• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
Ubungo Municipal Council
Ubungo Municipal Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Malengo na dhamira
    • Maadili ya Msingi
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Elimu Sekondari
      • Agriculture, Livestock and Fisheries
      • Industry,Trade and Investments
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure, Rural and Urban Development
      • Pre-Primary and Primary Education
      • Human Resources Management and administration
      • Health, Social Welfare and Nutrition Services
      • Communit Development
    • Vitengo
      • Legal Services
      • Ukaguzi wa ndani
      • TEHAMA
      • Procument Management
      • Government Communication
      • Finance and Accounts
      • Sports, Culture and Arts
      • Waste Management and Sanitation
      • Natural Resources and Environment Conservation
    • Sheria ndogo ndogo za Manispaa
      • Sheria ndogo ndogo za Manispaa
      • Other Laws
  • Fursa za Uwekezaji
    • Ufugaji
    • Kilimo
    • Masoko
    • Vituo vya Basi
    • Viwanda
  • Huduma zetu
    • Afya
      • iCHF
      • Lishe
      • Social welfare
    • Elimu
      • Pre and Primary Education
      • Elimu Sekondari
    • Biashara
      • Ushuru wa Huduma
      • Usajili wa Tax
      • Leseni za Biashara
      • Ushuru wa Hoteli
    • Ujasiliamali
      • Ten Percent Loans
    • Kilimo
    • Uvuvi
    • Ufugaji
      • UJUWA
  • Madiwani
    • Orodha za Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za kudumu
    • Ratiba za vikao vya kisheria
    • Ratiba ya Kumuona Meya
  • Miradi
    • Miradi iliyopangwa
    • Miradi endelevu
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Fomu za Maombi
    • Ripoti
    • Sheria
    • Bronchures
    • Zabuni iliyotangazwa
    • Mpango Mkakati
    • Newsletter
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Hotuba

RC MAKONDA ATOA MWEZI MMOJA KWA MKANDARASI TBA KUKAMILISHA UJENZI WA OFISI ZA MANISPAA YA UBUNGO

Posted on: June 30th, 2020

Hayo yamejiri  wakati wa ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda ya kupokea na kukabidhi miradi ya Maendeleo kwa uongozi wa chama mkoa inayotekelezwa katika Manispaa ya Ubungo hususani jimbo la Kibamba.

Katika ziara hiyo RC aliongozana na Kamati ya Siasa ya Mkoa ikiongozwa na Katibu wa chama Mkoa  Ndg. Zakaria Mwansansu  na kupokelewa na Viongozi wa Chama Wilaya, Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe.Kisare Makori, Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Beatrice Dominic, Katibu Tawala wa Wilaya ya Ubungo  Ndg.James Mkumbo,  Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya na  Wataalam kutoka Manispaa ya Ubungo.

"Tusipimane uwezo" Hiyo ilikuwa kauli ya Mhe. Paul Makonda kwa TBA wakati wa ukaguzi wa mradi wa Ofisi za Manispaa ya Ubungo.

Baada ya ukaguzi huo Mhe. Mkuu wa Mkoa aligoma kukabidhi mradi huo kwa Chama cha Mapinduzi na kuwapa TBA muda wa mwezi mmoja hadi tarehe 30 July mradi huo uwe umekamilika kwa ajili ya kukabidhiwa.

Sambamba na hiloMiradi iliyotembelewa ni kuona kazi za Wajasiriamali vikundi 20 waliopewa mikopo na Halmashauri na katika mradi huo Mkuu wa Mkoa alikabidhi bajaji 22 kwa vikundi vilivyokidhi vigezo, Mradi wa Upanuzi wa barabara ya Morogoro(Kimara-Kibaha)njia nane ikihusisha ujenzi wa daraja la Kibamba, Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Manispaa ya Ubungo uliopo Luguruni, Mradi wa Ujenzi wa Stendi ya Mabasi Mbezi Luis na Mradi wa ujenzi wa Kituo cha Afya Kimara

Lengo la ziara hiyo ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam  kukabidhi  miradi ya maendeleo iliyotekelezwa  kwa Ilani ya CCM na ahadi za Mhe. Rais kwa kipindi cha miaka mitano ya Mhe. Dr. John Pombe Magufuli kwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa.

"Niendelee kutoa shukrani za pekee kwa Mhe. Rais wa awamu ya tano kwa maendeleo anayoendelea kuyaleta kwa wananchi wa Wilaya ya Ubungo na kwa kauli yake kuwa maendeleo hayana chama na watanzania kwa ujumla, Miradi imejengwa kwa vigezo stahiki kwa kipindi chote cha miaka minne ya utawala wake." aliongeza Mkuu wa Mkoa.

"Kwa mwaka 2020-2021 Chama cha Mapinduzi kimeahidi kuhakikisha wananchi wa Wilaya ya Ubungo wanajengewa barabara za ndani(barabara za mitaani) zenye urefu wa KM 111.76  ili kutatua kero ya barabara  kwa wananchi hao" aliongeza Makonda.

Mkuu wa Mkoa alitoa taarifa ya  ahadi ya Mhe. Rais aliyoahidi kwa ajili ya ujenzi wa Hospitali ya Wilaya kuwa tayari fedha hizo  zimeshaingizwa ili mradi wa ujenzi wa Hospitali ya Wilaya uweze kukamilika.

Pia  Mhe.Mkuu wa Mkoa alisema kuwa katika kuhakikisha anaendelea kuleta maendeleo kwa wananchi Mhe.Rais amesamehe riba ya mikopo inayotolewa na  mfuko  wa vijana, wanawake na watu wenye  walemavu.

"Niwapongeze viongozi wa Wilaya ya Ubungo kwa mapokezi mazuri na tunaondoka tukiwa na matumaini mapya na mazuri na Wilaya ya Ubungo" alimalizia Mkuu wa Mkoa

NB. Ziara hii itafanyika kwa siku mbili kuanzia leo ambayo imefanyika kwa jimbo la Kibamba  na kumalizika kesho tarehe 1/7/2020 kwa jimbo la Ubungo

Taarifa

  • KIBALI CHA KUANZA KUTOZA USHURU WA KUSHUSHA NA KUPAKIA MIZIGO July 17, 2023
  • KUKANUSHA TAARIFA YA UWEPO WA HARAFU MBAYA STENDI YA MABASI MAGUFULI July 06, 2023
  • MATOKEO YA SENSA YA WATU NA MAKAZI 2022 Ubungo September 06, 2023
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI NAFASI YA DEREVA NA KATIBU MAHSUSI July 21, 2022
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MAAFISA HABARI HAKIKISHENI MNATANGAZA UTEKELEZAJI WA MIRADI KWA WANANCHI

    May 24, 2025
  • CRDB WAMKARIBISHA DC MSANDO KWA KUTOA MADAWATI 30 NA VIFAA VYA MICHEZO

    May 22, 2025
  • MAFUNZO KWA WATENDAJI NGAZI YA KATA KUHUSU UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA AWAMU YA PILI.

    May 14, 2025
  • NI LAZIMA UJENZI WA UKUTA UANZE NA KUKAMILIKA" DC MSANDO

    May 12, 2025
  • Tazama zote

Video

KIWANJA CHAKO KINA HATI? | UMEKUWA UKISUMBULIWA NA MIGOGORO YA ARDHI? | KARIBU KWENYE ARDHI CLINIC
More Videos

Viunganishi vya haraka

  • Leseni za biashara
  • Ushuru wa Hoteli
  • Kibali cha ujenzi
  • Sheria ndogondogo
  • Malengo na Dira
  • Muundo wa Uongozi
  • zabuni

Viunganishi linganifu

  • The National Examinations Council of Tanzania
  • TAMISEMI
  • Ministry of Education
  • President office State House
  • National Council for Technical Education
  • Ministry of Finace and Planning

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya wanaoingia

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Luguruni Area, Morogoro Road

    Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam

    Telephone: +255 22 2926341

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: md@ubungomc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa