• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
Ubungo Municipal Council
Ubungo Municipal Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Malengo na dhamira
    • Maadili ya Msingi
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Elimu Sekondari
      • Agriculture, Livestock and Fisheries
      • Industry,Trade and Investments
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure, Rural and Urban Development
      • Pre-Primary and Primary Education
      • Human Resources Management and administration
      • Health, Social Welfare and Nutrition Services
      • Communit Development
    • Vitengo
      • Legal Services
      • Ukaguzi wa ndani
      • TEHAMA
      • Procument Management
      • Government Communication
      • Finance and Accounts
      • Sports, Culture and Arts
      • Waste Management and Sanitation
      • Natural Resources and Environment Conservation
    • Sheria ndogo ndogo za Manispaa
      • Sheria ndogo ndogo za Manispaa
      • Other Laws
  • Fursa za Uwekezaji
    • Ufugaji
    • Kilimo
    • Masoko
    • Vituo vya Basi
    • Viwanda
  • Huduma zetu
    • Afya
      • iCHF
      • Lishe
      • Social welfare
    • Elimu
      • Pre and Primary Education
      • Elimu Sekondari
    • Biashara
      • Ushuru wa Huduma
      • Usajili wa Tax
      • Leseni za Biashara
      • Ushuru wa Hoteli
    • Ujasiliamali
      • Ten Percent Loans
    • Kilimo
    • Uvuvi
    • Ufugaji
      • UJUWA
  • Madiwani
    • Orodha za Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za kudumu
    • Ratiba za vikao vya kisheria
    • Ratiba ya Kumuona Meya
  • Miradi
    • Miradi iliyopangwa
    • Miradi endelevu
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Fomu za Maombi
    • Ripoti
    • Sheria
    • Bronchures
    • Zabuni iliyotangazwa
    • Mpango Mkakati
    • Newsletter
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Hotuba

MKURUGENZI UBUNGO ATEMBELEA MRADI WA UJENZI WA KITUO CHA KIBIASHARA CHA KIMATAIFA

Posted on: November 15th, 2023

Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg. Elias Ntiruhungwa  tarehe 15/11/2023 ametembelea mradi wa kituo cha kibiashara cha Kimataifa kinachojengwa na Kampuni ya EAST AFRICA COMMERCIAL & LOGISTICS CENTER (EACLC) eneo la Ubungo ilipokuwa stendi ya zamani ya mabasi yaendayo Mikoani na Nchi jirani.

Akiongea wakati anakagua mradi huo Ntiruhungwa ameeleza kuwa ujenzi wa Kituo hicho utagharimu Dola za Kimarekani Milioni 118 sawa na Shilingi Bilioni 294 za kitanzania na kitakuwa ni kituo kikubwa na cha kisasa Afrika Mashariki.

Ntiruhungwa ameendelea kueleza kuwa mradi huo utakuwa na jumla ya fremu za ukubwa tofauti tofauti zaidi 2000 na utazalisha ajira za moja kwa moja zaidi ya 15,000 na zisizo za moja kwa moja zaidi ya 50,000 lakini pia utaiwezesha Serikali kuongeza mapato yake.

Sambamba na hayo Ntiruhungwa ametoa wito kwa jamii hususani wafanyabiashara kuitumia fursa ya uwepo wa Kituo hicho muhimu kwao na kuwahi kupata fremu za biashara zao ambapo wafanyabiashara wakubwa na wadogo watapata fursa ya kufanya biashara ndani ya kituo hicho.


“Eneo linapojengwa kituo hiki ni eneo rafiki kwa wafanyabiashara kwani linafikika kiurahisi kutokana na uwepo wa miundombinu rafiki ya usafiri ambayo inamuwezesha mtu kufika kwa urahisi kutoka sehemu yeyote ndani na nje ya Mkoa wa Dar es salaam” aliongeza Ntiruhungwa.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kampuni ya EACLC Ndg. Catty Wang amewashukuru Viongozi wa Manispaa ya Ubungo kwa ushirikiano wanaoupata kipindi chote tangu kuanza kwa mradi huo na amesema ujenzi wa mradi huo utakamilika mnamo mwezi Juni 2024 na mara moja biashara zitaanza kufanyika. 

Catty ameendelea kueleza kuwa ukamilikaji wa mradi huo utawezesha kukua kwa biashara ndogo ndogo na kupanua biashara hizo ndani ya soko kubwa la Afrika kwani watanzania watapata fursa ya kuagiza na kuuza bidhaa nje ya Tanzania. 

Ikumbukwe kuwa Manispaa ya Ubungo iliingia mkataba na Kampuni ya Shanghai Linghang group limited ambaye ni mwekezaji na Kampuni hiyo imeiteua kampuni ya EAST AFRICA COMMERCIAL & LOGISTICS CENTER (EACLC) kwa ajili ya ujenzi wa kituo hicho

























Taarifa

  • KIBALI CHA KUANZA KUTOZA USHURU WA KUSHUSHA NA KUPAKIA MIZIGO July 17, 2023
  • KUKANUSHA TAARIFA YA UWEPO WA HARAFU MBAYA STENDI YA MABASI MAGUFULI July 06, 2023
  • MATOKEO YA SENSA YA WATU NA MAKAZI 2022 Ubungo September 06, 2023
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI NAFASI YA DEREVA NA KATIBU MAHSUSI July 21, 2022
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • KATA YA UBUNGO YAKABIDHI MKOPO WA TSH. 122,800,000/= KWA VIKUNDI SITA VYA ASILIMIA 10

    May 02, 2025
  • KAMPENI YA KATAA UCHAFU, SAFISHA, PENDESHA UBUNGO YAZINDULIWA, MITAA SAFI NA MICHAFU KUPEWA ZAWADI

    May 03, 2025
  • FANYENI KAZI, MSIJALI MASILAHI BINAFSI" ~ CHALAMILA

    May 01, 2025
  • HUDUMA YA KUJIFUNGUA KWA UPASUAJI YAANZA RASMI KITUO CHA AFYA GOBA,WANANCHI WAKARIBISHWA

    April 30, 2025
  • Tazama zote

Video

KIWANJA CHAKO KINA HATI? | UMEKUWA UKISUMBULIWA NA MIGOGORO YA ARDHI? | KARIBU KWENYE ARDHI CLINIC
More Videos

Viunganishi vya haraka

  • Leseni za biashara
  • Ushuru wa Hoteli
  • Kibali cha ujenzi
  • Sheria ndogondogo
  • Malengo na Dira
  • Muundo wa Uongozi
  • zabuni

Viunganishi linganifu

  • The National Examinations Council of Tanzania
  • TAMISEMI
  • Ministry of Education
  • President office State House
  • National Council for Technical Education
  • Ministry of Finace and Planning

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya wanaoingia

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Luguruni Area, Morogoro Road

    Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam

    Telephone: +255 22 2926341

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: md@ubungomc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa