• Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
Ubungo Municipal Council
Ubungo Municipal Council

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Ubungo Municipal Council

  • Home
  • About US
    • History
    • Mission and Vision
    • Core Values
  • Administration
    • Structure
    • Departments
      • Secondary Education
      • Agriculture, Livestock and Fisheries
      • Industry,Trade and Investments
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure, Rural and Urban Development
      • Pre-Primary and Primary Education
      • Human Resources Management and administration
      • Health, Social Welfare and Nutrition Services
      • Communit Development
    • Units
      • Legal Services
      • Internal Audit
      • ICT
      • Procument Management
      • Government Communication
      • Finance and Accounts
      • Sports, Culture and Arts
      • Waste Management and Sanitation
      • Natural Resources and Environment Conservation
    • Municipal By Laws
      • Municipal By Laws
      • Other Laws
  • Opportunities
    • Livestock
    • Agriculture
    • Markets
    • Bus Terminal
    • Industries
  • Services
    • Health
      • iCHF
      • Nutrition
      • Social welfare
    • Education
      • Pre and Primary Education
      • Secondary Education
    • Business
      • Service levy
      • Tax Registration
      • Business Licence
      • Hotel Levy
    • Enterpreneurship
      • Ten Percent Loans
    • Agriculture
    • Fishing
    • Livestock
      • UJUWA
  • Councilors
    • Councilors list
    • Council Committee
    • Council legal meeting
    • Meyor's schudule
  • Projects
    • Planned Projects
    • On going Projects
    • Completed projects
  • Publications
    • Guidelines
    • Application Forms
    • Reports
    • Acts
    • Bronchures
    • Tender Advert
    • Strategic Plan
    • Newsletter
  • Media Center
    • Photo Gallery
    • Video Gallery
    • Press Release
    • Speeches

MIKOPO YA HALMASHAURI YACHOCHEA MAFANIKIO YA WAJASIRIAMALI

Posted on: September 30th, 2025

Mpango wa utoaji wa mikopo midogo ya asilimia 10 inayotokana na makusanyo ya mapato ya ndani kwa vikundi vya wajasiriamali katika Manispaa ya Ubungo umeendelea kuleta mafanikio makubwa ya kijamii na kiuchumi, kwa kuwawezesha wanufaika kuanzisha na kukuza biashara zao, kujiajiri, na kuongeza kipato.

Mikopo hiyo, iliyotolewa kati ya Januari na Machi 2025 imewezesha vikundi mbalimbali kuanzisha na kupanua biashara ndogo, jambo ambalo limewasaidia kujiajiri na kuboresha hali zao za maisha.

Mojawapo ya mafanikio hayo yanatokana na kikundi cha Ukurasa Mpya kilichopo Kata ya Makuburi, ambacho kinajihusisha na uzalishaji wa siagi ya karanga. Mwenyekiti wa kikundi hicho, Bi. Blandina Samuel Pima, amesema mkopo walioupata umeleta mabadiliko makubwa katika shughuli zao za kiuchumi.

"Hapo awali tulikuwa tukizalisha majumbani mwetu kwa vifaa duni. Sasa tumepata eneo rasmi la uzalishaji, tumenunua mashine za kisasa pamoja na malighafi muhimu. Kweli mkopo umetuwezesha kupiga hatua kubwa," alisema Bi. Pima akiwa katika ofisi yao mpya ya uzalishaji.

Kadhalika, kikundi cha NEH Women Group, kinachojishughulisha na usambazaji wa vyakula katika maeneo mbalimbali, kimenufaika kwa kiasi kikubwa na mkopo huo. Bi. Fatuma Issa Faru, Mhazini wa kikundi hicho, alieleza kuwa mkopo huo umeimarisha biashara yao kwa kiasi kikubwa.

"Tunaishukuru serikali kwa kutupatia mkopo huu ambao ni mkombozi mkubwa kwa biashara yetu. Tumejipanga kuhakikisha tunarejesha kwa wakati kama njia ya kuendeleza mpango huu kwa wengine," alibainisha.

Vikundi vingine vilivyonufaika na mpango huo ni pamoja na Car Body Work and Painting, Nyota Njema Group, na Genius Group, vyote kutoka Kata ya Sinza. Pia, kunavikundi vingine kutoka Kata za Kimara, Ubungo, na Saranga ambavyo vimepata manufaa kama hayo.

Afisa Maendeleo ya Jamii wa Kata ya Kimara, Bi. Ketra Mwakimi, ametoa wito kwa vikundi zaidi kujitokeza kuchukua mikopo hii kwa lengo la kujikwamua kiuchumi na kuchangia ajenda ya Serikali ya Awamu ya Sita ya kupunguza ukosefu wa ajira kwa wanawake, vijana na watu wenye ulemavu.

Announcements

  • KIBALI CHA KUANZA KUTOZA USHURU WA KUSHUSHA NA KUPAKIA MIZIGO July 17, 2023
  • KUKANUSHA TAARIFA YA UWEPO WA HARAFU MBAYA STENDI YA MABASI MAGUFULI July 06, 2023
  • MATOKEO YA SENSA YA WATU NA MAKAZI 2022 Ubungo September 06, 2023
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI NAFASI YA DEREVA NA KATIBU MAHSUSI July 21, 2022
  • View All

Latest News

  • MIKOPO YA HALMASHAURI YACHOCHEA MAFANIKIO YA WAJASIRIAMALI

    September 30, 2025
  • UBUNGO YAAHIDI KUJIPANGA IMARA ZAIDI KWA MSIMU UJAO WA SHIMISEMITA | YAPOTEZA MBELE YA DODOMA JIJI

    August 29, 2025
  • WANANCHI MSIGANI WAANZA KUNUFAIKA NA MAFUNZO YA KILIMO MJINI.

    August 29, 2025
  • MAAFISA UBUNGO WATOA CHANJO KWA NG"OMBE YA HOMA YA MAPAFU

    August 22, 2025
  • View All

Video

KIWANJA CHAKO KINA HATI? | UMEKUWA UKISUMBULIWA NA MIGOGORO YA ARDHI? | KARIBU KWENYE ARDHI CLINIC
More Videos

Quick Links

  • Leseni za biashara
  • Ushuru wa Hoteli
  • Kibali cha ujenzi
  • Sheria ndogondogo
  • Malengo na Dira
  • Muundo wa Uongozi
  • zabuni

Related Links

  • The National Examinations Council of Tanzania
  • TAMISEMI
  • Ministry of Education
  • President office State House
  • National Council for Technical Education
  • Ministry of Finace and Planning

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Contact Us

    Luguruni Area, Morogoro Road

    Postal Address: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam

    Telephone: +255 22 2926341

    Mobile:

    Email: md@ubungomc.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • Site Map

Copyright ©2017Ubungo Municipal Council All rights reserved.