• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
Ubungo Municipal Council
Ubungo Municipal Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Malengo na dhamira
    • Maadili ya Msingi
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Elimu Sekondari
      • Agriculture, Livestock and Fisheries
      • Industry,Trade and Investments
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure, Rural and Urban Development
      • Pre-Primary and Primary Education
      • Human Resources Management and administration
      • Health, Social Welfare and Nutrition Services
      • Communit Development
    • Vitengo
      • Legal Services
      • Ukaguzi wa ndani
      • TEHAMA
      • Procument Management
      • Government Communication
      • Finance and Accounts
      • Sports, Culture and Arts
      • Waste Management and Sanitation
      • Natural Resources and Environment Conservation
    • Sheria ndogo ndogo za Manispaa
      • Sheria ndogo ndogo za Manispaa
      • Other Laws
  • Fursa za Uwekezaji
    • Ufugaji
    • Kilimo
    • Masoko
    • Vituo vya Basi
    • Viwanda
  • Huduma zetu
    • Afya
      • iCHF
      • Lishe
      • Social welfare
    • Elimu
      • Pre and Primary Education
      • Elimu Sekondari
    • Biashara
      • Ushuru wa Huduma
      • Usajili wa Tax
      • Leseni za Biashara
      • Ushuru wa Hoteli
    • Ujasiliamali
      • Ten Percent Loans
    • Kilimo
    • Uvuvi
    • Ufugaji
      • UJUWA
  • Madiwani
    • Orodha za Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za kudumu
    • Ratiba za vikao vya kisheria
    • Ratiba ya Kumuona Meya
  • Miradi
    • Miradi iliyopangwa
    • Miradi endelevu
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Fomu za Maombi
    • Ripoti
    • Sheria
    • Bronchures
    • Zabuni iliyotangazwa
    • Mpango Mkakati
    • Newsletter
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Hotuba

KAMPENI YA UPIMAJI AFYA KWA HIARI "AFYA CHECK" YAZINDULIWA HOSPITALI YA WILAYA UBUNGO, HUDUMA 7 ZA KIBINGWA ZATOLEWA BURE

Posted on: January 23rd, 2025

Hospitali ya Wilaya ya Ubungo iliyopo Kimara Baruti kwa kushirikiana na kampuni ya utengenezaji wa dawa za binadamu Denk Pharma,  Januari 23, 2025 imezindua kampeni ya kupima afya inayojulikana kwa jina la “Afya Check” ikilenga kuwapatia wananchi huduma za kibingwa za upimaji wa magonjwa mbalimbali bure kwa siku mbili.

Kampeni hiyo imezinduliwa na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ubungo, Mh. Jafar Nyaigesha, ambaye aliwataka wananchi na wakazi wa Wilaya ya  Ubungo kujitokeza kwa wingi kupima afya zao ambapo alieleza kuwa  huduma hiyo itatolewa bure  bila malipo yoyote.

Alieleza kuwa takwimu zinaonyesha kuwa wanaume wengi bado hawajahamasika kupima afya kwa hiari na hivyo kukwamisha jitihada za Serikali ya awamu ya sita kujua hali ya afya za wananchi wake ambayo inasaidia Serikali  katika upangaji wa bajeti za wizara ya  afya.

“Napenda kutoa wito kwa wataalam wa sekta ya afya kuendelea kutoa elimu kwa wananchi kuhusu umuhimu wa kupima afya zao kwa manufaa ya mtu mmoja mmoja na hatimaye taifa kwa ujumla wake” alisema Mh. Nyaigesha

Katika hatua nyingine, Mh. Nyaigesha ameutaja Ushirikiano kati ya Hospitali ya Wilaya ya Ubungo na kampuni ya Denk Pharma kuwa mfano mzuri wa ushirikiano kati ya sekta ya afya na wadau wa maendeleo katika kuboresha hudumza za afya kwa jamii.

Kwa upande wake Mganga mkuu wa Manispaa ya Ubungo Dkt. Tulitweni Mwinuka alisema katika siku ya kwanza ya uzinduzi wa kampeni hiyo ya upimaji iliyozinduliwa katika hospitali ya wilaya ya Ubungo, watu 500 wamejitokeza na kupima afya zao na kupatiwa ushauri na wataalam wa afya huku akisema matarajio ni kufukia watu 900 hadi 1000 kwa siku zote mbili.

Huduma zinazotolewa bure katika kipindi hiki ni pamoja na Upimaji wa kisukari, Uchangiaji wa damu, Upimaji wa saratani ya matiti na shingo ya kizazi, Kupima na kudhibiti presha, Huduma za macho, Matibabu ya kinywa na meno, Kisukari, Kupima uzito na ushauri wa afya bora.

Hata hivyo, huduma hizi zinajumuisha ushauri wa kidaktari, elimu ya lishe bora, na matibabu bure kwa wananchi wote watakaohudhuria.

Taarifa

  • KIBALI CHA KUANZA KUTOZA USHURU WA KUSHUSHA NA KUPAKIA MIZIGO July 17, 2023
  • KUKANUSHA TAARIFA YA UWEPO WA HARAFU MBAYA STENDI YA MABASI MAGUFULI July 06, 2023
  • MATOKEO YA SENSA YA WATU NA MAKAZI 2022 Ubungo September 06, 2023
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI NAFASI YA DEREVA NA KATIBU MAHSUSI July 21, 2022
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • KATA YA UBUNGO YAKABIDHI MKOPO WA TSH. 122,800,000/= KWA VIKUNDI SITA VYA ASILIMIA 10

    May 02, 2025
  • KAMPENI YA KATAA UCHAFU, SAFISHA, PENDESHA UBUNGO YAZINDULIWA, MITAA SAFI NA MICHAFU KUPEWA ZAWADI

    May 03, 2025
  • FANYENI KAZI, MSIJALI MASILAHI BINAFSI" ~ CHALAMILA

    May 01, 2025
  • HUDUMA YA KUJIFUNGUA KWA UPASUAJI YAANZA RASMI KITUO CHA AFYA GOBA,WANANCHI WAKARIBISHWA

    April 30, 2025
  • Tazama zote

Video

KIWANJA CHAKO KINA HATI? | UMEKUWA UKISUMBULIWA NA MIGOGORO YA ARDHI? | KARIBU KWENYE ARDHI CLINIC
More Videos

Viunganishi vya haraka

  • Leseni za biashara
  • Ushuru wa Hoteli
  • Kibali cha ujenzi
  • Sheria ndogondogo
  • Malengo na Dira
  • Muundo wa Uongozi
  • zabuni

Viunganishi linganifu

  • The National Examinations Council of Tanzania
  • TAMISEMI
  • Ministry of Education
  • President office State House
  • National Council for Technical Education
  • Ministry of Finace and Planning

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya wanaoingia

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Luguruni Area, Morogoro Road

    Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam

    Telephone: +255 22 2926341

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: md@ubungomc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa