• Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
Ubungo Municipal Council
Ubungo Municipal Council

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Ubungo Municipal Council

  • Home
  • About US
    • History
    • Mission and Vision
    • Core Values
  • Administration
    • Structure
    • Departments
      • Secondary Education
      • Agriculture, Livestock and Fisheries
      • Industry,Trade and Investments
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure, Rural and Urban Development
      • Pre-Primary and Primary Education
      • Human Resources Management and administration
      • Health, Social Welfare and Nutrition Services
      • Communit Development
    • Units
      • Legal Services
      • Internal Audit
      • ICT
      • Procument Management
      • Government Communication
      • Finance and Accounts
      • Sports, Culture and Arts
      • Waste Management and Sanitation
      • Natural Resources and Environment Conservation
    • Municipal By Laws
      • Municipal By Laws
      • Other Laws
  • Opportunities
    • Livestock
    • Agriculture
    • Markets
    • Bus Terminal
    • Industries
  • Services
    • Health
      • iCHF
      • Nutrition
      • Social welfare
    • Education
      • Pre and Primary Education
      • Secondary Education
    • Business
      • Service levy
      • Tax Registration
      • Business Licence
      • Hotel Levy
    • Enterpreneurship
      • Ten Percent Loans
    • Agriculture
    • Fishing
    • Livestock
      • UJUWA
  • Councilors
    • Councilors list
    • Council Committee
    • Council legal meeting
    • Meyor's schudule
  • Projects
    • Planned Projects
    • On going Projects
    • Completed projects
  • Publications
    • Guidelines
    • Application Forms
    • Reports
    • Acts
    • Bronchures
    • Tender Advert
    • Strategic Plan
    • Newsletter
  • Media Center
    • Photo Gallery
    • Video Gallery
    • Press Release
    • Speeches

DC KHERI ARIDHISHWA NA MIKAKATI YA KUBORESHA MIUNDOMBINU YA SHULE

Posted on: June 23rd, 2021

Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe. Kheri Denice James ameridhishwa na mikakati iliyowekwa na Manispaa ya U bungo ya kuboresha miundombinu ya shule ikwemo utengenezaji wa madawati na ujenzi wa madarasa katika shule za manispaa hiyo ikiwa ni maandalizi ya kuwapokea wanafunzi wa darasa la kwanza na kitado cha kwanza kwa mwaka 2022.

Mhe. Kheri ametoa kauli hiyo leo juni 23, 2021 wakati wa ziara ya kikazi ya kutembelea miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika manispaa hiyo na kueleza kuwa mkakati wa kujenga madarasa na kutengeneza madawati mapema utaondoa changamoto ya upungufu wa miundombinu hiyo kwenye shule na hivyo kufanya wanafunzi kusoma katika mazingira bora.

“Kwa mwaka 2022 sitegemei Ubungo iwe kati ya Halmashauri zenye changamoto ya upungufu wa madarasa na madawati ikiwa mikakati yetu itatekelezwa kwa ufanisi na hii itafanikwa zaidi jamii na wadau wa maendeleo wakishirikishwa kikamilifu katika kulitekeleza hili, kila mmoja atekeleze wajibu wake” alieleza Mhe. Kheri

Mhe. Kheri ameendelea kusema kuwa, kama  idadi ya wanafunzi wanaoratajia kujiunga na kidato cha kwanza kwa mwaka ujao tunayo ni dhahiri mahitaji ya madarasa na madawati yatakayotumika yanajulikana hivyo  naagiza madarasa hayo  yaanze kujengwa mapema  mwezi  julai  na hadi mwezi disemba yawe yamekamilika tayari kwa kuwapokea wanafunzi januari 2022.

Aidha, Mhe. Kheri amewapongeza wadau wa maendeleo wakiwemo benki ya CRDB, NMB na Kanisa Katoliki  kwa mchango wao mkubwa katika kuboresha miundombinu ya shule ya sekondari mashujaa iliyoko kata ya Sinza  kwa kujenga madarasa, fensi na  utengenezaji wa viti na meza hali inayoifanya shule hiyo kuwa na mazingira mazuri ya kujifunza na kujifunzia

“Huu mkakati wa kuboresha miundombinu katika shule zetu unapaswa kuwa shirikishi ili kila mtu awe na mchango katika kufanikisha zoezi hili mfano mzuri ni katika shule ya sekondari mashujaa ambapo kanisa katoliki limetoa milioni 20 kwa ajili ya ujenzi wa ukuta wa shule, nawashukuru na kuwapongeza sana viongozi wengine tuige mfano wa uongozi wa shule hiinamna ulivyoshirikisha wadau”

Mhe. Kheri amezitaka bodi na kamati za shule zote za Manispaa ya Ubungo kutekeleza majukumu yao ipasavyo katika kusimamia na kubuni mikakati itakayozifanya shule zetu kuondokana na changamoto mbalimbali ikiwemo madarasa na madawati  badala ya kusubiri serikali pekee itatue changamoto hizo.

“ifike wakati bodi na kamti za shule zishindanishwe kwa ubunifu wa kuboresha miundombinu ya shule hii itasaidia kuwakumbusha wajumbe majukumu yao ya msingi badala ya kufanya kazi kwa mazoea” alielekeza Mhe. Kheri.

Akieleza moja ya  mkakati wa manispaa, Mkurugenzi wa Manispaa hiyo Beatrice Dominic amesema kuwa pamoja na ujenzi wa madarasa unaoendelea katika shule mbalimbali, kwa mwaka  mpya wa fedha unaonza mwezi Julai 2021 manispaa imepanga kujenga madarasa 100 lengo likiwa ni kuhakikisha changamoto ya upungufu wa  madarasa na madawati inapungua kwa kiasi kikubwa.

Mhe.  Mkuu wa Wilaya Ubungo  ametembelea miradi yenye thamani ya shilingi bilioni 59.8 ikiwemo mradi wa ujenzi wa  kituo kikuu cha mabasi  cha magufuli kilichogharimu bilioni 56.

Announcements

  • KIBALI CHA KUANZA KUTOZA USHURU WA KUSHUSHA NA KUPAKIA MIZIGO July 17, 2023
  • KUKANUSHA TAARIFA YA UWEPO WA HARAFU MBAYA STENDI YA MABASI MAGUFULI July 06, 2023
  • MATOKEO YA SENSA YA WATU NA MAKAZI 2022 Ubungo September 06, 2023
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI NAFASI YA DEREVA NA KATIBU MAHSUSI July 21, 2022
  • View All

Latest News

  • MIRADI 7 YENYE THAMANI YA BILIONI 8.2 UBUNGO YAPITA KWA KISHINDO MBIO ZA MWENGE WA UHURU 2025

    June 05, 2025
  • TUZINGATIE USAFI KUEPUKA MAGONJWA

    May 31, 2025
  • BODI YA AFYA UBUNGO YAPONGEZA WATAALAM WA AFYA NA KUTOA MAAGIZO YAKUBORESHA NYANJA MBALIMBALI

    May 29, 2025
  • MAAFISA HABARI HAKIKISHENI MNATANGAZA UTEKELEZAJI WA MIRADI KWA WANANCHI

    May 24, 2025
  • View All

Video

KIWANJA CHAKO KINA HATI? | UMEKUWA UKISUMBULIWA NA MIGOGORO YA ARDHI? | KARIBU KWENYE ARDHI CLINIC
More Videos

Quick Links

  • Leseni za biashara
  • Ushuru wa Hoteli
  • Kibali cha ujenzi
  • Sheria ndogondogo
  • Malengo na Dira
  • Muundo wa Uongozi
  • zabuni

Related Links

  • The National Examinations Council of Tanzania
  • TAMISEMI
  • Ministry of Education
  • President office State House
  • National Council for Technical Education
  • Ministry of Finace and Planning

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Contact Us

    Luguruni Area, Morogoro Road

    Postal Address: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam

    Telephone: +255 22 2926341

    Mobile:

    Email: md@ubungomc.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • Site Map

Copyright ©2017Ubungo Municipal Council All rights reserved.