• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
Ubungo Municipal Council
Ubungo Municipal Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Malengo na dhamira
    • Maadili ya Msingi
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Elimu Sekondari
      • Agriculture, Livestock and Fisheries
      • Industry,Trade and Investments
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure, Rural and Urban Development
      • Pre-Primary and Primary Education
      • Human Resources Management and administration
      • Health, Social Welfare and Nutrition Services
      • Communit Development
    • Vitengo
      • Legal Services
      • Ukaguzi wa ndani
      • TEHAMA
      • Procument Management
      • Government Communication
      • Finance and Accounts
      • Sports, Culture and Arts
      • Waste Management and Sanitation
      • Natural Resources and Environment Conservation
    • Sheria ndogo ndogo za Manispaa
      • Sheria ndogo ndogo za Manispaa
      • Other Laws
  • Fursa za Uwekezaji
    • Ufugaji
    • Kilimo
    • Masoko
    • Vituo vya Basi
    • Viwanda
  • Huduma zetu
    • Afya
      • iCHF
      • Lishe
      • Social welfare
    • Elimu
      • Pre and Primary Education
      • Elimu Sekondari
    • Biashara
      • Ushuru wa Huduma
      • Usajili wa Tax
      • Leseni za Biashara
      • Ushuru wa Hoteli
    • Ujasiliamali
      • Ten Percent Loans
    • Kilimo
    • Uvuvi
    • Ufugaji
      • UJUWA
  • Madiwani
    • Orodha za Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za kudumu
    • Ratiba za vikao vya kisheria
    • Ratiba ya Kumuona Meya
  • Miradi
    • Miradi iliyopangwa
    • Miradi endelevu
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Fomu za Maombi
    • Ripoti
    • Sheria
    • Bronchures
    • Zabuni iliyotangazwa
    • Mpango Mkakati
    • Newsletter
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Hotuba

MHE. KATAMBI APONGEZA VIKUNDI VYA VIJANA UBUNGO

Posted on: August 8th, 2022

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira,na Wenye ulemavu, Mhe. Patrobas Katambi ameadhimisha sikukuu ya Nanenane kwa kutembelea vikundi vya vijana vilivyopo Manispaa ya Ubungo ambavyo vimenufaika na mkopo wa 10% inayotokana na mapato ya ndani ya Manispaa hiyo ambapo amevipongeza vikundi hivyo kwa kutendea haki mikopo hiyo kwa kufanya uzalishaji wenye tija na kurejesha kwa wakati.

Katika ziara Mhe. Katambi ametembelea kikundi cha Umoja ni Nguvu kinachojihusisha na utengenezaji wa mapambo ya ndani kwa kutumia unga wa gypsum na kikundi cha BRIACO kinachojishughulisha na uzalishaji wa Kripsi za viazi mbatata na kueleza kuwa dhima ya Serikali ni kuona vijana wanajiajiri kwenye shughuli za uzalishaji wakisaidiwa na Halmashauri  kwa kuongezewa mikopo isiyo na riba kama sheria inavyoelekeza.

Mhe. Katambi ametaka vijana kuwa na malengo, kusudio na shabaha katika mipango kazi yao ili waweze kuzalisha bidha zenye  ushindani kwenye soko la ndani na nje, kujikwamua kiuchumi, kuzalisha ajira na kuanzisha  viwanda kwa kutumia elimu  na ujuzi waliyonao kwani vijana ndio nguvu kazi ya jamii na Taifa kwa ujumla.

Kutokana na utendaji kazi mzuri wa vikundi alivyotembelea ikiwemo kufanya marejesho kwa wakati, Mhe. Katambi ameielekeza Manispaa ya Ubungo kuviongezea kiwango cha mkopo vikundi hivyo kwenye maombi yao mengine ili viweze kuboresha na kuongeza uzalishaji wa bidhaa zao.

Aidha Mhe. Katambi ameeleza kuwa “Kwa mujibu wa takwimu za Sensa ya mwaka 2012, vijana wanakadiriwa kuwa nusu ya idadi ya watu wote kwa maana hiyo ni kundi muhimu lenye maarifa, ujuzi na usomi,nguvu kazi kwa ujumla hivyo sisi kama serikali lazima tuwekeze  nguvu katika kulisaidia kubadilisha mitazamo waliyonayo, kuwahudumia kulingana na mahitaji yao  ili waweze kujitegemea na kufanya majukumu ya kimaendeleo”

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Beatrice Dominic amevipongeza vikundi hivyo kwa kazi nzuri na kuahidi kuwaongezea nguvu ikiwemo kupata eneo la kudumu la kufanyia kazi, kutangaza bidhaa zao  pamoja na kutumia bidhaa (mapambo zinazotengenezwa na unga wa gypsum)   kwenye miradi ya Halmshauri.

Wakiongea kwa nyakati tofauti, wananvikundi wameshukuru kupata ugeni huo mkubwa na kuona kuwa wameheshimishwa na wameahidi kuendelea kufanya shughuli zao kwa weledi mkubwa ili kufikia malengo waliyojiwekea hususani kuwa wazalishaji wakubwa wa bidhaa hizo

Hadi kufikia Juni 2021/2022 Halmashauri ya Manispaa ya ubungo imekopesha jumla ya shilingi 7,559,514,415 kwa vikundi 1,350 vyenye wanufaika 10,163 ambapo kati ya vikundi hivyo vikundi vya wananwake ni 747 vimekopeshwa shilingi 3,834,437,630 vikundi vya vijana 537 vimekopeshwa shilingi 3, 190,926,785 na vikundi vya watu wenye ulemavu 66 vimekopesha shilingi 534,150,000.


Taarifa

  • KIBALI CHA KUANZA KUTOZA USHURU WA KUSHUSHA NA KUPAKIA MIZIGO July 17, 2023
  • KUKANUSHA TAARIFA YA UWEPO WA HARAFU MBAYA STENDI YA MABASI MAGUFULI July 06, 2023
  • MATOKEO YA SENSA YA WATU NA MAKAZI 2022 Ubungo September 06, 2023
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI NAFASI YA DEREVA NA KATIBU MAHSUSI July 21, 2022
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • KATA YA UBUNGO YAKABIDHI MKOPO WA TSH. 122,800,000/= KWA VIKUNDI SITA VYA ASILIMIA 10

    May 02, 2025
  • KAMPENI YA KATAA UCHAFU, SAFISHA, PENDESHA UBUNGO YAZINDULIWA, MITAA SAFI NA MICHAFU KUPEWA ZAWADI

    May 03, 2025
  • FANYENI KAZI, MSIJALI MASILAHI BINAFSI" ~ CHALAMILA

    May 01, 2025
  • HUDUMA YA KUJIFUNGUA KWA UPASUAJI YAANZA RASMI KITUO CHA AFYA GOBA,WANANCHI WAKARIBISHWA

    April 30, 2025
  • Tazama zote

Video

KIWANJA CHAKO KINA HATI? | UMEKUWA UKISUMBULIWA NA MIGOGORO YA ARDHI? | KARIBU KWENYE ARDHI CLINIC
More Videos

Viunganishi vya haraka

  • Leseni za biashara
  • Ushuru wa Hoteli
  • Kibali cha ujenzi
  • Sheria ndogondogo
  • Malengo na Dira
  • Muundo wa Uongozi
  • zabuni

Viunganishi linganifu

  • The National Examinations Council of Tanzania
  • TAMISEMI
  • Ministry of Education
  • President office State House
  • National Council for Technical Education
  • Ministry of Finace and Planning

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya wanaoingia

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Luguruni Area, Morogoro Road

    Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam

    Telephone: +255 22 2926341

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: md@ubungomc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa