• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
Ubungo Municipal Council
Ubungo Municipal Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Malengo na dhamira
    • Maadili ya Msingi
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Elimu Sekondari
      • Agriculture, Livestock and Fisheries
      • Industry,Trade and Investments
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure, Rural and Urban Development
      • Pre-Primary and Primary Education
      • Human Resources Management and administration
      • Health, Social Welfare and Nutrition Services
      • Communit Development
    • Vitengo
      • Legal Services
      • Ukaguzi wa ndani
      • TEHAMA
      • Procument Management
      • Government Communication
      • Finance and Accounts
      • Sports, Culture and Arts
      • Waste Management and Sanitation
      • Natural Resources and Environment Conservation
    • Sheria ndogo ndogo za Manispaa
      • Sheria ndogo ndogo za Manispaa
      • Other Laws
  • Fursa za Uwekezaji
    • Ufugaji
    • Kilimo
    • Masoko
    • Vituo vya Basi
    • Viwanda
  • Huduma zetu
    • Afya
      • iCHF
      • Lishe
      • Social welfare
    • Elimu
      • Pre and Primary Education
      • Elimu Sekondari
    • Biashara
      • Ushuru wa Huduma
      • Usajili wa Tax
      • Leseni za Biashara
      • Ushuru wa Hoteli
    • Ujasiliamali
      • Ten Percent Loans
    • Kilimo
    • Uvuvi
    • Ufugaji
      • UJUWA
  • Madiwani
    • Orodha za Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za kudumu
    • Ratiba za vikao vya kisheria
    • Ratiba ya Kumuona Meya
  • Miradi
    • Miradi iliyopangwa
    • Miradi endelevu
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Fomu za Maombi
    • Ripoti
    • Sheria
    • Bronchures
    • Zabuni iliyotangazwa
    • Mpango Mkakati
    • Newsletter
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Hotuba

WALIMU WAJENGEWA UWEZO KUHUSU LISHE,WASISITIZWA KUTOA ELIMU KWA WANAFUNZI

Posted on: April 18th, 2024

Walimu wa maswala ya afya katika Shule za awali, Msingi na Sekondari wamejengewa uwezo wa namna ya kuwafundisha wanafunzi kuhusu lishe inayozingatia mlo kamili wenye makundi sita ya vyakula.

Akizungumza katika mafunzo hayo 18 april, 2024 yaliyofanyika katika ukumbi wa Manispaa ya Ubungo Katibu Tawala Wilaya ya Ubungo Mhe.Hassan Mkwawa amewasisitiza walimu kuhakikisha wanazingatia utoaji wa elimu kwa watoto kuhusu lishe inayozingatia makundi sahihi ya vyakula

Na pia Mhe.Mkwawa amewataka walimu kuhakikisha wanapotoa elimu ya lishe na wao pia wazingatie mashuleni vyakula vinavyotolewa vinazingatia makundi sahihi ya vyakula vitakavyomjenga mwanafunzi

"Lishe bora inasaidia mtoto katika makuzi yake anakuwa na uelewa mkubwa tofauti na mtoto anaepata lishe duni" alisisitiza Mkwawa

Aidha, Afisa lishe Manispaa ya Ubungo Beatrice Mossile aliendelea kuwajengea uwezo walimu hao na kusema kuwa, Mashuleni wanafunzi wanatakiwa kupewa elimu mara kwa mara hasa kwa watoto wanaoenda kubalehe wanastahili kufundishwa ulaji wa mbogamboga kwa wingi na matunda kwa sababu wanaelekea katika hatua ya ukuaji ambayo wasichana wengi wana balehe na mwili unahitaji kuwa na madini chuma kwa wingi

Mossile aliwafundisha pia juu ya Makundi sita ya vyakula ambavyo ni 1.vyakula vitokanavyo na nafaka, mizizi na ndizi za kupika 2.vyakula vya jamii ya mimea/mikunde 3.vyakula vyenye asili ya wanyama 4. mboga mboga 5. matunda 6. Mafuta sukari na asali

"Epukeni kula chunvi nyingi si salama kwa afya, chunvi itumike kidogo na chunvi isitumike wakati wa kula" alisisitiza Mossile

Na pia afisa kilimo Manispaa ya Ubungo Stela amewataka walimu kuwafundisha wanafunzi namna kilimo mjini kinavyoweza kuwasaidia katika kurahisisha maisha wanapokuwa majumbani kwa kulima mboga mboga ambazo hazitakuwa na gharama ya kununua

"Kilimo mjini ni muhimu watoto mashuleni wakipewa elimu wanaweza kutekeleza hilo, watoto wanatakiwa kula mboga mboga kwa wingi yaweza kuwa sio mboga za majani tu na matunda pia" alisisitiza Stela

Nae, Mratibu wa chanjo Manispaa ya Ubungo Hezron Msongole amewataka walimu kushiriki katika utoaji wa chanjo ya HPV

Taarifa

  • KIBALI CHA KUANZA KUTOZA USHURU WA KUSHUSHA NA KUPAKIA MIZIGO July 17, 2023
  • KUKANUSHA TAARIFA YA UWEPO WA HARAFU MBAYA STENDI YA MABASI MAGUFULI July 06, 2023
  • MATOKEO YA SENSA YA WATU NA MAKAZI 2022 Ubungo September 06, 2023
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI NAFASI YA DEREVA NA KATIBU MAHSUSI July 21, 2022
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • KATA YA UBUNGO YAKABIDHI MKOPO WA TSH. 122,800,000/= KWA VIKUNDI SITA VYA ASILIMIA 10

    May 02, 2025
  • KAMPENI YA KATAA UCHAFU, SAFISHA, PENDESHA UBUNGO YAZINDULIWA, MITAA SAFI NA MICHAFU KUPEWA ZAWADI

    May 03, 2025
  • FANYENI KAZI, MSIJALI MASILAHI BINAFSI" ~ CHALAMILA

    May 01, 2025
  • HUDUMA YA KUJIFUNGUA KWA UPASUAJI YAANZA RASMI KITUO CHA AFYA GOBA,WANANCHI WAKARIBISHWA

    April 30, 2025
  • Tazama zote

Video

KIWANJA CHAKO KINA HATI? | UMEKUWA UKISUMBULIWA NA MIGOGORO YA ARDHI? | KARIBU KWENYE ARDHI CLINIC
More Videos

Viunganishi vya haraka

  • Leseni za biashara
  • Ushuru wa Hoteli
  • Kibali cha ujenzi
  • Sheria ndogondogo
  • Malengo na Dira
  • Muundo wa Uongozi
  • zabuni

Viunganishi linganifu

  • The National Examinations Council of Tanzania
  • TAMISEMI
  • Ministry of Education
  • President office State House
  • National Council for Technical Education
  • Ministry of Finace and Planning

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya wanaoingia

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Luguruni Area, Morogoro Road

    Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam

    Telephone: +255 22 2926341

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: md@ubungomc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa