• Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
Ubungo Municipal Council
Ubungo Municipal Council

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Ubungo Municipal Council

  • Home
  • About US
    • History
    • Mission and Vision
    • Core Values
  • Administration
    • Structure
    • Departments
      • Secondary Education
      • Agriculture, Livestock and Fisheries
      • Industry,Trade and Investments
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure, Rural and Urban Development
      • Pre-Primary and Primary Education
      • Human Resources Management and administration
      • Health, Social Welfare and Nutrition Services
      • Communit Development
    • Units
      • Legal Services
      • Internal Audit
      • ICT
      • Procument Management
      • Government Communication
      • Finance and Accounts
      • Sports, Culture and Arts
      • Waste Management and Sanitation
      • Natural Resources and Environment Conservation
    • Municipal By Laws
      • Municipal By Laws
      • Other Laws
  • Opportunities
    • Livestock
    • Agriculture
    • Markets
    • Bus Terminal
    • Industries
  • Services
    • Health
      • iCHF
      • Nutrition
      • Social welfare
    • Education
      • Pre and Primary Education
      • Secondary Education
    • Business
      • Service levy
      • Tax Registration
      • Business Licence
      • Hotel Levy
    • Enterpreneurship
      • Ten Percent Loans
    • Agriculture
    • Fishing
    • Livestock
      • UJUWA
  • Councilors
    • Councilors list
    • Council Committee
    • Council legal meeting
    • Meyor's schudule
  • Projects
    • Planned Projects
    • On going Projects
    • Completed projects
  • Publications
    • Guidelines
    • Application Forms
    • Reports
    • Acts
    • Bronchures
    • Tender Advert
    • Strategic Plan
    • Newsletter
  • Media Center
    • Photo Gallery
    • Video Gallery
    • Press Release
    • Speeches

KAMPUNI YA YAPI MERKEZI YATOA MSAADA MILIONI 230 KUBORESHA MIUNDOMBINU YA SHULE UBUNGO

Posted on: January 26th, 2021

Mkuu wa Wilaya ya Ubungo jijini Dar Es salaam Mhe Kisare Makori anatarajia kupokea msaada wa fedha shilingi milioni 230 kutoka kampuni ya Yapi Merkezi kwa ajili ya   kujenga miundombinu ya Shule za Msingi na Sekondari wilayani humo.


Kampuni ya Yapi Merkezi inayofanya kazi ya ujenzi wa reli ya kisasa (SGR)   imetoa ahadi hiyo Leo januari 26, 2021 kwenye kikao kilichofanyika kwenye Ofisi ya Mkuu wa Wilaya hiyo na kueleza kuwa msaada huo ni sehemu ya wajibu wa kampuni kusaidia jamii katika changamoto mbalimbali.


Akiongea baada ya kupokea ahadi hiyo, Mkuu wa Wilaya huyo, ameishukuru kampuni hiyo kwa msaada wao katika kuboresha miundombinu ya Shule hususani Madarasa na madawati ambayo kwa sasa uhitaji wake ni mkubwa.


"Kwa niaba ya Serikali na wananchi wa Wilaya ya Ubungo napenda kuishukuru kampuni ya Hapi Merkezi kwa msaada wao kwani utasaidia kupunguza changamoto ya upungufu wa madarasa, madawati na vyoo kwenye shule zetu" ameeleza Makori

Mkori ameendelea kueleza kuwa , msaada huo utaelekezwa  kwenye shule zenye changamoto kubwa zaidi  ya madarasa na madawati  ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa agizo la Serikali la kuhakikisha wanafunzi wote hawakai chini wala kusomea nje.


Kwa upande wake Mkurugenzi wa Manispaa  ya Ubungo, Beatrice Dominic ameeleza kuwa ujenzi wa vyumba 37 kwa ajili ya kidato cha Kwanza  unaendelea na madawati 2000 yameagizwa na yameanza kupokekelewa na kusambazwa kwenye shule zenye upungufu. 


Aidha Beatrice amewaomba wadau wengine kuendelea kuchangia sekta ya elimu kwani uhitaji wa miundombinu ya Madarasa, madawati na vyoo kwa ajili ya kuboresha mazingira ya kujifunza na kujifunzia bado ni mkubwa sana.

Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Beatrice Dominic akitoa maelezo ya hali ya miundombinu kwa wawakilishi kutoka kampuni ya Yapi merkezi  wakati walipotembelea shule ya msindi Bwawani leo tarehe 26 januari, 2021


Announcements

  • KIBALI CHA KUANZA KUTOZA USHURU WA KUSHUSHA NA KUPAKIA MIZIGO July 17, 2023
  • KUKANUSHA TAARIFA YA UWEPO WA HARAFU MBAYA STENDI YA MABASI MAGUFULI July 06, 2023
  • MATOKEO YA SENSA YA WATU NA MAKAZI 2022 Ubungo September 06, 2023
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI NAFASI YA DEREVA NA KATIBU MAHSUSI July 21, 2022
  • View All

Latest News

  • MIAKA MINNE YA MAFANIKIO: UTELEKELEZA WA MIRADI YA MAENDELEO KATIKA HALMASHAURI YA MANISPAA YA UBUNGO CHINI YA UONGOZI WA RAIS SAMIA

    September 02, 2025
  • MIKOPO YA HALMASHAURI YACHOCHEA MAFANIKIO YA WAJASIRIAMALI

    September 30, 2025
  • UBUNGO YAAHIDI KUJIPANGA IMARA ZAIDI KWA MSIMU UJAO WA SHIMISEMITA | YAPOTEZA MBELE YA DODOMA JIJI

    August 29, 2025
  • WANANCHI MSIGANI WAANZA KUNUFAIKA NA MAFUNZO YA KILIMO MJINI.

    August 29, 2025
  • View All

Video

KIWANJA CHAKO KINA HATI? | UMEKUWA UKISUMBULIWA NA MIGOGORO YA ARDHI? | KARIBU KWENYE ARDHI CLINIC
More Videos

Quick Links

  • Leseni za biashara
  • Ushuru wa Hoteli
  • Kibali cha ujenzi
  • Sheria ndogondogo
  • Malengo na Dira
  • Muundo wa Uongozi
  • zabuni

Related Links

  • The National Examinations Council of Tanzania
  • TAMISEMI
  • Ministry of Education
  • President office State House
  • National Council for Technical Education
  • Ministry of Finace and Planning

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Contact Us

    Luguruni Area, Morogoro Road

    Postal Address: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam

    Telephone: +255 22 2926341

    Mobile:

    Email: md@ubungomc.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • Site Map

Copyright ©2017Ubungo Municipal Council All rights reserved.