• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
Ubungo Municipal Council
Ubungo Municipal Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Malengo na dhamira
    • Maadili ya Msingi
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Elimu Sekondari
      • Agriculture, Livestock and Fisheries
      • Industry,Trade and Investments
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure, Rural and Urban Development
      • Pre-Primary and Primary Education
      • Human Resources Management and administration
      • Health, Social Welfare and Nutrition Services
      • Communit Development
    • Vitengo
      • Legal Services
      • Ukaguzi wa ndani
      • TEHAMA
      • Procument Management
      • Government Communication
      • Finance and Accounts
      • Sports, Culture and Arts
      • Waste Management and Sanitation
      • Natural Resources and Environment Conservation
    • Sheria ndogo ndogo za Manispaa
      • Sheria ndogo ndogo za Manispaa
      • Other Laws
  • Fursa za Uwekezaji
    • Ufugaji
    • Kilimo
    • Masoko
    • Vituo vya Basi
    • Viwanda
  • Huduma zetu
    • Afya
      • iCHF
      • Lishe
      • Social welfare
    • Elimu
      • Pre and Primary Education
      • Elimu Sekondari
    • Biashara
      • Ushuru wa Huduma
      • Usajili wa Tax
      • Leseni za Biashara
      • Ushuru wa Hoteli
    • Ujasiliamali
      • Ten Percent Loans
    • Kilimo
    • Uvuvi
    • Ufugaji
      • UJUWA
  • Madiwani
    • Orodha za Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za kudumu
    • Ratiba za vikao vya kisheria
    • Ratiba ya Kumuona Meya
  • Miradi
    • Miradi iliyopangwa
    • Miradi endelevu
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Fomu za Maombi
    • Ripoti
    • Sheria
    • Bronchures
    • Zabuni iliyotangazwa
    • Mpango Mkakati
    • Newsletter
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Hotuba

MBUNGE WA UBUNGO AAHIDI KUSHUGHULIKIA KERO ZA WANANCHI

Posted on: December 27th, 2020

Mbunge  wa Jimbo la Ubungo  Prof. Kitila Mkumbo ambaye pia ni Waziri Ofisi ya Rais Uwekezaji amewahakikishia wananchi wa Jimbo hilo kushughulikia kero  zao  ikiwemo tatizo la barabara za mitaa, maji, elimu na afya kikamilifu ikiwa ni utekelezaji wa ahadi zake wakati wa kampeni.

Hayo ameyazungumza kwa wananchi wakati alipofanya Ziara  ya Siku nne katika kata za  Kimara, Manzese, Sinza ,Mabibo na Makulumla  kwa ajili ya kusikiliza kero  zao na kuweka mikakati ya  kuzitatua.

Aidha katika Ziara hiyo Prof. Kitila akipokea taarifa za utekelezaji wa miradi ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa barabara ya mavulunza na ujenzi wa Hospitali ya Sinza Palestina ambapo amepongeza utekelezaji wake na kuahidi kushirikiana nao kuhakikisha rasilimali fedha inapatikana ili miradi hiyo ikamilike ili wananchi waanze kupata huduma.

Mbunge wa Jimbo la Ubungo  Prof  Kitila Mkumbo (alievaa miwani) akiendelea na ziara ya kutambua kero za wananchi kata ya kimara. 

Prof Kitila amefafanua kuwa "Kukamilika kwa Miradi hii  kutaongeza ustawi wa wananchi mfano ujenzi wa hospitali ya sinza ambayo inahudumia wagonjwa kati ya 800 hadi 1000 kwa siku unapaswa kukamilika kwa haraka ili kurahisisha upatikanaji wa huduma bora kwa wananchi wetu"

Prof Kitila ameipongeza Manispaa ya Ubungo kwa kutoa fedha za mapato yake ya ndani zaidi ya shilingi milioni 100 kwa ajili ya  kupanua ujenzi wa hospitali hiyo huku serikali ikitoa shilingi milioni 200  kutokana na hospitali hiyo  hudumia wengi sana watu.

Akitoa taarifa hiyo mbele ya Mhe. Mbunge huyo, mganga Mkuu wa Manispaa Ubungo  Peter  Nsanya  alieleza kuwa, hospitali ya sinza palestina ilipandishwa hadhi  kutoka kituo cha afya na kuwa hospitali ya Wilaya mwaka 2016 wakati Manispaa ya Ubungo ilipoanzishwa kikimegwa kutoka Manispaa  ya kinondoni.

Aidha  Nsanya alisema kuwa kukamilika kwa hospitali hii kutapanua utoaji wa huduma za afya ikiwemo upatikanaji wa huduma za kibingwa ikiwemo upasuaji mkubwa tofauti na sasa ambapo upasuaji unaofanyika ni ya  uzazi pekee.

Katika Ziara hiyo Mhe Waziri alitembelea pia maeneo ya mto gide, bonde la mto china, na mto ng'ombe kujionea athari zinazosababishwa na mito hiyo kwa wananchi ikiwemo kubomboa makazi.

Pamoja na kwamba serikali imeendelea kuchukua hatua ya namna ya mito hiyo isiendelee kutela madhara kwa wananchi Prof Kitila amewaomba wananchi kuchukua hatua ikiwemo kuto jenga makazi au kufanya shughuli za kiuchumi karibu na mito ili kupunguza madhara yanayotokea sasa.

Mbunge wa Jimbo la Ubungo Prof Kitila Mkumbo ambaye pia ni waziri wa Uwekezaji akiongozana na viongozi mbalimbali kukagua athari za mto Ng'ombe  

Wakati wa Ziara hiyo, pia Mhe. Waziri alitembelea na kuzindua kazi mbalimbali za sana na michezo ikiwa ni moja ya sekta muhimu  inayowaingizia watu kipato  hususani vijana na kuwaeleza kuwa sekta hiyo ni nzuri kwani soko lake ni pana sana " hivyo mjitume na  mthamini kazi zenu kwani serikali pia inatambua mchango wenu kwa Taifa.


Taarifa

  • KIBALI CHA KUANZA KUTOZA USHURU WA KUSHUSHA NA KUPAKIA MIZIGO July 17, 2023
  • KUKANUSHA TAARIFA YA UWEPO WA HARAFU MBAYA STENDI YA MABASI MAGUFULI July 06, 2023
  • MATOKEO YA SENSA YA WATU NA MAKAZI 2022 Ubungo September 06, 2023
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI NAFASI YA DEREVA NA KATIBU MAHSUSI July 21, 2022
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • KATA YA UBUNGO YAKABIDHI MKOPO WA TSH. 122,800,000/= KWA VIKUNDI SITA VYA ASILIMIA 10

    May 02, 2025
  • KAMPENI YA KATAA UCHAFU, SAFISHA, PENDESHA UBUNGO YAZINDULIWA, MITAA SAFI NA MICHAFU KUPEWA ZAWADI

    May 03, 2025
  • FANYENI KAZI, MSIJALI MASILAHI BINAFSI" ~ CHALAMILA

    May 01, 2025
  • HUDUMA YA KUJIFUNGUA KWA UPASUAJI YAANZA RASMI KITUO CHA AFYA GOBA,WANANCHI WAKARIBISHWA

    April 30, 2025
  • Tazama zote

Video

KIWANJA CHAKO KINA HATI? | UMEKUWA UKISUMBULIWA NA MIGOGORO YA ARDHI? | KARIBU KWENYE ARDHI CLINIC
More Videos

Viunganishi vya haraka

  • Leseni za biashara
  • Ushuru wa Hoteli
  • Kibali cha ujenzi
  • Sheria ndogondogo
  • Malengo na Dira
  • Muundo wa Uongozi
  • zabuni

Viunganishi linganifu

  • The National Examinations Council of Tanzania
  • TAMISEMI
  • Ministry of Education
  • President office State House
  • National Council for Technical Education
  • Ministry of Finace and Planning

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya wanaoingia

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Luguruni Area, Morogoro Road

    Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam

    Telephone: +255 22 2926341

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: md@ubungomc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa