• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
Ubungo Municipal Council
Ubungo Municipal Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Malengo na dhamira
    • Maadili ya Msingi
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Elimu Sekondari
      • Agriculture, Livestock and Fisheries
      • Industry,Trade and Investments
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure, Rural and Urban Development
      • Pre-Primary and Primary Education
      • Human Resources Management and administration
      • Health, Social Welfare and Nutrition Services
      • Communit Development
    • Vitengo
      • Legal Services
      • Ukaguzi wa ndani
      • TEHAMA
      • Procument Management
      • Government Communication
      • Finance and Accounts
      • Sports, Culture and Arts
      • Waste Management and Sanitation
      • Natural Resources and Environment Conservation
    • Sheria ndogo ndogo za Manispaa
      • Sheria ndogo ndogo za Manispaa
      • Other Laws
  • Fursa za Uwekezaji
    • Ufugaji
    • Kilimo
    • Masoko
    • Vituo vya Basi
    • Viwanda
  • Huduma zetu
    • Afya
      • iCHF
      • Lishe
      • Social welfare
    • Elimu
      • Pre and Primary Education
      • Elimu Sekondari
    • Biashara
      • Ushuru wa Huduma
      • Usajili wa Tax
      • Leseni za Biashara
      • Ushuru wa Hoteli
    • Ujasiliamali
      • Ten Percent Loans
    • Kilimo
    • Uvuvi
    • Ufugaji
      • UJUWA
  • Madiwani
    • Orodha za Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za kudumu
    • Ratiba za vikao vya kisheria
    • Ratiba ya Kumuona Meya
  • Miradi
    • Miradi iliyopangwa
    • Miradi endelevu
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Fomu za Maombi
    • Ripoti
    • Sheria
    • Bronchures
    • Zabuni iliyotangazwa
    • Mpango Mkakati
    • Newsletter
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Hotuba

UBUNGO KUJA NA ELIMU YAMLIPA KODI

Posted on: November 6th, 2023

Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Ubungo  kwa kushirikiana na ofisi ya Manispaa ya Ubungo wanatarajia kuandaa na kutekeleza mpango mkakati wa pamoja wa ukusanyaji wa mapato utakaoambatana na utoaji wa elimu kwa mlipa kodi ili kufikia lengo la kukusanya 50% ya mapato katika kipindi cha robo ya pili kinachomalizika mwezi desemba 2023.

Uamuzi huo umetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe. Hashimu Komba kwenye kikao cha mapato kilichofanyika novemba 06, 2023 kilicholenga kufanya tathmini ya ukusanyaji wa mapato katika Manispaa hiyo ambapo kwa kipindi cha robo ya kwanza ilikusanya mapato yake  kwa 23% badala ya 25% iliyokuwa inatakiwa.

Akiongea kwenye kikao hicho, Mhe. Komba amesema kuwa timu hiyo itajikita zaidi kukusanya vyanzo vikubwa vya mapato ikiwemo ushuru wa Huduma, leseni za biashara , vibali vya ujenzi  na wadaiwa sugu (defaulters)  wakiwemo wa  leseni za biashara, ushuru wa huduma ili kuhakikisha mapato yanakusanywa kikamilifu.

Ili kutekeleza zoezi hilo kikamilifu Mhe.Komba ameiagiza menejimenti kuandaa kanzidata ya takwimu ya kila chanzo kwa ajili ya  kurahisisha ukusanyaji wa mapato kwani takwimu zitaonesha ukubwa wa kazi na uwekezaji wa nguvu katika ukusanyaji.

"Andaeni takwimu  halisi za Maduka, hotel, nyumba za kulala wageni, mabango, fremu za maduka, vizimba na wadaiwa sugu ili kujua tunapaswa kukusanya kiasi gani kwenye kila chanzo na kazi hii ifanyike haraka" aliagiza DC Komba

Aidha, pamoja na mkakati huo DC Komba amewataka mameneja wa vyanzo vya mapato katika Manispaa hiyo kuacha kufanya kazi kwa mazoea badala yake wawe wabunifu na kuhakikisha vyanzo wanavyosimami  vinakusanya mapato kwa asilimia 100 kwani hakuna sababu ya kutofikia lengo.

Nae Mkurugenzi wa Manispaa hiyo Ndg Elias Ntiruhungwa amemshukuru DC Komba kwa kikao hicho na kuahidi kuwa kwa kipindi cha robo ya pili kinachoishia mwezi disemba,Manispaa itafikia lengo la kukusanya asilimia 50 ya bajeti bila wasiwasi.

Kwa kipindi cha robo ya kwanza yaani kuanzia mwezi julai hadi Septemba Manispaa ya Ubungo imekusanya kiasi cha bilioni 7.9 kati ya bilioni 35.2 zilizopangwa kukusanywa kwa mwaka wa fedha 2023/ 2024.

pichani ni wajumbe wa kikao wakijadili namna bora ya itakayosaidia kuongezeka kwa  mapato
















Taarifa

  • KIBALI CHA KUANZA KUTOZA USHURU WA KUSHUSHA NA KUPAKIA MIZIGO July 17, 2023
  • KUKANUSHA TAARIFA YA UWEPO WA HARAFU MBAYA STENDI YA MABASI MAGUFULI July 06, 2023
  • MATOKEO YA SENSA YA WATU NA MAKAZI 2022 Ubungo September 06, 2023
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI NAFASI YA DEREVA NA KATIBU MAHSUSI July 21, 2022
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • WATOA HUDUMA ZA AFYA NGAZI YA JAMII 30 WAJENGEWA UWEZO

    July 14, 2025
  • MAKABURI 29 YA UFI UBUNGO KISIWANI YAHAMISHWA KUPISHA UPANUZI WA BARABARA.

    July 10, 2025
  • UBUNGO TAYARI TUPO KATIKA MAONESHO YA 49 YA KITAIFA YA BIASHARA 7'7, MNAKARIBISHWA

    June 30, 2025
  • SERIKALI YAZINDUA MADAWATI YA HUDUMA ZA USTAWI WA JAMII KATIKA VITUO VYA USAFIRISHAJI.

    June 30, 2025
  • Tazama zote

Video

KIWANJA CHAKO KINA HATI? | UMEKUWA UKISUMBULIWA NA MIGOGORO YA ARDHI? | KARIBU KWENYE ARDHI CLINIC
More Videos

Viunganishi vya haraka

  • Leseni za biashara
  • Ushuru wa Hoteli
  • Kibali cha ujenzi
  • Sheria ndogondogo
  • Malengo na Dira
  • Muundo wa Uongozi
  • zabuni

Viunganishi linganifu

  • The National Examinations Council of Tanzania
  • TAMISEMI
  • Ministry of Education
  • President office State House
  • National Council for Technical Education
  • Ministry of Finace and Planning

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya wanaoingia

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Luguruni Area, Morogoro Road

    Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam

    Telephone: +255 22 2926341

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: md@ubungomc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa