• Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
Ubungo Municipal Council
Ubungo Municipal Council

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Ubungo Municipal Council

  • Home
  • About US
    • History
    • Mission and Vision
    • Core Values
  • Administration
    • Structure
    • Departments
      • Secondary Education
      • Agriculture, Livestock and Fisheries
      • Industry,Trade and Investments
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure, Rural and Urban Development
      • Pre-Primary and Primary Education
      • Human Resources Management and administration
      • Health, Social Welfare and Nutrition Services
      • Communit Development
    • Units
      • Legal Services
      • Internal Audit
      • ICT
      • Procument Management
      • Government Communication
      • Finance and Accounts
      • Sports, Culture and Arts
      • Waste Management and Sanitation
      • Natural Resources and Environment Conservation
    • Municipal By Laws
      • Municipal By Laws
      • Other Laws
  • Opportunities
    • Livestock
    • Agriculture
    • Markets
    • Bus Terminal
    • Industries
  • Services
    • Health
      • iCHF
      • Nutrition
      • Social welfare
    • Education
      • Pre and Primary Education
      • Secondary Education
    • Business
      • Service levy
      • Tax Registration
      • Business Licence
      • Hotel Levy
    • Enterpreneurship
      • Ten Percent Loans
    • Agriculture
    • Fishing
    • Livestock
      • UJUWA
  • Councilors
    • Councilors list
    • Council Committee
    • Council legal meeting
    • Meyor's schudule
  • Projects
    • Planned Projects
    • On going Projects
    • Completed projects
  • Publications
    • Guidelines
    • Application Forms
    • Reports
    • Acts
    • Bronchures
    • Tender Advert
    • Strategic Plan
    • Newsletter
  • Media Center
    • Photo Gallery
    • Video Gallery
    • Press Release
    • Speeches

DC MSANDO ATEMBELEA MRADI WA MAJI KING'ONG'O, AONGEZA MUDA KWA DAWASA KUKAMILISHA KWA UBORA

Posted on: October 13th, 2025

Na Mwandishi Wetu, UbungoOktoba 13, 2025 – Dar es Salaam

Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Mheshimiwa Albert Msando, leo amefanya ziara ya ukaguzi katika eneo la Michungwani, Kata ya Saranga, kufuatilia utekelezaji wa mradi wa uboreshaji wa huduma ya maji unaogharimu Shilingi milioni 364, unaotekelezwa na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA).

Mradi huo unaolenga kuboresha upatikanaji wa maji safi kwa wakazi wa mitaa ya King’ong’o, Michungwani na Kimara B, unatarajiwa kunufaisha zaidi ya wananchi 92,000 katika umbali wa takriban kilomita 3.6.

Katika Mazungumzo yake baada ya kukagua uchimbaji wa mitaro kwaajili ya usambazaji wa mabomba, Mh. Msando amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kutoa fedha za utekelezaji wa miradi ya maendeleo, hususan miradi ya maji inayogusa maisha ya wananchi moja kwa moja.

Amesema uamuzi wa serikali umeonyesha dhamira ya kweli katika kutatua changamoto za msingi zinazowakabili wananchi.

Kutokana na umuhimu wa mradi huo na changamoto ya upatikanaji wa maji kwa wananchi, Mh. Msando aliielekeza DAWASA kuongeza muda wa utekelezaji wa mradi huo kutoka siku 10 hadi siku 21. Alieleza kuwa uamuzi huo unalenga kuhakikisha kazi inafanyika kwa viwango vya juu na kwa ubora utakaodumu.

"Nia yetu si kukamilisha kwa haraka tu, bali kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora, inayodumu na yenye kuleta unafuu wa kweli kwa maisha yao," alisema Msando.

Kwa upande wake, Mkuu wa kitengo cha Mazingira DAWASA aliyemwakilisha Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu DAWASA Mhandisi Modester Mushi amewahakikishia wananchi na uongozi wa wilaya kuwa kazi hiyo itafanyika kwa kasi kubwa, mchana na usiku, ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma hiyo muhimu kwa wakati na kwa ubora unaostahili. Alisisitiza kuwa DAWASA iko tayari kutekeleza maono ya Mhe. Rais ya kuhakikisha kila Mtanzania anapata huduma ya maji safi na salama.

Naye Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa ya Michungwani Bw. Sergius Kinyero, amesema ujio wa mradi huo ni mkombozi mkubwa kwa wananchi wake


Announcements

  • KIBALI CHA KUANZA KUTOZA USHURU WA KUSHUSHA NA KUPAKIA MIZIGO July 17, 2023
  • KUKANUSHA TAARIFA YA UWEPO WA HARAFU MBAYA STENDI YA MABASI MAGUFULI July 06, 2023
  • MATOKEO YA SENSA YA WATU NA MAKAZI 2022 Ubungo September 06, 2023
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI NAFASI YA DEREVA NA KATIBU MAHSUSI July 21, 2022
  • View All

Latest News

  • UBUNGO YAADHIMISHA SIKU YA UONI DUNIANI KWA UPIMAJI BURE WA MACHO ZAHANATI YA GOBA

    October 15, 2025
  • DC MSANDO ATEMBELEA MRADI WA MAJI KING'ONG'O, AONGEZA MUDA KWA DAWASA KUKAMILISHA KWA UBORA

    October 13, 2025
  • DC MSANDO AWATAKA WENYEVITI KUWASILISHA TAARIFA YA MAPATO NA MATUMIZI

    October 04, 2025
  • SERIKALI KUJA NA MPANGO WA DHARURA NA HARAKA KUTATUA CHANGAMOTO YA USAFIRI WA MWENDOKASI

    October 01, 2025
  • View All

Video

UBUNGO YAADHIMISHA SIKU YA MTOTO WA AFRIKA | WANAFUNZI WAASWA KUJITUNZA
More Videos

Quick Links

  • Leseni za biashara
  • Ushuru wa Hoteli
  • Kibali cha ujenzi
  • Sheria ndogondogo
  • Malengo na Dira
  • Muundo wa Uongozi
  • zabuni

Related Links

  • The National Examinations Council of Tanzania
  • TAMISEMI
  • Ministry of Education
  • President office State House
  • National Council for Technical Education
  • Ministry of Finace and Planning

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Contact Us

    Luguruni Area, Morogoro Road

    Postal Address: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam

    Telephone: +255 22 2926341

    Mobile:

    Email: md@ubungomc.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • Site Map

Copyright ©2017Ubungo Municipal Council All rights reserved.