• Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
Ubungo Municipal Council
Ubungo Municipal Council

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Ubungo Municipal Council

  • Home
  • About US
    • History
    • Mission and Vision
    • Core Values
  • Administration
    • Structure
    • Departments
      • Secondary Education
      • Agriculture, Livestock and Fisheries
      • Industry,Trade and Investments
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure, Rural and Urban Development
      • Pre-Primary and Primary Education
      • Human Resources Management and administration
      • Health, Social Welfare and Nutrition Services
      • Communit Development
    • Units
      • Legal Services
      • Internal Audit
      • ICT
      • Procument Management
      • Government Communication
      • Finance and Accounts
      • Sports, Culture and Arts
      • Waste Management and Sanitation
      • Natural Resources and Environment Conservation
    • Municipal By Laws
      • Municipal By Laws
      • Other Laws
  • Opportunities
    • Livestock
    • Agriculture
    • Markets
    • Bus Terminal
    • Industries
  • Services
    • Health
      • iCHF
      • Nutrition
      • Social welfare
    • Education
      • Pre and Primary Education
      • Secondary Education
    • Business
      • Service levy
      • Tax Registration
      • Business Licence
      • Hotel Levy
    • Enterpreneurship
      • Ten Percent Loans
    • Agriculture
    • Fishing
    • Livestock
      • UJUWA
  • Councilors
    • Councilors list
    • Council Committee
    • Council legal meeting
    • Meyor's schudule
  • Projects
    • Planned Projects
    • On going Projects
    • Completed projects
  • Publications
    • Guidelines
    • Application Forms
    • Reports
    • Acts
    • Bronchures
    • Tender Advert
    • Strategic Plan
    • Newsletter
  • Media Center
    • Photo Gallery
    • Video Gallery
    • Press Release
    • Speeches

MANISPAA YA UBUNGO YATOA BILIONI 1.1 KWA VIKUNDI 111

Posted on: January 7th, 2021

Manispaa ya Ubungo jijini Dar Es salaam leo januari 7 2020 imetoa mikopo isiyo na riba yenye thamani ya shilingi bilioni 1.1 kwa vikundi  111 vya  wanawake, vijana na watu wenye ulemavu  kwa ajili kuendeleza na kukuza mitaji  ya biashara zao na hatimaye kujikwamua na umasikini.

Mikopo hiyo iliyotolewa leo baada ya kupata mafunzo ya namna ya kuendesha biashara zao kwa vikundi hivyo vyenye wanufaika  1566 ambapo vikundi vya wanawake 62 vitapata shilingi milioni 560,135,200, milioni 424 161,000 kwa vikundi 38  vya vijana na  milioni 119 , 000, 000 kwa ajili ya vikundi 11 vya watu wenye ulemavu.

Wanufaika wa mikopo wakifuatilia mafunzo kabla ya kukabidhiwa mikopo


Akizungumza wakati wa kufungua mafunzo hayo na kutoa hundi ya mikopo kwa vikundi hivyo, Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Kisare Makori  amewaeleza wajasiliamali hao kuwa utoaji wa mikopo hiyo ni utekelezaji wa sera ya serikali inayozitaka Halmashauri kutenga asilimia 10 ya mapato ya ndani kwa ajili ya kuwezesha wananchi kiuchumi na kuondokana na umasikini

Makori amesema kuwa "Nawapongeza kwa kukidhi vigezo na kupata mikopo hii, nawasii  mkaitumie mikopo hii kwa ajili ya kukuza biashara zenu na sio kununua vijora vya sherehe kwani serikali imeamuankutoa mikopo hii isiyo na riba ili ujasiriamali uwe njia ya kumkwamua mwananchi kiuchumi kwa kukuza mitaji yao"

Makori ameendelea kueleza kuwa utoaji wa mikopo hiyo unaenda  sambamba na kufanya marejesho kwa wakati ili kuongeza fursa kwa watu wengine kupata mikopo lakini pia kuongeza kiwango cha kukopesha " hivyo rejesheni mikopo kwa wakati"

"Tusififishe ndoto na nia njema ya serikali ya kukuza uchumi wa wananchi kwa kutorejesha, hengeni nidhamu na uaminifu kwenye marejesho ili tupanue wigo wa kukopesha watu wengi zaidi na kutengeneza mabilioni" amesisitiza Makori

Kwa upande wake mratibu wa mfuko wa wanawake vijana na walemavu wa manispaa hiyo Elizabeth Kebwe ameeleza kuwa vikundi vinavyopata mkopo awamu hii vinajishughulisha na shughuli za kilimo,  mifugo, uzalishaji mali, usindikaji wa bidhaa mbalimbali, viwanda vidogovidogo ambavyo vimekidhi vigezo wa kupata mkopo.

Kebwe amesema kuwa kwa  kipindi cha miaka 3 kuanzia mwaka 2017 hadi 2019, Manispaa imefanikiwa kutoa mikopo yenye thamani ya shilingi 3,966,405,785 kwa vikundi 914 yenye wanufaika 9281 na kati ya fedha hizo shilingi 1,031,003, 687.25 ndio zimerejeshwa.


Aidha Elizabeth kebwe amefafanua kuwa mikopo inayotolewa leo kuna  vikundi vitapata mkopo wa milioni 70 kikiwa ndicho kiwango cha juu kuwahi kutolewa na Manispaa kwa vikundi vya wajasiriamali  "haya ni mafanikio makubwa sana kwa Manispaa  na wajasiliamali kwani dhana ya mikopo hii ni kukukuza uchumi.

Pamoja na kutoa fedha kwa vikundi lakini pia Manispaa imefanikiwa kutoa bajaji 45, pikipiki 22 na toyo 1 vikundi vya vijana na walemavu "tunaimani vyombo hivi vya usafiri vitaanza kuwaingizia kipato,  nawasii muanze marejesho haraka zaidi" alisisitiza Kebwe.

Akiongea kwa niaba  ya wajasiriamali wenzake  stuwart  Simon banda kutoka kikundi cha  jiwezeshe  Goba ameishukuru serikali na Manispaa  ya ubungo kwa kutoa mikopo kwa wajasiriamali  ili kukuza mitaji ya biashara  zetu zitakazotusaidia kujikwamua kiuchumi.

Announcements

  • KIBALI CHA KUANZA KUTOZA USHURU WA KUSHUSHA NA KUPAKIA MIZIGO July 17, 2023
  • KUKANUSHA TAARIFA YA UWEPO WA HARAFU MBAYA STENDI YA MABASI MAGUFULI July 06, 2023
  • MATOKEO YA SENSA YA WATU NA MAKAZI 2022 Ubungo September 06, 2023
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI NAFASI YA DEREVA NA KATIBU MAHSUSI July 21, 2022
  • View All

Latest News

  • MIRADI 7 YENYE THAMANI YA BILIONI 8.2 UBUNGO YAPITA KWA KISHINDO MBIO ZA MWENGE WA UHURU 2025

    June 05, 2025
  • TUZINGATIE USAFI KUEPUKA MAGONJWA

    May 31, 2025
  • BODI YA AFYA UBUNGO YAPONGEZA WATAALAM WA AFYA NA KUTOA MAAGIZO YAKUBORESHA NYANJA MBALIMBALI

    May 29, 2025
  • MAAFISA HABARI HAKIKISHENI MNATANGAZA UTEKELEZAJI WA MIRADI KWA WANANCHI

    May 24, 2025
  • View All

Video

KIWANJA CHAKO KINA HATI? | UMEKUWA UKISUMBULIWA NA MIGOGORO YA ARDHI? | KARIBU KWENYE ARDHI CLINIC
More Videos

Quick Links

  • Leseni za biashara
  • Ushuru wa Hoteli
  • Kibali cha ujenzi
  • Sheria ndogondogo
  • Malengo na Dira
  • Muundo wa Uongozi
  • zabuni

Related Links

  • The National Examinations Council of Tanzania
  • TAMISEMI
  • Ministry of Education
  • President office State House
  • National Council for Technical Education
  • Ministry of Finace and Planning

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Contact Us

    Luguruni Area, Morogoro Road

    Postal Address: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam

    Telephone: +255 22 2926341

    Mobile:

    Email: md@ubungomc.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • Site Map

Copyright ©2017Ubungo Municipal Council All rights reserved.