• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
Ubungo Municipal Council
Ubungo Municipal Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Malengo na dhamira
    • Maadili ya Msingi
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Elimu Sekondari
      • Agriculture, Livestock and Fisheries
      • Industry,Trade and Investments
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure, Rural and Urban Development
      • Pre-Primary and Primary Education
      • Human Resources Management and administration
      • Health, Social Welfare and Nutrition Services
      • Communit Development
    • Vitengo
      • Legal Services
      • Ukaguzi wa ndani
      • TEHAMA
      • Procument Management
      • Government Communication
      • Finance and Accounts
      • Sports, Culture and Arts
      • Waste Management and Sanitation
      • Natural Resources and Environment Conservation
    • Sheria ndogo ndogo za Manispaa
      • Sheria ndogo ndogo za Manispaa
      • Other Laws
  • Fursa za Uwekezaji
    • Ufugaji
    • Kilimo
    • Masoko
    • Vituo vya Basi
    • Viwanda
  • Huduma zetu
    • Afya
      • iCHF
      • Lishe
      • Social welfare
    • Elimu
      • Pre and Primary Education
      • Elimu Sekondari
    • Biashara
      • Ushuru wa Huduma
      • Usajili wa Tax
      • Leseni za Biashara
      • Ushuru wa Hoteli
    • Ujasiliamali
      • Ten Percent Loans
    • Kilimo
    • Uvuvi
    • Ufugaji
      • UJUWA
  • Madiwani
    • Orodha za Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za kudumu
    • Ratiba za vikao vya kisheria
    • Ratiba ya Kumuona Meya
  • Miradi
    • Miradi iliyopangwa
    • Miradi endelevu
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Fomu za Maombi
    • Ripoti
    • Sheria
    • Bronchures
    • Zabuni iliyotangazwa
    • Mpango Mkakati
    • Newsletter
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Hotuba

LAAC YAIPONGEZA UBUNGO KWA USIMAMIZI WA MIRADI

Posted on: January 27th, 2024

Kamati ya kudumu ya Bunge ya hesabu za Serikali za Mitaa ‘LAAC’ imeipongeza Manispaa ya Ubungo kwa usimamizi wa utekelezaji wa Miradi ya afya.

Pongezi hizo wamezitoa leo tarehe 27/01/2024 walipokuwa kwenye ziara ya ukaguzi wa miradi ndani ya Manispaa ya Ubungo lengo ikiwa ikiwa ni kuona jinsi nidhamu na udhibiti wa fedha za Umma kwa kuzingatia thamani ya Fedha unazingatiwa.

Akiongea Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Stanslaus Shing’oma Mabula sambamba na pongezi hizo pia ameiagiza Manispaa hiyo kufanya jitihada za haraka za kuhakikisha utatuzi wa haraka juu ya suala la ardhi iliyovamiwa na wananchi wa eneo iliyojengwa Hospitali ya Wilaya hiyo.

Agizo hilo limetokana na uwepo wa baadhi ya wakazi wa mtaa wa Baruti ilipojengwa Hospitali hiyo ambapo Manispaa ilibaini eneo lenye ukubwa wa zaidi ya ekari 30 limevamiwa na wananchi wa eneo hilo huku ekari 5 pekee zikiwa zimetumika kwa ajili ya ujenzi wa Hospitali hiyo.

Akisoma taarifa ya ujenzi wa Hospitali hiyo Mkuu wa Idara ya Mipango na Uratibu Ndg. Andambike Kyomo amesema Hospitali imegharimu kiasi cha shilingi 3,781,000,000 zilizotengwa kwa ajili ya ujenzi na ununuzi wa vifaa tiba kati ya hizo shilingi 3,300,000,000 zilikuwa ni Fedha kutoka Serikali kuu na shilingi 481,000,000 zilikuwa ni Fedha za mapato ya ndani ya Manispaa

Kyomo ameendelea kueleza kuwa hadi sasa ujenzi wa Hospitali hiyo umejumuisha majengo 8 likiwemo OPD, mionzi, utawala, wodi ya wazazi, maabara, stoo ya dawa, jengo la kufulia kwa awamu ya kwanza, wodi ya kawaida na nyumba ya kufua umeme kwa awamu ya pili na hadi sasa majengo yote yamekwisha kamilika na yanatoa huduma.

Kwa awamu ya tatu inatarajiwa kujenga ghorofa litakalojumuisha chumba cha upasuaji, wodi za kulala wanaume, wanawake, watoto,  huduma za macho na neno ambapo awamu hii iko katika hatua ya kibali cha mchoro.

Kwa upande wake Naibu Waziri ofisi ya Rais TAMISEMI Festo Dugange ameitaka Manispaa hiyo kuhakikisha inatenga bajeti kwa ajili ya ujenzi wa njia ya kutembelea wagonjwa ‘walk ways’ sambamba na kuhakikisha upatikanaji wa vifaa vya Hospitali.

Manispaa ya Ubungo ina jumla ya vituo 280 vya kutolea huduma za Afya vya Umma, mashirika na binafsi.

Taarifa

  • KIBALI CHA KUANZA KUTOZA USHURU WA KUSHUSHA NA KUPAKIA MIZIGO July 17, 2023
  • KUKANUSHA TAARIFA YA UWEPO WA HARAFU MBAYA STENDI YA MABASI MAGUFULI July 06, 2023
  • MATOKEO YA SENSA YA WATU NA MAKAZI 2022 Ubungo September 06, 2023
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI NAFASI YA DEREVA NA KATIBU MAHSUSI July 21, 2022
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • KATA YA UBUNGO YAKABIDHI MKOPO WA TSH. 122,800,000/= KWA VIKUNDI SITA VYA ASILIMIA 10

    May 02, 2025
  • KAMPENI YA KATAA UCHAFU, SAFISHA, PENDESHA UBUNGO YAZINDULIWA, MITAA SAFI NA MICHAFU KUPEWA ZAWADI

    May 03, 2025
  • FANYENI KAZI, MSIJALI MASILAHI BINAFSI" ~ CHALAMILA

    May 01, 2025
  • HUDUMA YA KUJIFUNGUA KWA UPASUAJI YAANZA RASMI KITUO CHA AFYA GOBA,WANANCHI WAKARIBISHWA

    April 30, 2025
  • Tazama zote

Video

KIWANJA CHAKO KINA HATI? | UMEKUWA UKISUMBULIWA NA MIGOGORO YA ARDHI? | KARIBU KWENYE ARDHI CLINIC
More Videos

Viunganishi vya haraka

  • Leseni za biashara
  • Ushuru wa Hoteli
  • Kibali cha ujenzi
  • Sheria ndogondogo
  • Malengo na Dira
  • Muundo wa Uongozi
  • zabuni

Viunganishi linganifu

  • The National Examinations Council of Tanzania
  • TAMISEMI
  • Ministry of Education
  • President office State House
  • National Council for Technical Education
  • Ministry of Finace and Planning

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya wanaoingia

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Luguruni Area, Morogoro Road

    Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam

    Telephone: +255 22 2926341

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: md@ubungomc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa