• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
Ubungo Municipal Council
Ubungo Municipal Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Malengo na dhamira
    • Maadili ya Msingi
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Elimu Sekondari
      • Agriculture, Livestock and Fisheries
      • Industry,Trade and Investments
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure, Rural and Urban Development
      • Pre-Primary and Primary Education
      • Human Resources Management and administration
      • Health, Social Welfare and Nutrition Services
      • Communit Development
    • Vitengo
      • Legal Services
      • Ukaguzi wa ndani
      • TEHAMA
      • Procument Management
      • Government Communication
      • Finance and Accounts
      • Sports, Culture and Arts
      • Waste Management and Sanitation
      • Natural Resources and Environment Conservation
    • Sheria ndogo ndogo za Manispaa
      • Sheria ndogo ndogo za Manispaa
      • Other Laws
  • Fursa za Uwekezaji
    • Ufugaji
    • Kilimo
    • Masoko
    • Vituo vya Basi
    • Viwanda
  • Huduma zetu
    • Afya
      • iCHF
      • Lishe
      • Social welfare
    • Elimu
      • Pre and Primary Education
      • Elimu Sekondari
    • Biashara
      • Ushuru wa Huduma
      • Usajili wa Tax
      • Leseni za Biashara
      • Ushuru wa Hoteli
    • Ujasiliamali
      • Ten Percent Loans
    • Kilimo
    • Uvuvi
    • Ufugaji
      • UJUWA
  • Madiwani
    • Orodha za Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za kudumu
    • Ratiba za vikao vya kisheria
    • Ratiba ya Kumuona Meya
  • Miradi
    • Miradi iliyopangwa
    • Miradi endelevu
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Fomu za Maombi
    • Ripoti
    • Sheria
    • Bronchures
    • Zabuni iliyotangazwa
    • Mpango Mkakati
    • Newsletter
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Hotuba

WADAU WA MAGUFULI WAIOMBA SERIKALI KUTIA MKAZO JUU YA MABASI YASIYOINGIA NDANI YA KITUO HICHO

Posted on: October 28th, 2023

Wadau wa Mabasi yaendayo mikoani na Nchi jirani wa kituo cha Mabasi cha Magufuli  tarehe 28/09/2023 wameomba Serikali kuzuia wamiliki wa mabasi ambao hawatumii Kituo hicho kushusha na kupakia abiria na badala yake wamekuwa wakitumia ofisi zao za nje ya kituo zilizopo maeneo mbalimbali hususani Shekilango na Urafiki na hivyo kupelekea Serikali kupoteza mapato mengi.

Akiongea Ndg. Erick Peter wakala wa Mabasi ya Ngeleja ndani ya kituo hicho amesema Serikali imejenga miundombinu rafiki ya Kituo hicho ili kuiwezesha kupata mapato yatakayosaidia kuboresha huduma mbalimbali lakini imekuwa tofauti kutokana na Mabasi mengi kutoshusha wala kupakia abiria ndani ya Kituo hicho jambo ambalo linapelekea Serikali kupoteza mapato yake.

“Tunaiomba Manispaa ya Ubungo ihakikishe mabasi yote yanaingia ndani ya kituo hicho” alisisitiza Peter.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Ubungo amesema tayari ofisi yake kwa kushirikina na Ofisi ya Mkurugenzi wa Manispaa hiyo imeanza kuchukua hatua kwa lengo la kuhakikisha Mabasi hayo yanashusha na kupakia abiria ndani ya Kituo hicho.

Hatua hizo ni pamoja na kushirikisha TANROADS, Kiwanda cha Urafiki pamoja na wamiliki wa Mabasi hayo alieleza Komba.

Akisoma taarifa ya kituo hicho Ndg. Isihaka Waziri Meneja wa Kituo hicho kwa Wajumbe wa Kamati ya Siasa na Sekretarieti ya Wilaya ya Ubungo amesema ujenzi wa Kituo hicho hadi sasa umegharimu fedha kiasi cha shilingi Bilioni 49.7 kati ya shilingi bilioni 54.5 zilizotengwa ambazo kati ya hizo Bilioni 50.9 ni fedha kutoka Serikali kuu na Bilioni 3.6 ni fedha za mapato ya ndani ya Manispaa hiyo.

Waziri ameendelea kueleza kuwa utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa kituo hicho hadi sasa umekamilika kwa asilimia 97 hivyo maeneo mengine yanaendelea kuboreshwa ikiwemo maeneo ya migahawa, basements, mabenki na ofisi za tiketi.

Kwa mwaka wa fedha 2022/2023 kituo hicho kilikusanya shilingi bilioni 4.4 sawa na asilimia 88 ya makusanyo yaliyopaswa kukusanywa ambayo ni bilioni 5 hii ni kutokana na mabasi kushusha na kupakia nje ya Kituo cha Magufuli na hivyo kuikosesha mapato Manispaa.


Taarifa

  • KIBALI CHA KUANZA KUTOZA USHURU WA KUSHUSHA NA KUPAKIA MIZIGO July 17, 2023
  • KUKANUSHA TAARIFA YA UWEPO WA HARAFU MBAYA STENDI YA MABASI MAGUFULI July 06, 2023
  • MATOKEO YA SENSA YA WATU NA MAKAZI 2022 Ubungo September 06, 2023
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI NAFASI YA DEREVA NA KATIBU MAHSUSI July 21, 2022
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • KATA YA UBUNGO YAKABIDHI MKOPO WA TSH. 122,800,000/= KWA VIKUNDI SITA VYA ASILIMIA 10

    May 02, 2025
  • KAMPENI YA KATAA UCHAFU, SAFISHA, PENDESHA UBUNGO YAZINDULIWA, MITAA SAFI NA MICHAFU KUPEWA ZAWADI

    May 03, 2025
  • FANYENI KAZI, MSIJALI MASILAHI BINAFSI" ~ CHALAMILA

    May 01, 2025
  • HUDUMA YA KUJIFUNGUA KWA UPASUAJI YAANZA RASMI KITUO CHA AFYA GOBA,WANANCHI WAKARIBISHWA

    April 30, 2025
  • Tazama zote

Video

KIWANJA CHAKO KINA HATI? | UMEKUWA UKISUMBULIWA NA MIGOGORO YA ARDHI? | KARIBU KWENYE ARDHI CLINIC
More Videos

Viunganishi vya haraka

  • Leseni za biashara
  • Ushuru wa Hoteli
  • Kibali cha ujenzi
  • Sheria ndogondogo
  • Malengo na Dira
  • Muundo wa Uongozi
  • zabuni

Viunganishi linganifu

  • The National Examinations Council of Tanzania
  • TAMISEMI
  • Ministry of Education
  • President office State House
  • National Council for Technical Education
  • Ministry of Finace and Planning

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya wanaoingia

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Luguruni Area, Morogoro Road

    Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam

    Telephone: +255 22 2926341

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: md@ubungomc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa