• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
Ubungo Municipal Council
Ubungo Municipal Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Malengo na dhamira
    • Maadili ya Msingi
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Elimu Sekondari
      • Agriculture, Livestock and Fisheries
      • Industry,Trade and Investments
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure, Rural and Urban Development
      • Pre-Primary and Primary Education
      • Human Resources Management and administration
      • Health, Social Welfare and Nutrition Services
      • Communit Development
    • Vitengo
      • Legal Services
      • Ukaguzi wa ndani
      • TEHAMA
      • Procument Management
      • Government Communication
      • Finance and Accounts
      • Sports, Culture and Arts
      • Waste Management and Sanitation
      • Natural Resources and Environment Conservation
    • Sheria ndogo ndogo za Manispaa
      • Sheria ndogo ndogo za Manispaa
      • Other Laws
  • Fursa za Uwekezaji
    • Ufugaji
    • Kilimo
    • Masoko
    • Vituo vya Basi
    • Viwanda
  • Huduma zetu
    • Afya
      • iCHF
      • Lishe
      • Social welfare
    • Elimu
      • Pre and Primary Education
      • Elimu Sekondari
    • Biashara
      • Ushuru wa Huduma
      • Usajili wa Tax
      • Leseni za Biashara
      • Ushuru wa Hoteli
    • Ujasiliamali
      • Ten Percent Loans
    • Kilimo
    • Uvuvi
    • Ufugaji
      • UJUWA
  • Madiwani
    • Orodha za Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za kudumu
    • Ratiba za vikao vya kisheria
    • Ratiba ya Kumuona Meya
  • Miradi
    • Miradi iliyopangwa
    • Miradi endelevu
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Fomu za Maombi
    • Ripoti
    • Sheria
    • Bronchures
    • Zabuni iliyotangazwa
    • Mpango Mkakati
    • Newsletter
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Hotuba

MBUNGE WA UBUNGO AFANYA KIKAO NA WATUMISHI WA MANISPAA YA UBUNGO, AAHIDI KUSHIRIKIANA NAO

Posted on: January 4th, 2021

Mhe. Mbunge wa Jimbo la Ubungo  ambaye pia ni Waziri wa Ofisi  ya Rais  Uwekezaji Prof. Kitila Mkumbo leo tarehe 4 januari, 2021, amefanya kikao na watumishi wa Manispaa ya Ubungo kilicholenga  kujua majukumu ya kila idara na vitengo  na kuweka mikakati ya namna ya kutatua kero za wananchi katika sekta mbalimbali.

Akizungumza na watumishi hao Mhe. Mbunge amesema, amelazimika kufanya kikao hicho  kupata uelewa wa utekelezajia wa  shughuli  mbalimbali zinazofanywa na Idara pamoja na vitengo ili kufahamu mipango  yao  katika kuhudumia wananchi  na changamoto zinazowakabili na hatimaye kuweka mikakati wa pamoja wa namna ya kuzitatua  

Wakuu wa Idara na vitengo wa Manispaa ya Ubungo wakimsikiliza kwa makini Mbunge wa jimbo la ubungo prof Kitila Mkumbo (hayupo pichani) alieleza mikakati ya kuboresha utoaji huduma kwa wananchi 


Prof Kitila  ameeleza kuwa "Kikao hiki kitanipa fursa ya kujua mipango yenu na wapi mnakwama ili kwa nafasi yangu nione tunashirikianaje  kupanga mikakati ambayo itasaidia kuwaletea maendeleo wananchi wa jimbo la ubungo kwa kutatua kero mbalimbali ikiwemo ubovu wa barabara za mitaa, elimu afya, maji na namna ya kutengeneza mazingira mazuri kwa wafanyabiashara wadogo na wakubwa sekta ambayo 50%  ya wakazi wa jimbo hilo wanaitegemea"

Prof. Kitila ameendelea kuwaeleza watumishi hao kuwa  hali ya  barabara nyingi za mitaa ndani ya jimbo la Ubungo ni mbaya hazipitiki muda wote na ndio kero ya kwanza kwa wananchi hivyo " kama manispaa kwa kishirikiana na tarura tuone namna ya kuanzisha mfumo ambao utawezesha barabara  za mitaa kufanyiwa matengenezo angalau kiwango cha changalawe ili ziweze kupitika muda  kwani wananchi wanateseka sana" 


Aidha prof Kitila  ameendelea kueleza kuwa uboreshaji wa upatikanaji  wa huduma za elimu, maji na afya utapapelekea kuitafsiri kwa vitendo ilani ya chama cha mapinduzi ambayo imejikita zaidi  kutatua kero za wananchi katika nyanja zote " nyinyi kama wataalamu mnapaswa kubuni mbinu za kitaalamu zinazolenga kupuguza kero hizo ili kujenga uaminifu kwa serikali yao"

Baadhi ya watendaji wa kata za Jimbo la Ubungo wakiwa kwenye kikao 

"Utoaji wa huduma bora unategemea upatikanaji wa fedha, hivyo tunapaswa kutengeneza mazingira mazuri ya kufanyia biashara  ikiwemo kuimarisha masoko yaliyopo pamoja kusimamia kwa makini ukusanyaji wa mapato kwenye vyanzo vyote vilivyoainishwa kwenye bajeti" anaelekeza prof  Kitila

Kwa upande wake Mkurugenzi  wa Manispaa ya Ubungo Beatrice Dominic ameeleza kuwa Manispaa  imekuwa ikitoa  fedha za mapato ya ndani kwa ajili ya kujenga miundombinu mbalimbali ikiwemo barabara, ujenzi wa madarasa, vituo vya kutolea huduma za afya na miundombinu mingine lengo likiwa ni kuhakikisha wananchi wanapata huduma mhimu.

Mkurugenzi  wa Manispaa ya Ubungo Beatrice Dominic akitoa ufafanuzi wa namna Manispaa inavyotekeleza shughuli mbalimbali kwenye kikao kati ya watumishi wa Manispaa hiyo na Mhe Mbunge wa Jimbo la Ubungo Prof Kitila Mkumbo.

"Kutokana na ongezeko la ufaulu wa wanafunzi wa kujiunga kidato cha kwanza, Manispaa imetoa  milioni  500 kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa 37 pamoja na madawati lengo ikiwa kuhakikisha wanafunzi wote waliofaulu hawapotezi  nafasi  ya kusoma kwa sababu ya ukosefu wa vyumba vya madarasa" ameeleza Beatrice 

Akichangia hoja kwenye kikao hicho, Afisa Elimu Msingi wa Manispaa hiyo  Abdul Buhety amempongeza Mhe. Mbunge kwa kufanya kikao  hicho ambacho kimempa fursa ya kujua utekelezaji wa shughuli mbalimbali  na kueleza mikakati ya pamoja ya namna ya kutatua kero mbalimbali kwa ustawi wa wananchi wa Jimbo hilo na Manispaa kwa ujumla.

Afisa Elimu Msingi wa Manispaa hiyo  Abdul Buhety( aliyesimama) akichangia hoja kwenye  kikao kati ya Mbunge wa Jimbo la Ubungo Prof Kitila Mkumbo na watumishi wa Manispaa hiyo  leo tarehe 04.01.2021 

Taarifa

  • KIBALI CHA KUANZA KUTOZA USHURU WA KUSHUSHA NA KUPAKIA MIZIGO July 17, 2023
  • KUKANUSHA TAARIFA YA UWEPO WA HARAFU MBAYA STENDI YA MABASI MAGUFULI July 06, 2023
  • MATOKEO YA SENSA YA WATU NA MAKAZI 2022 Ubungo September 06, 2023
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI NAFASI YA DEREVA NA KATIBU MAHSUSI July 21, 2022
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • KATA YA UBUNGO YAKABIDHI MKOPO WA TSH. 122,800,000/= KWA VIKUNDI SITA VYA ASILIMIA 10

    May 02, 2025
  • KAMPENI YA KATAA UCHAFU, SAFISHA, PENDESHA UBUNGO YAZINDULIWA, MITAA SAFI NA MICHAFU KUPEWA ZAWADI

    May 03, 2025
  • FANYENI KAZI, MSIJALI MASILAHI BINAFSI" ~ CHALAMILA

    May 01, 2025
  • HUDUMA YA KUJIFUNGUA KWA UPASUAJI YAANZA RASMI KITUO CHA AFYA GOBA,WANANCHI WAKARIBISHWA

    April 30, 2025
  • Tazama zote

Video

KIWANJA CHAKO KINA HATI? | UMEKUWA UKISUMBULIWA NA MIGOGORO YA ARDHI? | KARIBU KWENYE ARDHI CLINIC
More Videos

Viunganishi vya haraka

  • Leseni za biashara
  • Ushuru wa Hoteli
  • Kibali cha ujenzi
  • Sheria ndogondogo
  • Malengo na Dira
  • Muundo wa Uongozi
  • zabuni

Viunganishi linganifu

  • The National Examinations Council of Tanzania
  • TAMISEMI
  • Ministry of Education
  • President office State House
  • National Council for Technical Education
  • Ministry of Finace and Planning

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya wanaoingia

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Luguruni Area, Morogoro Road

    Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam

    Telephone: +255 22 2926341

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: md@ubungomc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa