• Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
Ubungo Municipal Council
Ubungo Municipal Council

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Ubungo Municipal Council

  • Home
  • About US
    • History
    • Mission and Vision
    • Core Values
  • Administration
    • Structure
    • Departments
      • Secondary Education
      • Agriculture, Livestock and Fisheries
      • Industry,Trade and Investments
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure, Rural and Urban Development
      • Pre-Primary and Primary Education
      • Human Resources Management and administration
      • Health, Social Welfare and Nutrition Services
      • Communit Development
    • Units
      • Legal Services
      • Internal Audit
      • ICT
      • Procument Management
      • Government Communication
      • Finance and Accounts
      • Sports, Culture and Arts
      • Waste Management and Sanitation
      • Natural Resources and Environment Conservation
    • Municipal By Laws
      • Municipal By Laws
      • Other Laws
  • Opportunities
    • Livestock
    • Agriculture
    • Markets
    • Bus Terminal
    • Industries
  • Services
    • Health
      • iCHF
      • Nutrition
      • Social welfare
    • Education
      • Pre and Primary Education
      • Secondary Education
    • Business
      • Service levy
      • Tax Registration
      • Business Licence
      • Hotel Levy
    • Enterpreneurship
      • Ten Percent Loans
    • Agriculture
    • Fishing
    • Livestock
      • UJUWA
  • Councilors
    • Councilors list
    • Council Committee
    • Council legal meeting
    • Meyor's schudule
  • Projects
    • Planned Projects
    • On going Projects
    • Completed projects
  • Publications
    • Guidelines
    • Application Forms
    • Reports
    • Acts
    • Bronchures
    • Tender Advert
    • Strategic Plan
    • Newsletter
  • Media Center
    • Photo Gallery
    • Video Gallery
    • Press Release
    • Speeches

UBORESHAJI WA HUDUMA ZA AFYA KWA WAZEE YAPENDEZESHA MAADHIMISHO YA SIKU YA WAZEE DUNIANI

Posted on: October 3rd, 2020


 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo imeadhimisha siku ya Wazee duniani iliyosindikizwa na kaulimbiu isemayo “familia na jamii ishiriki kuwatunza wazee” kwa kutoa huduma mbalimbali kwa wazee ikiwemo upimaji wa afya na matibabu pamoja na kutoa kadi za bima ya afya (iCHF) ikiwa ni moja ya mkakati wa serikali wa kuboresha huduma za afya kwa wazee.

Utoaji wa huduma hizo za afya umefanyika kwa muda wa siku mbili kuanzia tarehe 1 hadi 2 oktoba, 2020 na kilele kufanyika tarehe 3 oktoba, 2020  katika viwanja vya mnazimmoja jijini Dar es salaam ambapo wazee walipata fursa ya kupimwa magonjwa kama macho, kisukari, shinikizo la damu , moyo  pamoja na kinywa na meno pamoja na kupewa ushauri nasaa wa masuala mbalimbali.

Akizungumza kwa niaba ya wazee wenzake kwenye maadhimisho  hayo, Bibi Hafsa Ismail Yasile wa kata ya Makurumila Wilaya ya Ubungo, ameeleza kuwa siku ya wazee duniani  imekuwa nzuri sana kwakwe kwani amepata fursa ya kupata vipimo vya maradhi mbalimbali ikiwemo sukari ,  moyo, shinikizo la damu na amegundulika kuwa na ugonjwa wa shinikizo la damu ambapo ameshauriwa kuanza matibabu mapema.

Bibi Hafsa amesema faida ya kushiriki maadhimisho hayo amepata huduma za afya bure  jambo ambalo kwa wazee ni zuri ukizingatia wazee wengi hawana uwezo wa kifedha kugharamia matibabu yao  wakati wote “kwa kufika kwenye maadhimisho ya siku ya wazee nimebahatika kupata bima ya afya ( iCHF) ambayo itanisaidia kupata matibabu bure mwaka mzima kwenye kituo chochote cha kutolea huduma za afya”

Aidha, Bibi hafsa amewasii wazee wenzake kujenga utamaduni wa kushiriki kwenye shughuli mbalimbali zinazowahusu wao ili waweze kujua mambo mbalimbali kwa ustawi wa maisha yao “ siku nyingine wanapopata wito wowote  wawajibike kuitika badala kukaidi na kubaki kuilalamikia serikali kuwa haiwajali”

Kwa upande wake Mzee Abuu Juma Segamba kutoka kata ya Manzese Wilaya ya Ubungo ameipongeza  Serikali kwa kuweka utaratibu wa upimaji na utoaji wa huduma za afya bure kwa wazee na ameomba utaratibu huu uwe endelevu.

Mzee Segamba amefafanua kuwa, miaka ya nyuma wazee walikuwa wakiachwa nyuma ila kuanzia mwaka 2018 mpaka mwaka huu wazee wamekumbukwa kwa kupewa  kipaumbele kwenye mambo mbalimbali ikiwemo kwenye huduma za afya.

Mmoja wa wazee wakipata akifanyiwa uchunguzi  kwenye maadhimisho ya siku wazee duniani iliyoadhimishwa kimkoa katika viwanja vya Mnazi mmoja jijini Dar es Salaam leo tarehe 3 oktoba, 2020

Aidha Mzee Segamba ameeleza kuwa wazee hasa wanaume bado wameachwa nyuma kushirikishwa kwenye Nyanja ya utoaji maamuzi na utungaji wa sera ikiwemo kutokuwa na uwakilishi bungeni.

“Ukiangalia makundi kama ya wanawake, vijana na walemavu wamepewa kipaumbele katika bunge ambapo wanapata uwakilishi bungeni kupitia uwepo wa nafasi za viti maalumu lakini wazee hasa wanaume hatuna fursa hiyo, hivyo tunaiomba serikali itupatie fursa ya kupata uwakilishi vyombo vya maamuzi kuanzi kwenye mabaraza ya madiwani na bungeni kama yalivyo makundi ya wenzetu” ameomba  Mzee Segamba.

Aidha mwakilishi wa wazee jijini Dar es salaam ametumia siku hii ya wazee kutoa rai kwa serikali kuweka sheria itakayowafanya watoto kuwajibika kuwatunza wazee na wasipotekeleza wachukuliwe hatua za kisheria kama makosa mengine, kwa kufanya hivyo familia itakuwa imeshiriki kwa vitendo kuwatunza wazee kama kaulimbui ya maadhimisho haya  ya mwaka huu inavyosema “familia na jamii ishiriki kuwatunza wazee”

Tanzania inaungana na nchi nyingine za umoja wa mataifa kuadhimisha siku hii kwa mujibu wa Azimio la Umoja wa Mataifa Na. 49 ya Mwaka 1991 kila mwaka, lengo ikiwa kuhamasisha jamii kuweza kulinda na kutetea haki za wazee duniani kote pamoja na kutatua changamoto zinazowakabili na kuweka mipango ya kuzitatua ili waishi kwa heshima, hadhi na kuthaminiwa.

IMEANDALIWA NA;

Kitengo cha habari na uhususiano

Halmashauri ya manispaa ya ubungo

 

Announcements

  • KIBALI CHA KUANZA KUTOZA USHURU WA KUSHUSHA NA KUPAKIA MIZIGO July 17, 2023
  • KUKANUSHA TAARIFA YA UWEPO WA HARAFU MBAYA STENDI YA MABASI MAGUFULI July 06, 2023
  • MATOKEO YA SENSA YA WATU NA MAKAZI 2022 Ubungo September 06, 2023
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI NAFASI YA DEREVA NA KATIBU MAHSUSI July 21, 2022
  • View All

Latest News

  • MIRADI 7 YENYE THAMANI YA BILIONI 8.2 UBUNGO YAPITA KWA KISHINDO MBIO ZA MWENGE WA UHURU 2025

    June 05, 2025
  • TUZINGATIE USAFI KUEPUKA MAGONJWA

    May 31, 2025
  • BODI YA AFYA UBUNGO YAPONGEZA WATAALAM WA AFYA NA KUTOA MAAGIZO YAKUBORESHA NYANJA MBALIMBALI

    May 29, 2025
  • MAAFISA HABARI HAKIKISHENI MNATANGAZA UTEKELEZAJI WA MIRADI KWA WANANCHI

    May 24, 2025
  • View All

Video

KIWANJA CHAKO KINA HATI? | UMEKUWA UKISUMBULIWA NA MIGOGORO YA ARDHI? | KARIBU KWENYE ARDHI CLINIC
More Videos

Quick Links

  • Leseni za biashara
  • Ushuru wa Hoteli
  • Kibali cha ujenzi
  • Sheria ndogondogo
  • Malengo na Dira
  • Muundo wa Uongozi
  • zabuni

Related Links

  • The National Examinations Council of Tanzania
  • TAMISEMI
  • Ministry of Education
  • President office State House
  • National Council for Technical Education
  • Ministry of Finace and Planning

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Contact Us

    Luguruni Area, Morogoro Road

    Postal Address: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam

    Telephone: +255 22 2926341

    Mobile:

    Email: md@ubungomc.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • Site Map

Copyright ©2017Ubungo Municipal Council All rights reserved.