• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
Ubungo Municipal Council
Ubungo Municipal Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Malengo na dhamira
    • Maadili ya Msingi
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Elimu Sekondari
      • Agriculture, Livestock and Fisheries
      • Industry,Trade and Investments
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure, Rural and Urban Development
      • Pre-Primary and Primary Education
      • Human Resources Management and administration
      • Health, Social Welfare and Nutrition Services
      • Communit Development
    • Vitengo
      • Legal Services
      • Ukaguzi wa ndani
      • TEHAMA
      • Procument Management
      • Government Communication
      • Finance and Accounts
      • Sports, Culture and Arts
      • Waste Management and Sanitation
      • Natural Resources and Environment Conservation
    • Sheria ndogo ndogo za Manispaa
      • Sheria ndogo ndogo za Manispaa
      • Other Laws
  • Fursa za Uwekezaji
    • Ufugaji
    • Kilimo
    • Masoko
    • Vituo vya Basi
    • Viwanda
  • Huduma zetu
    • Afya
      • iCHF
      • Lishe
      • Social welfare
    • Elimu
      • Pre and Primary Education
      • Elimu Sekondari
    • Biashara
      • Ushuru wa Huduma
      • Usajili wa Tax
      • Leseni za Biashara
      • Ushuru wa Hoteli
    • Ujasiliamali
      • Ten Percent Loans
    • Kilimo
    • Uvuvi
    • Ufugaji
      • UJUWA
  • Madiwani
    • Orodha za Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za kudumu
    • Ratiba za vikao vya kisheria
    • Ratiba ya Kumuona Meya
  • Miradi
    • Miradi iliyopangwa
    • Miradi endelevu
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Fomu za Maombi
    • Ripoti
    • Sheria
    • Bronchures
    • Zabuni iliyotangazwa
    • Mpango Mkakati
    • Newsletter
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Hotuba

WAJASIRIAMALI 700 WAANZA KUNUFAIKA NA SOKO LILILOJENGWA NA MANISPAA YA UBUNGO ENEO LA MBEZI

Posted on: December 14th, 2020

Leo tarehe 14 desemba, 2020 Manispaa ya Ubungo imewahamisha wajasiriamali wadogo zaidi ya 700 wanaofanya biashara zao barabarani eneo la mbezi kwenye mabanda ya wajasiriamali yaliyojengwa na Manispaa ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Serikali la kutenga maeneo maalumu ya wajasiriamali yatakayowawezesha kufanya Biashara zao kwa usalama.


Akiongea na wajasiriamali hao , Mkurugenzi Mtendaji wa Manispaa hiyo Beatrice Dominic amesema kuwa zoezi limeanza leo rasmi kwa kuwagawia vizimba  wajasiriamali ili kesho tarehe 15 desemba,2020 waanze kufanyia biashara zao hapo.

Wajasiriamali wakisikiliza kwa makini utaratibu wa kugawa vizimba kwenye soko la Mbezi Louis 

"Baada ya kugawa vizimba hivi hatutegemei kumwona mfanyabiashara yeyote akifanya Biashara zake kandokando ya barabara na maeneo yasiyo rasmi katika eneo hili la Mbezi.


Beatrice ameendelea kueleza kuwa "baad ya zoezi hili kukamilika tunategemea wajasiriamali wote wataondoka barabarani kama Mheshimiwa Rais alivyosema watengewe maeneo maalum kama haya na sisi kama Manispaa tutalisimamia hili" nawasii wafanyabiashara wasijaribu kufanya biashara nje ya eneo hili maalumu kwani hatua zitachuliwa dhidi yake.

Mkurugenzi Mtendaji  wa Manispaa ya Ubungo Beatrice Dominic (wa kwanza kulia) akimuonesha kizimba moja ya wajasiriamali kwenye soko la mbezi


Beatrice ameainisha kuwa, wafanyabiashara watakao anza kuhamishwa ni wenye Biashara za matunda, mbogamboga na vyakula kwa ujumla huku wengine wakisubiri kidogo.


Aidha, Kila mfanyabiashara atawajibika kulipa shilingi 500 kila siku ikiwa ni gharama za usafi wa soko ukizingatia soko litahusisha uuzaji wa bidhaa za vyakula


Pia Beatrice kaeleza kuwa  Ujenzi wa soko hili la wajasiriamali wadogo ni utekelezaji agizo la Mheshimiwa Rais ya kutengewa maeneo maalum ya kufanyia biashara zao ambapo Manispaa imetumia zaidi ya bilioni 900 kwa ajili ya kulipa fidia na kujenga mabanda hayo kwa zaidi shilingi milioni 600, fedha zote ikiwa ni mapato ya ndani.

Mkurugenzi Mtendaji wa Manispaa ya Ubungo akiwafunda wajasiriamali wa Mbezi Louis kabla ya zoezi la kutoa maeneo ya kufanyia biashara.

Mtambue kuwa moja ya kazi ya kodi zinalipwa na wananchi wakiwemo wafanyabiashara ni kuboresha huduma Kwa wananchi " ndio maana Manispaa imeweza kujenga soko hili ambalo litawasaidia wajasiriamali kufanya biashara kwa utulivu"


Kwa upande wake Afisa Biashara wa Manispaa hiyo Prisca Mjema aliwaeleza wajasiriamali hao kuwa utambuzi wa wajasiriamali umefanywa na watendaji wa mtaa hivyo haki imetendeka  hatutegemei kupata malalamiko.

Afisa biashara wa Manispaa ya Ubungo akifanya zoezi la kuhakiki wajasiriamali kabla ya kupewa eneo la kufanyia biashara.

Aidha Mjema amewasisitiza wajasiriamali hao kutambua kuwa uhamisho huo utawaondolea kibali cha kufanya biashara maeneo ya barabarani ili kupisha matumizi bora na salama ya barabara.


Akizungumza Kwa niaba ya wajasiliamali wenzake zuhura yusuph ameishukuru Manispaa Kwa kujenga mabanda hayo ambayo yatawasaidia kufanya biashara Kwa utulivu


"Jua na mvua vilikuwa halali yetu, lakini Kwa sasa tutaondokana navyo tutafanya biashara wakati wote bila mateso ,  asante Kwa Serikali ya awamu ya tano Kwa kutukimbukka wajasiriamali" alisema Zuhura.

Taarifa

  • KIBALI CHA KUANZA KUTOZA USHURU WA KUSHUSHA NA KUPAKIA MIZIGO July 17, 2023
  • KUKANUSHA TAARIFA YA UWEPO WA HARAFU MBAYA STENDI YA MABASI MAGUFULI July 06, 2023
  • MATOKEO YA SENSA YA WATU NA MAKAZI 2022 Ubungo September 06, 2023
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI NAFASI YA DEREVA NA KATIBU MAHSUSI July 21, 2022
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MAAFISA HABARI HAKIKISHENI MNATANGAZA UTEKELEZAJI WA MIRADI KWA WANANCHI

    May 24, 2025
  • CRDB WAMKARIBISHA DC MSANDO KWA KUTOA MADAWATI 30 NA VIFAA VYA MICHEZO

    May 22, 2025
  • MAFUNZO KWA WATENDAJI NGAZI YA KATA KUHUSU UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA AWAMU YA PILI.

    May 14, 2025
  • NI LAZIMA UJENZI WA UKUTA UANZE NA KUKAMILIKA" DC MSANDO

    May 12, 2025
  • Tazama zote

Video

KIWANJA CHAKO KINA HATI? | UMEKUWA UKISUMBULIWA NA MIGOGORO YA ARDHI? | KARIBU KWENYE ARDHI CLINIC
More Videos

Viunganishi vya haraka

  • Leseni za biashara
  • Ushuru wa Hoteli
  • Kibali cha ujenzi
  • Sheria ndogondogo
  • Malengo na Dira
  • Muundo wa Uongozi
  • zabuni

Viunganishi linganifu

  • The National Examinations Council of Tanzania
  • TAMISEMI
  • Ministry of Education
  • President office State House
  • National Council for Technical Education
  • Ministry of Finace and Planning

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya wanaoingia

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Luguruni Area, Morogoro Road

    Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam

    Telephone: +255 22 2926341

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: md@ubungomc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa