• Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
Ubungo Municipal Council
Ubungo Municipal Council

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Ubungo Municipal Council

  • Home
  • About US
    • History
    • Mission and Vision
    • Core Values
  • Administration
    • Structure
    • Departments
      • Secondary Education
      • Agriculture, Livestock and Fisheries
      • Industry,Trade and Investments
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure, Rural and Urban Development
      • Pre-Primary and Primary Education
      • Human Resources Management and administration
      • Health, Social Welfare and Nutrition Services
      • Communit Development
    • Units
      • Legal Services
      • Internal Audit
      • ICT
      • Procument Management
      • Government Communication
      • Finance and Accounts
      • Sports, Culture and Arts
      • Waste Management and Sanitation
      • Natural Resources and Environment Conservation
    • Municipal By Laws
      • Municipal By Laws
      • Other Laws
  • Opportunities
    • Livestock
    • Agriculture
    • Markets
    • Bus Terminal
    • Industries
  • Services
    • Health
      • iCHF
      • Nutrition
      • Social welfare
    • Education
      • Pre and Primary Education
      • Secondary Education
    • Business
      • Service levy
      • Tax Registration
      • Business Licence
      • Hotel Levy
    • Enterpreneurship
      • Ten Percent Loans
    • Agriculture
    • Fishing
    • Livestock
      • UJUWA
  • Councilors
    • Councilors list
    • Council Committee
    • Council legal meeting
    • Meyor's schudule
  • Projects
    • Planned Projects
    • On going Projects
    • Completed projects
  • Publications
    • Guidelines
    • Application Forms
    • Reports
    • Acts
    • Bronchures
    • Tender Advert
    • Strategic Plan
    • Newsletter
  • Media Center
    • Photo Gallery
    • Video Gallery
    • Press Release
    • Speeches

MD UBUNGO AKUTANA NA WATENDAJI KUJADILI USAFI WA MAZINGIRA.

Posted on: November 28th, 2023

“Ninawaagiza watendaji wa Kata na Mitaa kuhakikisha wakandarasi au vikundi vya kuzoa taka vyote vilivyopo kwenye maeneo yenu vinalipwa malipo yao wakati” 

Kauli hiyo imetolewa  tarehe 28/12/2023 na Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Elias Ntiruhungwa katika kikao kilichojumuisha watendaji wa Kata na Mitaa, wenyeviti wa mitaa na wakandarasi au vikundi vya kuzoa taka mitaani kilichofanyika katika ukumbi wa Manispaa hiyo kilicholenga kujadili masuala mbalimbali ya usafi wa mazingira ndani ya Manispaa hiyo.

Ntiruhungwa ameendelea kueleza kuwa ucheleweshwaji  wa malipo ya fedha kwa wakandarasi hao umekuwa ukichochea kwa kiasi kikubwa maeneo mengi kuwa machafu kitendo ambacho kinaweza kupelekea kusababisha magonjwa ya mlipuko.

Aidha, Ntiruhungwa amewataka watendaji hao kuhakikisha sheria za uchafuzi wa mazingira zinasimamiwa vyema ikiwemo na utoaji wa elimu ya usafi wa mazingira kwa wananchi sambamba na kuwachukulia hatua wachafuzi wa mazingira na wanaokiuka kulipa ada ya usafi wa mazingira kwenye maeneo yao.

Sambamba na hayo Ntiruhungwa amewataka wakandarasi kuhakikisha taka zinaondolewa kwa wakati kwenye maeneo wanayoyafanyia kazi ili kuimarisha usafi kwenye maeneo hayo.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa kikundi kinachozoa taka Mtaa wa Mianzini Mariam Abdi ameeleza kuwa changamoto ya malipo yao yanatokana na mfumo mpya wa TAUSI ambao mara nyingi umekuwa ukisumbua hivyo ameiomba Serikali kuondoa changamoto za mfumo huo ili kuleta mazingira mazuri ya utendaji kwa wakandarasi hao na hivyo kuchochea hali ya usafi wa mazingira kwenye maeneo yetu.


Manispaa ya Ubungo inajumla ya Mitaa 90 na Kata 14 ambayo inawazabuni ambao wapewewa jukumu la kuzoa taka kwenye mitaa hiyo na kuzifikisha dampo kwa lengo la kuhakikisha maeneo yote yanakuwa safi muda wote.















Announcements

  • KIBALI CHA KUANZA KUTOZA USHURU WA KUSHUSHA NA KUPAKIA MIZIGO July 17, 2023
  • KUKANUSHA TAARIFA YA UWEPO WA HARAFU MBAYA STENDI YA MABASI MAGUFULI July 06, 2023
  • MATOKEO YA SENSA YA WATU NA MAKAZI 2022 Ubungo September 06, 2023
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI NAFASI YA DEREVA NA KATIBU MAHSUSI July 21, 2022
  • View All

Latest News

  • NI LAZIMA UJENZI WA UKUTA UANZE NA KUKAMILIKA" DC MSANDO

    May 12, 2025
  • CHALAMILA AZINDUA BIASHARA SAA 24 UBUNGO

    May 09, 2025
  • KATA YA UBUNGO YAKABIDHI MKOPO WA TSH. 122,800,000/= KWA VIKUNDI SITA VYA ASILIMIA 10

    May 02, 2025
  • KAMPENI YA KATAA UCHAFU, SAFISHA, PENDESHA UBUNGO YAZINDULIWA, MITAA SAFI NA MICHAFU KUPEWA ZAWADI

    May 03, 2025
  • View All

Video

KIWANJA CHAKO KINA HATI? | UMEKUWA UKISUMBULIWA NA MIGOGORO YA ARDHI? | KARIBU KWENYE ARDHI CLINIC
More Videos

Quick Links

  • Leseni za biashara
  • Ushuru wa Hoteli
  • Kibali cha ujenzi
  • Sheria ndogondogo
  • Malengo na Dira
  • Muundo wa Uongozi
  • zabuni

Related Links

  • The National Examinations Council of Tanzania
  • TAMISEMI
  • Ministry of Education
  • President office State House
  • National Council for Technical Education
  • Ministry of Finace and Planning

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Contact Us

    Luguruni Area, Morogoro Road

    Postal Address: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam

    Telephone: +255 22 2926341

    Mobile:

    Email: md@ubungomc.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • Site Map

Copyright ©2017Ubungo Municipal Council All rights reserved.