• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
Ubungo Municipal Council
Ubungo Municipal Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Malengo na dhamira
    • Maadili ya Msingi
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Elimu Sekondari
      • Agriculture, Livestock and Fisheries
      • Industry,Trade and Investments
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure, Rural and Urban Development
      • Pre-Primary and Primary Education
      • Human Resources Management and administration
      • Health, Social Welfare and Nutrition Services
      • Communit Development
    • Vitengo
      • Legal Services
      • Ukaguzi wa ndani
      • TEHAMA
      • Procument Management
      • Government Communication
      • Finance and Accounts
      • Sports, Culture and Arts
      • Waste Management and Sanitation
      • Natural Resources and Environment Conservation
    • Sheria ndogo ndogo za Manispaa
      • Sheria ndogo ndogo za Manispaa
      • Other Laws
  • Fursa za Uwekezaji
    • Ufugaji
    • Kilimo
    • Masoko
    • Vituo vya Basi
    • Viwanda
  • Huduma zetu
    • Afya
      • iCHF
      • Lishe
      • Social welfare
    • Elimu
      • Pre and Primary Education
      • Elimu Sekondari
    • Biashara
      • Ushuru wa Huduma
      • Usajili wa Tax
      • Leseni za Biashara
      • Ushuru wa Hoteli
    • Ujasiliamali
      • Ten Percent Loans
    • Kilimo
    • Uvuvi
    • Ufugaji
      • UJUWA
  • Madiwani
    • Orodha za Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za kudumu
    • Ratiba za vikao vya kisheria
    • Ratiba ya Kumuona Meya
  • Miradi
    • Miradi iliyopangwa
    • Miradi endelevu
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Fomu za Maombi
    • Ripoti
    • Sheria
    • Bronchures
    • Zabuni iliyotangazwa
    • Mpango Mkakati
    • Newsletter
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Hotuba

MKURUGENZI UBUNGO MANISPAA AKUTANA NA WAMILIKI, WAKUU WA SHULE BINAFSI.

Posted on: July 21st, 2023

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo Ndg. Elias Ntiruhungwa amewataka wamiliki na wakuu wa Shule za Msingi na Sekondari binafsi kulipa madeni ya ada ya ushuru wa huduma “service levy” kabla ya tarehe 1 Septemba, 2023 kwa Shule ambazo zinadaiwa.

Agizo hilo amelitoa  tarehe 21 Julai, 2023 wakati wa kikao kilichofanyika katika ukumbi wa Manispaa hiyo kilichojumuisha wamiliki na wakuu wa Shule za Msingi na Sekondari za binafsi zilizopo ndani ya Manispaa hiyo.

Ntiruhungwa ameendelea kwa kusema kuwa ni jukumu la kila Shule binafsi ambayo wanafunzi wa Shule hizo wanalipa ada ili kupata huduma ya elimu kulipa ada  ya ushuru wa huduma kama ambavyo sheria inataka, na ameiagiza ofisi ya biashara kuendelea kuzifuatilia Shule hizo ili kulipa ada hiyo.

Akifafanua sheria hiyo Mwanasheria wa Manispaa hiyo Ndg. Kissah Mbila amesema ushuru wa huduma ni kodi inayotozwa kwa mujibu wa sheria No.9 ya mwaka 1982 sura ya 290 iliyofanyiwa marekebisho yake kwa sheria No 8 ya mwaka 2012 sura ya 290, ambayo inamtaka kila mfanyabiashara anaefanya biashara kulipa ushuru wa huduma ndani ya Halmashauri husika.

Kissah ameendelea kueleza kuwa sambamba na sheria hiyo, sheria ndogo ya Halmashauri hiyo ya mwaka 2022 imefafanua zaidi namna ya kulipa ada hiyo ambapo imeeleza ada ya ushuru wa huduma ni asilimia 0.3 ya mapato ghafi ya biashara husika.


“Kama Shule yako imepata jumla ya shilingi 100,000 ya mapato ghafi basi ushuru wa huduma ni shilingi 3,000 na unaweza kulipia kwa mwezi mmoja, miezi mitatu, miezi sita au mwaka mzima” Alisema Kissah.

Akiongea kwa niaba ya wamiliki na wakuu wa Shule hizo Mwalimu Mkuu wa  Shule ya Anazak Mwl. Nkuba E Msemakweli amesema wao wapo tayari kulipa ada hizo na ameomba zinaandaliwe barua za kuonesha deni la kila Shule ili malipo yafanyike.

Manispaa ya Ubungo ina jumla ya Shule za Msingi binafsi 138 na Shule za Sekondari binafsi 37 ambazo zinapaswa kulipa ada ya ushuru wa huduma.


Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya ubungo ELIAS NTIRUHUNGWA akitoa maelekezo kwa wamiliki wa shule za msingi na sekondari katika kikao hicho

Taarifa

  • KIBALI CHA KUANZA KUTOZA USHURU WA KUSHUSHA NA KUPAKIA MIZIGO July 17, 2023
  • KUKANUSHA TAARIFA YA UWEPO WA HARAFU MBAYA STENDI YA MABASI MAGUFULI July 06, 2023
  • MATOKEO YA SENSA YA WATU NA MAKAZI 2022 Ubungo September 06, 2023
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI NAFASI YA DEREVA NA KATIBU MAHSUSI July 21, 2022
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • KATA YA UBUNGO YAKABIDHI MKOPO WA TSH. 122,800,000/= KWA VIKUNDI SITA VYA ASILIMIA 10

    May 02, 2025
  • KAMPENI YA KATAA UCHAFU, SAFISHA, PENDESHA UBUNGO YAZINDULIWA, MITAA SAFI NA MICHAFU KUPEWA ZAWADI

    May 03, 2025
  • FANYENI KAZI, MSIJALI MASILAHI BINAFSI" ~ CHALAMILA

    May 01, 2025
  • HUDUMA YA KUJIFUNGUA KWA UPASUAJI YAANZA RASMI KITUO CHA AFYA GOBA,WANANCHI WAKARIBISHWA

    April 30, 2025
  • Tazama zote

Video

KIWANJA CHAKO KINA HATI? | UMEKUWA UKISUMBULIWA NA MIGOGORO YA ARDHI? | KARIBU KWENYE ARDHI CLINIC
More Videos

Viunganishi vya haraka

  • Leseni za biashara
  • Ushuru wa Hoteli
  • Kibali cha ujenzi
  • Sheria ndogondogo
  • Malengo na Dira
  • Muundo wa Uongozi
  • zabuni

Viunganishi linganifu

  • The National Examinations Council of Tanzania
  • TAMISEMI
  • Ministry of Education
  • President office State House
  • National Council for Technical Education
  • Ministry of Finace and Planning

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya wanaoingia

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Luguruni Area, Morogoro Road

    Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam

    Telephone: +255 22 2926341

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: md@ubungomc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa