• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
Ubungo Municipal Council
Ubungo Municipal Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Malengo na dhamira
    • Maadili ya Msingi
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Elimu Sekondari
      • Agriculture, Livestock and Fisheries
      • Industry,Trade and Investments
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure, Rural and Urban Development
      • Pre-Primary and Primary Education
      • Human Resources Management and administration
      • Health, Social Welfare and Nutrition Services
      • Communit Development
    • Vitengo
      • Legal Services
      • Ukaguzi wa ndani
      • TEHAMA
      • Procument Management
      • Government Communication
      • Finance and Accounts
      • Sports, Culture and Arts
      • Waste Management and Sanitation
      • Natural Resources and Environment Conservation
    • Sheria ndogo ndogo za Manispaa
      • Sheria ndogo ndogo za Manispaa
      • Other Laws
  • Fursa za Uwekezaji
    • Ufugaji
    • Kilimo
    • Masoko
    • Vituo vya Basi
    • Viwanda
  • Huduma zetu
    • Afya
      • iCHF
      • Lishe
      • Social welfare
    • Elimu
      • Pre and Primary Education
      • Elimu Sekondari
    • Biashara
      • Ushuru wa Huduma
      • Usajili wa Tax
      • Leseni za Biashara
      • Ushuru wa Hoteli
    • Ujasiliamali
      • Ten Percent Loans
    • Kilimo
    • Uvuvi
    • Ufugaji
      • UJUWA
  • Madiwani
    • Orodha za Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za kudumu
    • Ratiba za vikao vya kisheria
    • Ratiba ya Kumuona Meya
  • Miradi
    • Miradi iliyopangwa
    • Miradi endelevu
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Fomu za Maombi
    • Ripoti
    • Sheria
    • Bronchures
    • Zabuni iliyotangazwa
    • Mpango Mkakati
    • Newsletter
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Hotuba

UBUNGO,TANESCO NA SONGAS WAPEWA SIKU TANO NA DC KOMBA

Posted on: October 18th, 2023

Kufuatia mgogoro wa ardhi uliopo mtaa wa Kinzudi kata ya Goba, Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe. Hashimu Komba ametoa siku tano kwa  Manispaa ya ubungo kwa kushirikiaana na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) na SONGAS kutambua mipaka ya eneo la wazi lililokuwa linatumiwa na TANESCO baada ya kupewa na SONGAS inayodaiwa kumiliki eneo hilo.

Mhe.Komba amefikia maamuzi ya kutaka mipaka ya eneo hilo kutambuliwa na kuwekwa alama  baada ya kuzuka mgogoro baina ya wananchi wanaotumia sehemu ya  eneo hilo kuzikana na baadhi ya watu wanaosadikika kujimilikisha vipande vya ardhi katika eneo hilo kinyume na sheria.

Mhe Komba amesema "Baada ya kutambua mipaka ya eneo na kuweka alama wale ambao nyumba zao zitakuwa ndani ya eneo la wazi wataulizwa walipatapataje umiliki wa maeneo yao, tutaanzia hapo"

Kutokana na hali hiyo Mhe. Komba amewaomba wananchi kutofanya maendelezo yoyote ya kujenga au kupanda miti katika eneo hilo mpaka mgogoro huo utakapotatuliwa ambapo ameahidi kuwa katika mgogoro huo serikali itatetea maslahi ya wananchi na sio watu wachache wanaokiuka sheria.

Aidha,Mhe Komba amewaomba wananchi wa kinzudi  kutotawanya makaburi katika eneo hilo kwa lengo la kulilinda badala  yake watumie eneo la awali kwa ajili ya mazishi mpaka pale mgogoro utakapo tatuliwa.

Kutokana na mgogoro huu wa ardhi hasa maeneo ya wazi, Mkuu wa Wilaya ameagiza kupata ripoti ya kamati ya maeneo ya wazi na mpango wa kudhibiti uvamizi wa maeneo hayo ndani ya Wilaya hiyo kwa ajili ya kufanya ufuatiliaji.

Akiongea mbele ya Mkuu wa Wilaya huyo, mmoja wa wananchi amesema kumekuwa na uvamizi wa eneo hilo la wazi  ambapo baadhi ya watu wamejimilikisha na kujenga makazi lakini kinachoumiza hawazuiliwi ila wananchi wakitaka kuzikana wanazuiliwa.


Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe. Hashim Komba akiwa na Mwatalaam kutoka Manispaa ya Ubungo na wananchi wa kinzudi katika utatuzi wa mgogoro uliopo Kata ya Goba Mtaa wa kinzudi

Taarifa

  • KIBALI CHA KUANZA KUTOZA USHURU WA KUSHUSHA NA KUPAKIA MIZIGO July 17, 2023
  • KUKANUSHA TAARIFA YA UWEPO WA HARAFU MBAYA STENDI YA MABASI MAGUFULI July 06, 2023
  • MATOKEO YA SENSA YA WATU NA MAKAZI 2022 Ubungo September 06, 2023
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI NAFASI YA DEREVA NA KATIBU MAHSUSI July 21, 2022
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • KATA YA UBUNGO YAKABIDHI MKOPO WA TSH. 122,800,000/= KWA VIKUNDI SITA VYA ASILIMIA 10

    May 02, 2025
  • KAMPENI YA KATAA UCHAFU, SAFISHA, PENDESHA UBUNGO YAZINDULIWA, MITAA SAFI NA MICHAFU KUPEWA ZAWADI

    May 03, 2025
  • FANYENI KAZI, MSIJALI MASILAHI BINAFSI" ~ CHALAMILA

    May 01, 2025
  • HUDUMA YA KUJIFUNGUA KWA UPASUAJI YAANZA RASMI KITUO CHA AFYA GOBA,WANANCHI WAKARIBISHWA

    April 30, 2025
  • Tazama zote

Video

KIWANJA CHAKO KINA HATI? | UMEKUWA UKISUMBULIWA NA MIGOGORO YA ARDHI? | KARIBU KWENYE ARDHI CLINIC
More Videos

Viunganishi vya haraka

  • Leseni za biashara
  • Ushuru wa Hoteli
  • Kibali cha ujenzi
  • Sheria ndogondogo
  • Malengo na Dira
  • Muundo wa Uongozi
  • zabuni

Viunganishi linganifu

  • The National Examinations Council of Tanzania
  • TAMISEMI
  • Ministry of Education
  • President office State House
  • National Council for Technical Education
  • Ministry of Finace and Planning

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya wanaoingia

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Luguruni Area, Morogoro Road

    Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam

    Telephone: +255 22 2926341

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: md@ubungomc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa