• Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
Ubungo Municipal Council
Ubungo Municipal Council

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Ubungo Municipal Council

  • Home
  • About US
    • History
    • Mission and Vision
    • Core Values
  • Administration
    • Structure
    • Departments
      • Secondary Education
      • Agriculture, Livestock and Fisheries
      • Industry,Trade and Investments
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure, Rural and Urban Development
      • Pre-Primary and Primary Education
      • Human Resources Management and administration
      • Health, Social Welfare and Nutrition Services
      • Communit Development
    • Units
      • Legal Services
      • Internal Audit
      • ICT
      • Procument Management
      • Government Communication
      • Finance and Accounts
      • Sports, Culture and Arts
      • Waste Management and Sanitation
      • Natural Resources and Environment Conservation
    • Municipal By Laws
      • Municipal By Laws
      • Other Laws
  • Opportunities
    • Livestock
    • Agriculture
    • Markets
    • Bus Terminal
    • Industries
  • Services
    • Health
      • iCHF
      • Nutrition
      • Social welfare
    • Education
      • Pre and Primary Education
      • Secondary Education
    • Business
      • Service levy
      • Tax Registration
      • Business Licence
      • Hotel Levy
    • Enterpreneurship
      • Ten Percent Loans
    • Agriculture
    • Fishing
    • Livestock
      • UJUWA
  • Councilors
    • Councilors list
    • Council Committee
    • Council legal meeting
    • Meyor's schudule
  • Projects
    • Planned Projects
    • On going Projects
    • Completed projects
  • Publications
    • Guidelines
    • Application Forms
    • Reports
    • Acts
    • Bronchures
    • Tender Advert
    • Strategic Plan
    • Newsletter
  • Media Center
    • Photo Gallery
    • Video Gallery
    • Press Release
    • Speeches

TATHMINI YA ZIARA YA KATA KWA KATA YAFANYIKA KWA KIPEKEE | MIRADI 34 ILIYOKAGULIWA YATOLEWA TATHMINI YAKE | UWAJIBIKAJI WA WATUMISHI WA UMMA WASISITIZWA

Posted on: September 2nd, 2023

Katika ule utamaduni wake wa Uongozi wa pamoja "One Line Approach" wa mkuu wa wilaya ya Ubungo Mhe. Hashim Komba, leo Septemba 02, 2023 ameongoza kikao maalumu cha tathmini ya ziara yake ya kata kwa kata ambayo ilifanyika kuanzia Julai 11 mpaka Agosti 14, 2023 Katika kata zote 14 za Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo

Katika ziara hiyo jumla ya mikutano 14 ilifanyika, Miradi 34 ilikaguliwa na kero za wananchi 220 zilisikilizwa na kutatuliwa katika kata zote 14. Hivyo kikao cha leo kimekuja maalumu kwaajili ya kutathmini ziara hiyo na kupata mrejesho wa maelekezo yaliyotolewa kwenye miradi mbalimbali ya maendeleo na utatuzi wa kero za wananchi

Akiongea katika kikao hicho Mhe. Komba amemshukuru mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo, wakuu wa idara na watumishi wote kwa ushirikiano wao wa dhati walioutoa katika kipindi chote cha ziara hiyo. Aidha, DC Komba ametoa maelekezo kwa miradi yote ambayo haijakamilika, ikamilishwe haraka kutoka sasa ili kugatua huduma kwa wananchi

"Watumishi wenzangu ni muhimu kuzingatia maadili ya utumishi wetu ikiwa ni pamoja na kuwa wawajibikaji kwenye usimamizi wa miradi ya maendeleo. Na pia ninatoa onyo kwa watendaji wa mitaa ambao bado hawawajibiki kwenye majukumu yao ya kila siku, na onyo hili ni la mwisho kwenu" alisema Komba

Nae mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo Ndg, Elias Ntiruhungwa amempongeza DC Komba kwa ziara hiyo ambayo imesaidia kuongeza kasi ya ukamilishaji wa miradi na pia ameahidi kuendelea kusimamia miradi ya Manispaa kwa ukaribu zaidi ili malengo ya serikali ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan yatimie kwa vitendo

Akitoa shukrani kwa niaba ya baraza la madiwani Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ubungo Mhe. Jaffery Nyaigesha amempongeza mkuu wa wilaya kwa ziara hiyo na ametoa rai ya kuwepo kwa ziara hizo mara kwa mara ili kuongeza ari ya usimamiaji na ufuatiliaji wa miradi ya maendeleo

Mwisho, DC Komba ametoa vyeti vya pongezi kwa baadhi ya watumishi kwa ushiriki mzuri katika ziara hiyo kwa niaba ya watumishi wengine wa Wilaya na Manispaa ya Ubungo

pichani ni Afisa habari Manispaa ya Ubungo ndg. Mustapha Mwakibete akipokea cheti cha pongezi


















Announcements

  • KIBALI CHA KUANZA KUTOZA USHURU WA KUSHUSHA NA KUPAKIA MIZIGO July 17, 2023
  • KUKANUSHA TAARIFA YA UWEPO WA HARAFU MBAYA STENDI YA MABASI MAGUFULI July 06, 2023
  • MATOKEO YA SENSA YA WATU NA MAKAZI 2022 Ubungo September 06, 2023
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI NAFASI YA DEREVA NA KATIBU MAHSUSI July 21, 2022
  • View All

Latest News

  • MIAKA MINNE YA MAFANIKIO: UTELEKELEZA WA MIRADI YA MAENDELEO KATIKA HALMASHAURI YA MANISPAA YA UBUNGO CHINI YA UONGOZI WA RAIS SAMIA

    September 02, 2025
  • MIKOPO YA HALMASHAURI YACHOCHEA MAFANIKIO YA WAJASIRIAMALI

    September 30, 2025
  • UBUNGO YAAHIDI KUJIPANGA IMARA ZAIDI KWA MSIMU UJAO WA SHIMISEMITA | YAPOTEZA MBELE YA DODOMA JIJI

    August 29, 2025
  • WANANCHI MSIGANI WAANZA KUNUFAIKA NA MAFUNZO YA KILIMO MJINI.

    August 29, 2025
  • View All

Video

KIWANJA CHAKO KINA HATI? | UMEKUWA UKISUMBULIWA NA MIGOGORO YA ARDHI? | KARIBU KWENYE ARDHI CLINIC
More Videos

Quick Links

  • Leseni za biashara
  • Ushuru wa Hoteli
  • Kibali cha ujenzi
  • Sheria ndogondogo
  • Malengo na Dira
  • Muundo wa Uongozi
  • zabuni

Related Links

  • The National Examinations Council of Tanzania
  • TAMISEMI
  • Ministry of Education
  • President office State House
  • National Council for Technical Education
  • Ministry of Finace and Planning

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Contact Us

    Luguruni Area, Morogoro Road

    Postal Address: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam

    Telephone: +255 22 2926341

    Mobile:

    Email: md@ubungomc.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • Site Map

Copyright ©2017Ubungo Municipal Council All rights reserved.