• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
Ubungo Municipal Council
Ubungo Municipal Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Malengo na dhamira
    • Maadili ya Msingi
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Elimu Sekondari
      • Agriculture, Livestock and Fisheries
      • Industry,Trade and Investments
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure, Rural and Urban Development
      • Pre-Primary and Primary Education
      • Human Resources Management and administration
      • Health, Social Welfare and Nutrition Services
      • Communit Development
    • Vitengo
      • Legal Services
      • Ukaguzi wa ndani
      • TEHAMA
      • Procument Management
      • Government Communication
      • Finance and Accounts
      • Sports, Culture and Arts
      • Waste Management and Sanitation
      • Natural Resources and Environment Conservation
    • Sheria ndogo ndogo za Manispaa
      • Sheria ndogo ndogo za Manispaa
      • Other Laws
  • Fursa za Uwekezaji
    • Ufugaji
    • Kilimo
    • Masoko
    • Vituo vya Basi
    • Viwanda
  • Huduma zetu
    • Afya
      • iCHF
      • Lishe
      • Social welfare
    • Elimu
      • Pre and Primary Education
      • Elimu Sekondari
    • Biashara
      • Ushuru wa Huduma
      • Usajili wa Tax
      • Leseni za Biashara
      • Ushuru wa Hoteli
    • Ujasiliamali
      • Ten Percent Loans
    • Kilimo
    • Uvuvi
    • Ufugaji
      • UJUWA
  • Madiwani
    • Orodha za Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za kudumu
    • Ratiba za vikao vya kisheria
    • Ratiba ya Kumuona Meya
  • Miradi
    • Miradi iliyopangwa
    • Miradi endelevu
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Fomu za Maombi
    • Ripoti
    • Sheria
    • Bronchures
    • Zabuni iliyotangazwa
    • Mpango Mkakati
    • Newsletter
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Hotuba

MANISPAA YA UBUNGO YAKABIDHIWA MRADI NA TBA BAADA YA KUVUNJA MKATABA WA UJENZI

Posted on: October 3rd, 2020


 HALMASHAURI ya Manispaa ya Ubungo mkoani Dar es salaam leo tarehe 3 oktoba, 2020 imekabidhiwa mradi wa ujenzi wa jengo jipya la utawala linalojengwa katika  kata ya Kwembe Mtaa wa mji mpya  na Wakala wa Majengo Tanzania (TBA)  wenye thamani ya shilingi bilioni 6.2 baada ya kuvunja mkataba wa ujenzi Wa mradi huo tarehe 23 septemba mwaka huu  kutokana na kushindwa kukamilisha kwa wakati mradi huo.

Maamuzi hayo yamefikiwa leo  tarehe 3 oktoba, 2020 kwenye kikao cha pamoja kati ya wakala wa majengo Tanzania (TBA) na timu ya menejimenti ya manispaa ya Ubungo   kilichomtaka TBA kukabidhi mradi  huo kwa Manispaa ili atafutwe mkandarasi mwingine wa kumalizia kazi zilizobaki.

Halmashauri imefikia hatua ya kutaka kukabidhiwa mradi  huo baada ya mkandarasi huyo kushindwa kukamilisha mradi  kwa mujibu wa mkataba ambapo mradi huo ulipaswa kukamilika na kukabidhiwa januari 2020 tangu uliposainiwa desemba 2018, lakini hata baada ya kuongezewa muda wa zaidi ya miezi sita alishindwa kukamilisha mradi.

Akiongea kwenye kikao hicho Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Bibi Beatrice Dominic alisema kuwa baada ya kuongezewa muda wa kukamilisha mradi TBA walipaswa kukabidhi mradi tarehe 19 septemba, 2020 lakini bado hawakuwa wamemaliza kazi ndio maana  Manispaa iliamua kuvunja mkataba na leo mkandarasi "tunamtaka atukabidhi mradi ili tutafute mkandarasi mwingine wa kukamilisha mradi"

Beatrice amefafanua kuwa “ifahamike kuwa Halmashauri imeendelea kulipa kodi ya majengo ya ofisi yaliyopangwa katika maeneo tofauti jambo ambalo ni kinyume na maagizo ya serikali”

Aidha, Beatrice ameendelea kueleza adha wanayopata wananchi wakati wa kupata huduma mbalimbali   kwani ofisi zimetawanyika katika maeneo tofauti   “ndio maana tulifika maamuzi ya kuvunja mkataba na TBA na leo tumemtaka atukabidhi mradi kwani ameshindwa kutekeleza mradi kwa wakati"

Serikali iliamua kutoa fedha za ujenzi wa jengo hili ili kusogeza huduma karibu na wananchi, kucheleweshwa kwa maradi huu ni kwenda kinyume na agizo la serikali linalozitaka Halmashauri zote nchini kuwa katika maeneo yake ya utawala. Hadi kufikia sasa mradi umefikia asilimia 80

Kwa upande wao TBA wamekubaliana na uamuzi wa kukabidhi mradi kwa Halmashauri itafute mkandarasi mwingine kumalizia kazi zilizobaki 

Aidha Timu ya wataalamu imeundwa ili kufanya tathimini ya kazi zilizobaki kwa pamoja ili kutenda haki kwa kila upande

Watalaam kutoka wakala wa majengo Tanzania (TBA) na  Manispaa ya Ubungo wakikagua mradi wa ujenzi wa jengo la Utawala lililiokuwa linajengwa na TBA kabla ya kuvunjiwa mkataba leo tarehe 3 oktoba, 2020 katika ukumbi wa jengo hilo

 IMEANDALIWA NA;

Kitengo cha habari na uhususiano

Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo

Taarifa

  • KIBALI CHA KUANZA KUTOZA USHURU WA KUSHUSHA NA KUPAKIA MIZIGO July 17, 2023
  • KUKANUSHA TAARIFA YA UWEPO WA HARAFU MBAYA STENDI YA MABASI MAGUFULI July 06, 2023
  • MATOKEO YA SENSA YA WATU NA MAKAZI 2022 Ubungo September 06, 2023
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI NAFASI YA DEREVA NA KATIBU MAHSUSI July 21, 2022
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • KATA YA UBUNGO YAKABIDHI MKOPO WA TSH. 122,800,000/= KWA VIKUNDI SITA VYA ASILIMIA 10

    May 02, 2025
  • KAMPENI YA KATAA UCHAFU, SAFISHA, PENDESHA UBUNGO YAZINDULIWA, MITAA SAFI NA MICHAFU KUPEWA ZAWADI

    May 03, 2025
  • FANYENI KAZI, MSIJALI MASILAHI BINAFSI" ~ CHALAMILA

    May 01, 2025
  • HUDUMA YA KUJIFUNGUA KWA UPASUAJI YAANZA RASMI KITUO CHA AFYA GOBA,WANANCHI WAKARIBISHWA

    April 30, 2025
  • Tazama zote

Video

KIWANJA CHAKO KINA HATI? | UMEKUWA UKISUMBULIWA NA MIGOGORO YA ARDHI? | KARIBU KWENYE ARDHI CLINIC
More Videos

Viunganishi vya haraka

  • Leseni za biashara
  • Ushuru wa Hoteli
  • Kibali cha ujenzi
  • Sheria ndogondogo
  • Malengo na Dira
  • Muundo wa Uongozi
  • zabuni

Viunganishi linganifu

  • The National Examinations Council of Tanzania
  • TAMISEMI
  • Ministry of Education
  • President office State House
  • National Council for Technical Education
  • Ministry of Finace and Planning

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya wanaoingia

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Luguruni Area, Morogoro Road

    Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam

    Telephone: +255 22 2926341

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: md@ubungomc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa