• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
Ubungo Municipal Council
Ubungo Municipal Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Malengo na dhamira
    • Maadili ya Msingi
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Elimu Sekondari
      • Kilimo umwagiliaji na ushirika
      • Fedha na Biashara
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Mipango miji na Ardhi
      • Elimu Msingi
      • Utumishi na Utawala
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Maendeleo ya Jamii na Vijana
      • Maji na Usafishaji
      • Ufugaji na Uvuvi
      • Ujenzi
      • Mazingira na udhibiti wa taka ngumu
    • Vitengo
      • Kitengo cha Sheria
      • Ukaguzi wa ndani
      • TEHAMA
        • Uhusiano
      • Uchaguzi
      • Manunuzi na Ugavi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Ufugaji
    • Kilimo
    • Masoko
    • Vituo vya Basi
    • Viwanda
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Biashara
      • Ushuru wa Huduma
      • Usajili wa Tax
      • Leseni za Biashara
      • Ushuru wa Hoteli
    • Ujasiliamali
    • Kilimo
    • Uvuvi
    • Ufugaji
      • UJUWA
  • Madiwani
    • Orodha za Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za kudumu
    • Ratiba za vikao vya kisheria
    • Ratiba ya Kumuona Meya
  • Miradi
    • Miradi iliyopangwa
    • Miradi endelevu
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Fomu za Maombi
    • Ripoti
    • Sheria
    • Bronchures
    • Zabuni iliyotangazwa
    • Mpango Mkakati
    • Newsletter
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Hotuba

UBUNGO YATIA FORA KAMPENI YA SAFISHA PENDEZESHA DAR ES SALAAM, RC MAKALLA AIPONGEZA

Posted on: February 25th, 2023

Katika kuendeleza kampeni ya Safisha Pendezesha Dar es Salaam ambayo hufanyika kila jumamosi ya mwisho wa mwezi, leo Februari 25, 2023 mkuu wa mkoa wa Dar es salaam CPA Amos Makalla ameiongoza kampeni hiyo kwa mafanikio ambayo kimkoa imefanyika katika wilaya ya Ubungo barabara ya Sam Nujoma. 

Kampeni hiyo ni mahsusi kwaajili ya kuhakikisha usafi wa mazingira unafanyika kwa ujumla katika maeneo yote ili kutokuruhusu mlipuko wa magonjwa pamoja na muonekano mbaya wa viunga vya jiji la Dar es Salaam 

Awali mkuu wa wilaya ya Ubungo Mhe. Hashim Komba amempongeza Mhe. Makalla kwa maono yake makubwa kwenye suala la usafi wa Mazingira na wao kama uongozi wa Wilaya ya Ubungo watahakikisha wanakuwa wa kwanza kwenye kuendeleza na kutafsiri kwa vitendo kampeni ya Safisha Pendezesha Dar es Salaam. 

Nae mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam CPA Amos Makalla amechukua nafasi hiyo kuipongeza Wilaya ya Ubungo kwa hamasa kubwa waliyonayo kwenye suala la usafi na mwitikio mkubwa waliouonesha leo.

"Niseme tu naupongeza uongozi wa Wilaya na Manispaa ya Ubungo kwa jinsi mnavyojipanga linapokuja suala la usafi kiukweli hamjawahi kuniangusha. Ubungo kwenye usafi siku zote imekuwa ya kwanza na huo ndio mwelekeo tunaoutaka kwa jiji letu la Dar Es Salaam" Alisema Makalla 

Mkuu wa Mkoa Mheshimiwa AMOS MAKALLA akipanda mti katika zoezi la usafi 

Vilevile Mhe. Makalla ameendelea kuwakumbusha wafanyabiashara ndogondogo maarufu kama machinga kuwa bado ni marufuku kufanya biashara kwenye maeneo yaliyokatazwa ikiwema pembezoni mwa barabara, juu ya mitaro ya maji, njia za wapita kwa miguu pamoja na maeneo ya mbele kwenye taasisi za umma 


Kwa upande mwingine Mhe. Makalla amemuagiza mkuu wa wilaya ya Ubungo pamoja na mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo kuhakikisha wanatatua changamoto ya soko la Mawasiliano ili kuzuia wananchi kutoka nje ya soko hilo kwaajili ya shughuli zao 


Aidha wadau mbalimbali  wameshiriki kwenye zoezi hilo ikiwemo benki ya NMB, taasisi isiyo ya kiserikali ya HUDEFO 


Taarifa

  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI NAFASI YA DEREVA NA KATIBU MAHSUSI July 21, 2022
  • JOINING INSTRUCTIONS KWA SHULE ZA SEKONDARI ZA UBUNGO MANISPAA 2023. December 28, 2022
  • SELECTION ZA KIDATO CHA KWANZA UBUNGO MANISPAA 2023 December 28, 2022
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI June 02, 2022
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • UBUNGO YAFANYA MAADHIMISHO YA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI KIWILAYA

    March 08, 2023
  • ZIARA YA KUTEMBELEA MIRADI YAFANYIKA , DC KOMBA ATOA MAELEKEZO

    March 01, 2023
  • UBUNGO YATIA FORA KAMPENI YA SAFISHA PENDEZESHA DAR ES SALAAM, RC MAKALLA AIPONGEZA

    February 25, 2023
  • BODI YA AFYA YAPITIA TAARIFA YA UTENDAJI ROBO YA PILI

    March 24, 2023
  • Tazama zote

Video

FAHAMU ALICHOKISEMA DC KOMBA KWENYE ZIARA LEO | AIAGIZA TAKUKURU KUFANYA UCHUNGUZI
More Videos

Viunganishi vya haraka

  • Leseni za biashara
  • Ushuru wa Hoteli
  • Kibali cha ujenzi
  • Sheria ndogondogo
  • Malengo na Dira
  • Muundo wa Uongozi
  • zabuni

Viunganishi linganifu

  • The National Examinations Council of Tanzania
  • TAMISEMI
  • Ministry of Education
  • President office State House
  • National Council for Technical Education
  • Ministry of Finace and Planning

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya wanaoingia

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Luguruni Area, Morogoro Road

    Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam

    Telephone: +255 22 2926341

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: md@ubungomc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa