• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
Ubungo Municipal Council
Ubungo Municipal Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Malengo na dhamira
    • Maadili ya Msingi
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Elimu Sekondari
      • Agriculture, Livestock and Fisheries
      • Industry,Trade and Investments
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure, Rural and Urban Development
      • Pre-Primary and Primary Education
      • Human Resources Management and administration
      • Health, Social Welfare and Nutrition Services
      • Communit Development
    • Vitengo
      • Legal Services
      • Ukaguzi wa ndani
      • TEHAMA
      • Procument Management
      • Government Communication
      • Finance and Accounts
      • Sports, Culture and Arts
      • Waste Management and Sanitation
      • Natural Resources and Environment Conservation
    • Sheria ndogo ndogo za Manispaa
      • Sheria ndogo ndogo za Manispaa
      • Other Laws
  • Fursa za Uwekezaji
    • Ufugaji
    • Kilimo
    • Masoko
    • Vituo vya Basi
    • Viwanda
  • Huduma zetu
    • Afya
      • iCHF
      • Lishe
      • Social welfare
    • Elimu
      • Pre and Primary Education
      • Elimu Sekondari
    • Biashara
      • Ushuru wa Huduma
      • Usajili wa Tax
      • Leseni za Biashara
      • Ushuru wa Hoteli
    • Ujasiliamali
      • Ten Percent Loans
    • Kilimo
    • Uvuvi
    • Ufugaji
      • UJUWA
  • Madiwani
    • Orodha za Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za kudumu
    • Ratiba za vikao vya kisheria
    • Ratiba ya Kumuona Meya
  • Miradi
    • Miradi iliyopangwa
    • Miradi endelevu
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Fomu za Maombi
    • Ripoti
    • Sheria
    • Bronchures
    • Zabuni iliyotangazwa
    • Mpango Mkakati
    • Newsletter
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Hotuba

MUDA WA LESENI ZA BAR KUONGEZWA MPAKA SAA 9 ALFAJIRI

Posted on: April 25th, 2024

Bodi ya Vileo ya Manispaa ya Ubungo jijini Dar es Salaam inategemea kutoa leseni za nyongeza ya muda wa kufunga biashara za bar na grosari kutoka saa sita usiku mpaka saa tisa alfajiri lengo ikiwa ni kuongeza mapato ya Halmashauri kupitia chanzo hicho na wateja kufurahia huduma hiyo masaa 24

Maamuzi hayo yametolewa  Aprili 25, 2024 kwenye kikao cha bodi hiyo kilicholenga kujadili na kupitisha maombi ya leseni za vileo kwa kipindi cha kwanza cha mwezi Aprili hadi septemba 30, 2024 ambapo jumla ya maombi ya leseni 1131 yameridhiwa na bodi hiyo na kusisitiza kuwa utoaji wa elimu uendelee ili wafanyabiashara wengi wapatiwe leseni.

Mwenyekiti wa kikao hicho, Mhe Omary Yusuph Yenga amesema leseni hiyo itakayotozwa shilling 50,000 kwa mwezi, bodi imeamua kuanzisha utaratibu huo baada ya bar na grosari nyingi katika Manispaa hiyo kutofuata sheria ya leseni zao za kawaida zinazowataka kufunga biashara hiyo saa tano usiku kwa siku za kazi na saa sita usiku kwa siku za wikiendi hivyo  utaratibu huo utawawezesha kufanya bishara kwa kufuata sheria tofauti na sasa ambapo bar zinakesha bila kibali.

Akifafanua umuhimu wa kuanzisha utaratibu huo, Mhe. Yenga amesema kwasababu biashara nyingi katika jiji hilo zinafanyika masaa 24, utoaji wa leseni za nyongeza ya muda wa kufunga Bar na Grosari ni mhimu ili watu wasivunje sheria lakini pia halmashauri isipoteze mapato.

Kwa mujibu wa takwimu, Manispaa ya Ubungo inajumla ya bar na grosari 800 ambapo kupitia maamuzi hayo halmashauri inatarajia kukusanya zaidi ya milioni 480 kwa mwaka kutoka kwenye chanzo hicho kipya cha leseni kiasi ambacho ni zaidi ya makisio ya bajeti ya shilingi milioni 200 kwa mwaka huu wa fedha 2023/2024 kwa leseni zote za biashara.

Katika kuhakikisha agizo hilo linatekelezwa, bodi imeielekeza idara ya biashara kutaarifu wamiliki wote kulipia leseni ya kibali cha muda wa nyongeza wa kufunga biashara hizo na atakayebainika kukesha na biashara hiyo bila kibali hicho atatozwa fine ya shilingi 1,000,000.

Taarifa

  • KIBALI CHA KUANZA KUTOZA USHURU WA KUSHUSHA NA KUPAKIA MIZIGO July 17, 2023
  • KUKANUSHA TAARIFA YA UWEPO WA HARAFU MBAYA STENDI YA MABASI MAGUFULI July 06, 2023
  • MATOKEO YA SENSA YA WATU NA MAKAZI 2022 Ubungo September 06, 2023
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI NAFASI YA DEREVA NA KATIBU MAHSUSI July 21, 2022
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • KATA YA UBUNGO YAKABIDHI MKOPO WA TSH. 122,800,000/= KWA VIKUNDI SITA VYA ASILIMIA 10

    May 02, 2025
  • KAMPENI YA KATAA UCHAFU, SAFISHA, PENDESHA UBUNGO YAZINDULIWA, MITAA SAFI NA MICHAFU KUPEWA ZAWADI

    May 03, 2025
  • FANYENI KAZI, MSIJALI MASILAHI BINAFSI" ~ CHALAMILA

    May 01, 2025
  • HUDUMA YA KUJIFUNGUA KWA UPASUAJI YAANZA RASMI KITUO CHA AFYA GOBA,WANANCHI WAKARIBISHWA

    April 30, 2025
  • Tazama zote

Video

KIWANJA CHAKO KINA HATI? | UMEKUWA UKISUMBULIWA NA MIGOGORO YA ARDHI? | KARIBU KWENYE ARDHI CLINIC
More Videos

Viunganishi vya haraka

  • Leseni za biashara
  • Ushuru wa Hoteli
  • Kibali cha ujenzi
  • Sheria ndogondogo
  • Malengo na Dira
  • Muundo wa Uongozi
  • zabuni

Viunganishi linganifu

  • The National Examinations Council of Tanzania
  • TAMISEMI
  • Ministry of Education
  • President office State House
  • National Council for Technical Education
  • Ministry of Finace and Planning

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya wanaoingia

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Luguruni Area, Morogoro Road

    Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam

    Telephone: +255 22 2926341

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: md@ubungomc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa