• Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
Ubungo Municipal Council
Ubungo Municipal Council

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Ubungo Municipal Council

  • Home
  • About US
    • History
    • Mission and Vision
    • Core Values
  • Administration
    • Structure
    • Departments
      • Secondary Education
      • Agriculture, Livestock and Fisheries
      • Industry,Trade and Investments
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure, Rural and Urban Development
      • Pre-Primary and Primary Education
      • Human Resources Management and administration
      • Health, Social Welfare and Nutrition Services
      • Communit Development
    • Units
      • Legal Services
      • Internal Audit
      • ICT
      • Procument Management
      • Government Communication
      • Finance and Accounts
      • Sports, Culture and Arts
      • Waste Management and Sanitation
      • Natural Resources and Environment Conservation
    • Municipal By Laws
      • Municipal By Laws
      • Other Laws
  • Opportunities
    • Livestock
    • Agriculture
    • Markets
    • Bus Terminal
    • Industries
  • Services
    • Health
      • iCHF
      • Nutrition
      • Social welfare
    • Education
      • Pre and Primary Education
      • Secondary Education
    • Business
      • Service levy
      • Tax Registration
      • Business Licence
      • Hotel Levy
    • Enterpreneurship
      • Ten Percent Loans
    • Agriculture
    • Fishing
    • Livestock
      • UJUWA
  • Councilors
    • Councilors list
    • Council Committee
    • Council legal meeting
    • Meyor's schudule
  • Projects
    • Planned Projects
    • On going Projects
    • Completed projects
  • Publications
    • Guidelines
    • Application Forms
    • Reports
    • Acts
    • Bronchures
    • Tender Advert
    • Strategic Plan
    • Newsletter
  • Media Center
    • Photo Gallery
    • Video Gallery
    • Press Release
    • Speeches

BANDA LA UBUUNGO LAFURIKA, MAONESHO YA NANE NANE - MOROGORO

Posted on: August 8th, 2025

Banda la Ubungo Lafurika Nanenane Morogoro – Viongozi, Wananchi Wajionea Ubunifu na Maendeleo ya Sekta ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi

Ikiwa ni kilele cha sikukuu ya wakulima na sherehe za wavuvi na wafugaji zinazoendelea Katika maonesho ya Nanenane yanayoendelea katika viwanja vya Nanenane, banda la Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo limevutia mamia ya watu wakiwemo viongozi wa serikali, wananchi wa kawaida, wataalamu wa sekta mbalimbali pamoja na wanafunzi waliokuja kujifunza na kujionea kwa macho ubunifu na maendeleo ya sekta ya kilimo, mifugo na uvuvi.

Tangu kufunguliwa kwa maonesho hayo, kumekuwa na msururu wa watu wakimiminika katika banda hilo maarufu kutokana na namna lilivyoandaliwa kitaalamu, kuonyesha teknolojia bunifu, bidhaa za asili zilizoongezwa thamani, vipando bora vya mazao mbalimbali, mifugo yenye tija, na mbinu mpya za kisasa za uvuvi.

VIONGOZI WATEMBELEA, WAPONGEZA

Miongoni mwa viongozi waliotembelea banda hilo ni pamoja na Wakuu wa idara, vitengo na sehemu, viongozi wa mikoa na wilaya, wakuu wa taasisi mbalimbali za utafiti kutoka maeneo mbalimbali nchini.

Viongozi hao walionesha kufurahishwa na namna Manispaa ya Ubungo ilivyoweza kuonesha utekelezaji wa sera za serikali kwa vitendo kupitia ubunifu na matumizi ya teknolojia rafiki kwa wakulima na wafugaji.

Akizungumza baada ya kutembelea banda hilo, mmoja wa viongozi hao alisema:

"Hili ni banda la mfano. Ubungo wameonyesha dhahiri kuwa kilimo kinaweza kuwa cha kisasa na chenye faida. Hii ni hatua kubwa kuelekea mapinduzi ya kilimo nchini."

WANANCHI WAJIONEA FURSA NA KUJIFUNZA

Kwa upande wa wananchi waliofika, wengi wao walieleza kufurahishwa na maonyesho hayo ambayo yamewapa maarifa mapya kuhusu njia bora za kilimo cha umwagiliaji, ufugaji wa kisasa wa kuku, ng’ombe wa maziwa, pamoja na uzalishaji wa samaki kwenye mabwawa ya kisasa.

Aidha, vipando vya kisasa vya mazao kama mahindi, mihogo, mboga mboga, pamoja na miche ya matunda vilivutia wengi waliokuwa na shauku ya kuboresha shughuli zao za kilimo. Wengine walivutiwa na bidhaa za kuongeza thamani kama vile siagi ya karanga, sabuni za asili, unga wa mihogo, na juisi mbalimbali zilizotengenezwa kwa viungo vya asili.

Announcements

  • KIBALI CHA KUANZA KUTOZA USHURU WA KUSHUSHA NA KUPAKIA MIZIGO July 17, 2023
  • KUKANUSHA TAARIFA YA UWEPO WA HARAFU MBAYA STENDI YA MABASI MAGUFULI July 06, 2023
  • MATOKEO YA SENSA YA WATU NA MAKAZI 2022 Ubungo September 06, 2023
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI NAFASI YA DEREVA NA KATIBU MAHSUSI July 21, 2022
  • View All

Latest News

  • BANDA LA UBUUNGO LAFURIKA, MAONESHO YA NANE NANE - MOROGORO

    August 08, 2025
  • MHE.MALIMA KATIKA BANDA LA UBUNGO MAONESHO NANENANE

    August 06, 2025
  • UBUNGO YAADHIMISHA WIKI YA UNYONYESHAJI MAZIWA YA MAMA DUNIANI, ZAHANATI YA GOBA

    August 05, 2025
  • MAFUNZO YA WASIMAMIZI WA UCHAGUZI NGAZI YA KATA YAZINDULIWA

    August 04, 2025
  • View All

Video

KIWANJA CHAKO KINA HATI? | UMEKUWA UKISUMBULIWA NA MIGOGORO YA ARDHI? | KARIBU KWENYE ARDHI CLINIC
More Videos

Quick Links

  • Leseni za biashara
  • Ushuru wa Hoteli
  • Kibali cha ujenzi
  • Sheria ndogondogo
  • Malengo na Dira
  • Muundo wa Uongozi
  • zabuni

Related Links

  • The National Examinations Council of Tanzania
  • TAMISEMI
  • Ministry of Education
  • President office State House
  • National Council for Technical Education
  • Ministry of Finace and Planning

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Contact Us

    Luguruni Area, Morogoro Road

    Postal Address: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam

    Telephone: +255 22 2926341

    Mobile:

    Email: md@ubungomc.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • Site Map

Copyright ©2017Ubungo Municipal Council All rights reserved.