2022 Ubungo September 06, 2023
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI NAFASI YA DEREVA NA KATIBU MAHSUSI July 21, 2022
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MAAFISA HABARI HAKIKISHENI MNATANGAZA UTEKELEZAJI WA MIRADI KWA WANANCHI

    May 24, 2025
  • CRDB WAMKARIBISHA DC MSANDO KWA KUTOA MADAWATI 30 NA VIFAA VYA MICHEZO

    May 22, 2025
  • MAFUNZO KWA WATENDAJI NGAZI YA KATA KUHUSU UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA AWAMU YA PILI.

    May 14, 2025
  • NI LAZIMA UJENZI WA UKUTA UANZE NA KUKAMILIKA" DC MSANDO

    May 12, 2025
  • Tazama zote

Video

KIWANJA CHAKO KINA HATI? | UMEKUWA UKISUMBULIWA NA MIGOGORO YA ARDHI? | KARIBU KWENYE ARDHI CLINIC
More Videos

Viunganishi vya haraka

  • Leseni za biashara
  • Ushuru wa Hoteli
  • Kibali cha ujenzi
  • Sheria ndogondogo
  • Malengo na Dira
  • Muundo wa Uongozi
  • zabuni

Viunganishi linganifu

  • The National Examinations Council of Tanzania
  • TAMISEMI
  • Ministry of Education
  • President office State House
  • National Council for Technical Education
  • Ministry of Finace and Planning

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya wanaoingia

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Luguruni Area, Morogoro Road

    Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam

    Telephone: +255 22 2926341

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: md@ubungomc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa