• Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
Ubungo Municipal Council
Ubungo Municipal Council

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Ubungo Municipal Council

  • Home
  • About US
    • History
    • Mission and Vision
    • Core Values
  • Administration
    • Structure
    • Departments
      • Secondary Education
      • Agriculture, Livestock and Fisheries
      • Industry,Trade and Investments
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure, Rural and Urban Development
      • Pre-Primary and Primary Education
      • Human Resources Management and administration
      • Health, Social Welfare and Nutrition Services
      • Communit Development
    • Units
      • Legal Services
      • Internal Audit
      • ICT
      • Procument Management
      • Government Communication
      • Finance and Accounts
      • Sports, Culture and Arts
      • Waste Management and Sanitation
      • Natural Resources and Environment Conservation
    • Municipal By Laws
      • Municipal By Laws
      • Other Laws
  • Opportunities
    • Livestock
    • Agriculture
    • Markets
    • Bus Terminal
    • Industries
  • Services
    • Health
      • iCHF
      • Nutrition
      • Social welfare
    • Education
      • Pre and Primary Education
      • Secondary Education
    • Business
      • Service levy
      • Tax Registration
      • Business Licence
      • Hotel Levy
    • Enterpreneurship
      • Ten Percent Loans
    • Agriculture
    • Fishing
    • Livestock
      • UJUWA
  • Councilors
    • Councilors list
    • Council Committee
    • Council legal meeting
    • Meyor's schudule
  • Projects
    • Planned Projects
    • On going Projects
    • Completed projects
  • Publications
    • Guidelines
    • Application Forms
    • Reports
    • Acts
    • Bronchures
    • Tender Advert
    • Strategic Plan
    • Newsletter
  • Media Center
    • Photo Gallery
    • Video Gallery
    • Press Release
    • Speeches

GHARAMA ZA UPANGISHAJI ZASHUSHWA STENDI YA MABASI YA MAGUFULI

Posted on: September 13th, 2022

Mapema Leo tarehe 13/09/2022 Manispaa ya Ubungo imekutana na wafanyabiashara waliopanga kwenye fremu na vizimba vya Kituo cha Magufuli Bus Terminal lengo ikiwa ni kuweka mikakati juu ya ulipaji wa kodi mpya za upangishaji tofauti na zile za awali.


Kikao hicho kimejumuisha wapangaji wa Jengo la Utawala, Jengo la Abiria na Wamiliki wa Mabasi wenye ofisi za kukatisha tiketi wa Kituo hicho ambapo hapo awali gharama za upangishaji walikuwa wakilipia Tsh 40,000/= kwa square mita moja.

Akiongea katika kikao hicho Mkurugenzi wa Manispaa hiyo Beatrice Dominic ameeleza kuwa ombi la wapangaji hao la kushushiwa gharama za kodi limefanyiwa kazi kwa kupunguzwa kwa kiasi ambacho ni rahisi kwa kila mfanyabiashara kulipia.


Beatrice ameendelea kueleza kuwa kodi hizo mpya zimeanza kuchajiwa kuanzia tarehe 01/07/2022 na kwamba kutokana na ushushwaji wa kodi hizo, kwa sasa kila mfanya biashara atawajibika kulipia gharama za umeme kutokana na matumizi yake kwa utaratibu utakaopangwa isipokuwa gharama za maji zitaendelea kugharamiwa na Manispaa kama ilivyokuwa hapo awali.


Akiendelea kufafanua Mkuu wa Kitengo cha Fedha wa Manispaa hiyo George Mzeru ameeleza kuwa kodi hizo kwa sasa zitalipwa kwa mchanganuo ufuatao Wafanyabiashara wa Jengo la Utawala kwa Sakafu ya chini (ground floor) Tsh 25,000, Floor ya kwanza Tsh 24,500, Floor ya pili Tsh 24,000 na Floor ya mwisho ambayo ni ya Tatu italipiwa Tsh 22,000.


George ameendelea kueleza kuwa kwa Wafanyabiashara wa Jengo la abiria ambalo chini Lina basement kwahivo floor ya kwanza (mezzanine floor) itakuwa Tsh 22,500, floor ya kwanza Tsh 22,000 na floor ya pili ambayo ni ya mwisho italipiwa Tsh 22,000

Nae Mkuu wa kitengo cha sheria wa Manispaa hiyo Kissah Mbila amewataka Wafanyabiashara hao kuhakikisha hadi kufikia tarehe 25/09/2022 wote wawe wameshalipia kodi ya mwezi Julai, Agosti na September 2022 na kupatiwa mkataba wake na ambae atafanya kinyume na hapo hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.


Kissah ameendelea kueleza kuwa mfanyabiashara mwenye madeni ya nyuma ya mwezi Julai atapatiwa mkataba wa makubaliano ya malipo ya madeni yao ya nyuma kwa gharama za awali


#ubungoyetufahariyetu

#UbungoYaKibingwa

Announcements

  • KIBALI CHA KUANZA KUTOZA USHURU WA KUSHUSHA NA KUPAKIA MIZIGO July 17, 2023
  • KUKANUSHA TAARIFA YA UWEPO WA HARAFU MBAYA STENDI YA MABASI MAGUFULI July 06, 2023
  • MATOKEO YA SENSA YA WATU NA MAKAZI 2022 Ubungo September 06, 2023
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI NAFASI YA DEREVA NA KATIBU MAHSUSI July 21, 2022
  • View All

Latest News

  • NI LAZIMA UJENZI WA UKUTA UANZE NA KUKAMILIKA" DC MSANDO

    May 12, 2025
  • CHALAMILA AZINDUA BIASHARA SAA 24 UBUNGO

    May 09, 2025
  • KATA YA UBUNGO YAKABIDHI MKOPO WA TSH. 122,800,000/= KWA VIKUNDI SITA VYA ASILIMIA 10

    May 02, 2025
  • KAMPENI YA KATAA UCHAFU, SAFISHA, PENDESHA UBUNGO YAZINDULIWA, MITAA SAFI NA MICHAFU KUPEWA ZAWADI

    May 03, 2025
  • View All

Video

KIWANJA CHAKO KINA HATI? | UMEKUWA UKISUMBULIWA NA MIGOGORO YA ARDHI? | KARIBU KWENYE ARDHI CLINIC
More Videos

Quick Links

  • Leseni za biashara
  • Ushuru wa Hoteli
  • Kibali cha ujenzi
  • Sheria ndogondogo
  • Malengo na Dira
  • Muundo wa Uongozi
  • zabuni

Related Links

  • The National Examinations Council of Tanzania
  • TAMISEMI
  • Ministry of Education
  • President office State House
  • National Council for Technical Education
  • Ministry of Finace and Planning

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Contact Us

    Luguruni Area, Morogoro Road

    Postal Address: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam

    Telephone: +255 22 2926341

    Mobile:

    Email: md@ubungomc.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • Site Map

Copyright ©2017Ubungo Municipal Council All rights reserved.