• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
Ubungo Municipal Council
Ubungo Municipal Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Malengo na dhamira
    • Maadili ya Msingi
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Elimu Sekondari
      • Agriculture, Livestock and Fisheries
      • Industry,Trade and Investments
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure, Rural and Urban Development
      • Pre-Primary and Primary Education
      • Human Resources Management and administration
      • Health, Social Welfare and Nutrition Services
      • Communit Development
    • Vitengo
      • Legal Services
      • Ukaguzi wa ndani
      • TEHAMA
      • Procument Management
      • Government Communication
      • Finance and Accounts
      • Sports, Culture and Arts
      • Waste Management and Sanitation
      • Natural Resources and Environment Conservation
    • Sheria ndogo ndogo za Manispaa
      • Sheria ndogo ndogo za Manispaa
      • Other Laws
  • Fursa za Uwekezaji
    • Ufugaji
    • Kilimo
    • Masoko
    • Vituo vya Basi
    • Viwanda
  • Huduma zetu
    • Afya
      • iCHF
      • Lishe
      • Social welfare
    • Elimu
      • Pre and Primary Education
      • Elimu Sekondari
    • Biashara
      • Ushuru wa Huduma
      • Usajili wa Tax
      • Leseni za Biashara
      • Ushuru wa Hoteli
    • Ujasiliamali
      • Ten Percent Loans
    • Kilimo
    • Uvuvi
    • Ufugaji
      • UJUWA
  • Madiwani
    • Orodha za Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za kudumu
    • Ratiba za vikao vya kisheria
    • Ratiba ya Kumuona Meya
  • Miradi
    • Miradi iliyopangwa
    • Miradi endelevu
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Fomu za Maombi
    • Ripoti
    • Sheria
    • Bronchures
    • Zabuni iliyotangazwa
    • Mpango Mkakati
    • Newsletter
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Hotuba

MBUNGE WA JIMBO LA UBUNGO ATOA MOTISHA KWA WALIMU NA WANAFUNZI JIMBONI KWAKE

Posted on: January 29th, 2022

Mbunge wa Jimbo la Ubungo  Profesa Kitila Mkumbo amewapa motisha walimu wa Sekondari waliofaulisha somo la Hisabati kwa daraja A kwenye matokeo ya  wanafunzi wa kidato cha nne jimboni humo ambapo ni utekelezaji wa ahadi yake aliyoitoa mwezi Aprili 2021 ikiwa ni mkakati wa kuongeza ufaulu wa somo hilo

 

Akifafanua ahadi hizo Profesa Mkumbo  amesema, kila A moja mwalimu wa somo atapata Tsh 100,000, mwanafunzi aliyepata alama A atalipiwa Ada yote ya kidato cha tano na sita huku waliopata alama B watalipiwa nusu Ada pamoja na zawadi hizo amesema wanafunzi na walimu hao watapata fursa ya kwenda hifadhi ya Saadan kwa siku tatu .


Shule 6 zimefanikiwa kupata tuzo hizo ambazo ni Sekondari ya Urafiki imepata A moja, Mugabe imepata A moja, Mabibo imepata A tatu,  Mburahati imepata A tatu, Makurumla imepata A nne na Kimara imepata A 18.


Akieleza mafanikio ya mkakati huo mbele ya Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda ambae ndiye mgeni rasmi wa tukio hilo, wadau wa elimu, Madiwani, waalimu, wanafunzi na wazazi Profesa Mkumbo ameeleza kuwa mkakati huo umefanikiwa kwani ufaulu wa somo hilo  umeongezeka kutoka 11.6%  kwa matokeo ya mwaka 2020 hadi kufikia 16% kwa matokeo ya mwaka 2021


"Mkakati huu umefanikiwa kwa sababu  kwa matokeo ya mwaka 2020 hakukuwa na mwanafunzi aliyepata alama A lakini baada ya mkakati huu wa kuamua kuwapa motisha walimu, wanafunzi 30 wamepata daraja A na wanafunzi 31 wamepata daraja B kwa matokea ya mwaka 2021 wakati kwa matokeo ya mwaka 2020 wanafunzi 9 tu walifaulu kwa alama B pekee".


Profesa Mkumbo ameendelea kufafanua kuwa hakuna elimu bila mwalimu hivyo kumpa motisha mwalimu kunachochea kiu ya kufundisha ambapo matokeo yake yanaongeza ufaulu kwa kiasi kikubwa 


Kwa upande wake Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Profesa Adolf Mkenda amempongeza Profesa Kitila Mkumbo kwa mkakati wake uliozaa matunda ya kuongeza ufaulu somo hilo kwa kuwapa motisha walimu na kwamba serikali imebeba mkakati huo na itatoa ushirikiano katika kufanya utafiti wa kuongeza  ufaulu wa somo hilo unaotarajiwa kufanywa na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.








Taarifa

  • KIBALI CHA KUANZA KUTOZA USHURU WA KUSHUSHA NA KUPAKIA MIZIGO July 17, 2023
  • KUKANUSHA TAARIFA YA UWEPO WA HARAFU MBAYA STENDI YA MABASI MAGUFULI July 06, 2023
  • MATOKEO YA SENSA YA WATU NA MAKAZI 2022 Ubungo September 06, 2023
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI NAFASI YA DEREVA NA KATIBU MAHSUSI July 21, 2022
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • KATA YA UBUNGO YAKABIDHI MKOPO WA TSH. 122,800,000/= KWA VIKUNDI SITA VYA ASILIMIA 10

    May 02, 2025
  • KAMPENI YA KATAA UCHAFU, SAFISHA, PENDESHA UBUNGO YAZINDULIWA, MITAA SAFI NA MICHAFU KUPEWA ZAWADI

    May 03, 2025
  • FANYENI KAZI, MSIJALI MASILAHI BINAFSI" ~ CHALAMILA

    May 01, 2025
  • HUDUMA YA KUJIFUNGUA KWA UPASUAJI YAANZA RASMI KITUO CHA AFYA GOBA,WANANCHI WAKARIBISHWA

    April 30, 2025
  • Tazama zote

Video

KIWANJA CHAKO KINA HATI? | UMEKUWA UKISUMBULIWA NA MIGOGORO YA ARDHI? | KARIBU KWENYE ARDHI CLINIC
More Videos

Viunganishi vya haraka

  • Leseni za biashara
  • Ushuru wa Hoteli
  • Kibali cha ujenzi
  • Sheria ndogondogo
  • Malengo na Dira
  • Muundo wa Uongozi
  • zabuni

Viunganishi linganifu

  • The National Examinations Council of Tanzania
  • TAMISEMI
  • Ministry of Education
  • President office State House
  • National Council for Technical Education
  • Ministry of Finace and Planning

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya wanaoingia

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Luguruni Area, Morogoro Road

    Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam

    Telephone: +255 22 2926341

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: md@ubungomc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa