• Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
Ubungo Municipal Council
Ubungo Municipal Council

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Ubungo Municipal Council

  • Home
  • About US
    • History
    • Mission and Vision
    • Core Values
  • Administration
    • Structure
    • Departments
      • Secondary Education
      • Agriculture, Livestock and Fisheries
      • Industry,Trade and Investments
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure, Rural and Urban Development
      • Pre-Primary and Primary Education
      • Human Resources Management and administration
      • Health, Social Welfare and Nutrition Services
      • Communit Development
    • Units
      • Legal Services
      • Internal Audit
      • ICT
      • Procument Management
      • Government Communication
      • Finance and Accounts
      • Sports, Culture and Arts
      • Waste Management and Sanitation
      • Natural Resources and Environment Conservation
    • Municipal By Laws
      • Municipal By Laws
      • Other Laws
  • Opportunities
    • Livestock
    • Agriculture
    • Markets
    • Bus Terminal
    • Industries
  • Services
    • Health
      • iCHF
      • Nutrition
      • Social welfare
    • Education
      • Pre and Primary Education
      • Secondary Education
    • Business
      • Service levy
      • Tax Registration
      • Business Licence
      • Hotel Levy
    • Enterpreneurship
      • Ten Percent Loans
    • Agriculture
    • Fishing
    • Livestock
      • UJUWA
  • Councilors
    • Councilors list
    • Council Committee
    • Council legal meeting
    • Meyor's schudule
  • Projects
    • Planned Projects
    • On going Projects
    • Completed projects
  • Publications
    • Guidelines
    • Application Forms
    • Reports
    • Acts
    • Bronchures
    • Tender Advert
    • Strategic Plan
    • Newsletter
  • Media Center
    • Photo Gallery
    • Video Gallery
    • Press Release
    • Speeches

MANISPAA YA UBUNGO YAKABIDHI VITI NA MEZA 200 KWA AJILI YA KIDATO CHA KWANZA

Posted on: January 8th, 2021

Ikiwa  zimebaki Siku chache kufunguliwa kwa shule, Manispaa ya Ubungo leo januari 8, 2021 imekabidho madawati 200 shule za sekondari  ambazo zina upungufu wa viti na meza ikiwa ni maandalizi ya kuwapokea wanafunzi wa  kidato cha kwanza kwa mwaka 2021.

Akizungumza wakati wa kukabidhi viti na meza hizo, Afisa elimu wa Manispaa hiyo Hilda sharanda amesema kuwa Manispaa imekabidhi viti na meza hivyo 200 kwa shule za sekondari ikiwa ni moja ya mkakati wake wa hukakikisha wanafunzi wa kidato cha kwanza kutoshindwa kusoma kwa sababu ya ukosefu wa viti na meza.

Sharanda ameeleza kuwa,   Wanafunzi wote 13, 347 walichaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza watasoma katika mazingira mazuri kwani Manispaa imetoa fedha shilingi milioni 115  kwa ajili ya kutengeneza viti na meza ambapo kwa leo tu akabidhi viti na meza hizi 200 huku vingine 1000 ikiwa hatua za mwisho za matengenezo

Kwa ujumla, shule zina upungufu wa viti na meza 2847 kati ya 10500 vilivyopo ambapo katika upungufu huo viti 1200 vinatengenezwa na Manispaa kupitia mapato ya ndani,  1000 vimefanyiwa ukarabati shuleni hivyo tunaendelea kuomba wadau wengine waendelee kutusaidia ukizingatia elimu ni sekta mhimu sana kwa ustawi wa jamii na Taifa kwa ujumla.

Kwa upande wa vyumba cha madarasa , sharanda amesema kuwa   wanafunzi 13,347 waliofaulu kujiunga kidato cha kwanza wanahitaji vyumba cha madarasa  268 lakini vyumba 231 vipo na hivyo  kufanya upungufu wa vyumba 37

Aidha, sharanda amesema,   katika kukabiliana na upungufu huo manispaa imetoa fedha milioni 500 kwa ajili ya ujenzi wa vyumba cha madarasa 37 ambapo utekelezaji wake upo hatua mbalimbali lengo ikiwa ni kuhakikisha wanafunzi wote walichaguliwa kuanza kidato cha kwanza  hawaikosi furss hiyo kutokana na ukosefu wa madarasa ya kusomea.

Kutokana na juhudi hizi za Manispaa na  serikali kwa ujumla, sharanda amewataka wazazi na walezi wahakikishe wanafunzi wote waliochaguliwa kujiunga kidato cha kwanza wanaripoti shule kwa wakati wakiwa na mahitaji yote ya msingi kwani mazingira ya kujifunzia yako vizuri yaani Walimu, madarasa na madawati.

Akiongea wakati wa kukabidhiwa viti na meza kwa ajili ya kidato cha kwanza Mwalimu Andrea Ndagire kutoka shule ya sekondari Kibweheri ameishukuru serikali kupitia Manispaa ya Ubungo kwa kutoa viti na meza hizo kwani vitapunguza kwa Miesi kikubwa upungufu uliokuwepo shuleni mwaka

Aidha Mwalimu Ndagire ameeleza kuwa kitendo cha Manispaa ya hiyo kutumia fedha nyingi kwa ajili ya kutatua changamoto katika sekta ya elimu ni kutekeleza kwa vitendo Dhana ya uchumi wa kati kwa vitendo maana wanafunzi anakuwa katika mazingira mazuri ya kujifunzia na hivyo kuwa na Taifa bora ukizingatia elimu ni msingi wa ustawi wa sekta zingine.

Walter priscus prosper ni moja ya wanafunzi walichaguliwa kujiunga kidato cha kwanza katika shule ya sekondari kimara, ameipongeza serikali  kwa kutoa viti na meza kwenye shule zake ili wanafunzi wasome katika mazingira mazuri.

"Kwa niaba ya wanafunzi wenzangu tunaahidi kusoma kwa bidii ili fedha zinazotumika kujenga miundombinu ya shule pamoja na utoaji wa elimu bila malipo zisipotee bure" aliahidi mwanafunzi prosper.

Announcements

  • KIBALI CHA KUANZA KUTOZA USHURU WA KUSHUSHA NA KUPAKIA MIZIGO July 17, 2023
  • KUKANUSHA TAARIFA YA UWEPO WA HARAFU MBAYA STENDI YA MABASI MAGUFULI July 06, 2023
  • MATOKEO YA SENSA YA WATU NA MAKAZI 2022 Ubungo September 06, 2023
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI NAFASI YA DEREVA NA KATIBU MAHSUSI July 21, 2022
  • View All

Latest News

  • MIRADI 7 YENYE THAMANI YA BILIONI 8.2 UBUNGO YAPITA KWA KISHINDO MBIO ZA MWENGE WA UHURU 2025

    June 05, 2025
  • TUZINGATIE USAFI KUEPUKA MAGONJWA

    May 31, 2025
  • BODI YA AFYA UBUNGO YAPONGEZA WATAALAM WA AFYA NA KUTOA MAAGIZO YAKUBORESHA NYANJA MBALIMBALI

    May 29, 2025
  • MAAFISA HABARI HAKIKISHENI MNATANGAZA UTEKELEZAJI WA MIRADI KWA WANANCHI

    May 24, 2025
  • View All

Video

KIWANJA CHAKO KINA HATI? | UMEKUWA UKISUMBULIWA NA MIGOGORO YA ARDHI? | KARIBU KWENYE ARDHI CLINIC
More Videos

Quick Links

  • Leseni za biashara
  • Ushuru wa Hoteli
  • Kibali cha ujenzi
  • Sheria ndogondogo
  • Malengo na Dira
  • Muundo wa Uongozi
  • zabuni

Related Links

  • The National Examinations Council of Tanzania
  • TAMISEMI
  • Ministry of Education
  • President office State House
  • National Council for Technical Education
  • Ministry of Finace and Planning

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Contact Us

    Luguruni Area, Morogoro Road

    Postal Address: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam

    Telephone: +255 22 2926341

    Mobile:

    Email: md@ubungomc.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • Site Map

Copyright ©2017Ubungo Municipal Council All rights reserved.