• Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
Ubungo Municipal Council
Ubungo Municipal Council

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Ubungo Municipal Council

  • Home
  • About US
    • History
    • Mission and Vision
    • Core Values
  • Administration
    • Structure
    • Departments
      • Secondary Education
      • Agriculture, Livestock and Fisheries
      • Industry,Trade and Investments
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure, Rural and Urban Development
      • Pre-Primary and Primary Education
      • Human Resources Management and administration
      • Health, Social Welfare and Nutrition Services
      • Communit Development
    • Units
      • Legal Services
      • Internal Audit
      • ICT
      • Procument Management
      • Government Communication
      • Finance and Accounts
      • Sports, Culture and Arts
      • Waste Management and Sanitation
      • Natural Resources and Environment Conservation
    • Municipal By Laws
      • Municipal By Laws
      • Other Laws
  • Opportunities
    • Livestock
    • Agriculture
    • Markets
    • Bus Terminal
    • Industries
  • Services
    • Health
      • iCHF
      • Nutrition
      • Social welfare
    • Education
      • Pre and Primary Education
      • Secondary Education
    • Business
      • Service levy
      • Tax Registration
      • Business Licence
      • Hotel Levy
    • Enterpreneurship
      • Ten Percent Loans
    • Agriculture
    • Fishing
    • Livestock
      • UJUWA
  • Councilors
    • Councilors list
    • Council Committee
    • Council legal meeting
    • Meyor's schudule
  • Projects
    • Planned Projects
    • On going Projects
    • Completed projects
  • Publications
    • Guidelines
    • Application Forms
    • Reports
    • Acts
    • Bronchures
    • Tender Advert
    • Strategic Plan
    • Newsletter
  • Media Center
    • Photo Gallery
    • Video Gallery
    • Press Release
    • Speeches

UBUNGO YATEKELEZA MPANGO WA MBOLEA YA RUZUKU.

Posted on: November 17th, 2023

Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo ni miongoni mwa Halmashauri zinazotekeleza mpango wa ruzuku ya mbolea kwa msimu wa 2022/2023 na 2023/2024 kupitia idara ya kilimo, mifugo na uvuvi.

 tarehe 17/11/2023 imefanya kikao cha kujadili taarifa ya tathimini ya utekelezaji wa mpango wa ruzuku ya mbolea kwa mwaka wa fedha 2022/2023 hadi 2023/2024 kilichojumuisha maafisa Kilimo wa Manispaa hiyo, Maafisa wa Mamlaka ya udhibiti wa mbolea Tanzania ‘TFRA’ na Maafisa kutoka Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa ‘TAKUKURU’ na wakulima mbalimbali.

Akiongea Mratibu wa Pembejeo Manispaa ya Ubungo Msafiri Barnabas amesema kwa mwaka wa fedha 2022/2023 Manispaa ya Ubungo imefanikiwa kusajili jumla ya wakulima 469 sawa na 20.52% kwenye mfumo wa ruzuku na wakulima 540 kwa mwaka wa fedha 2023/2024 sawa na 23.63% kati ya wakulima 2285 wa Manispaa hiyo.

Msafiri ameendelea kueleza kuwa Serikali imepanga kutoa ruzuku ya mbolea kwa wakulima kwa lengo la kupunguza gharama ya mbolea kwa wakulima ili kuongeza uzalishaji na tija katika kilimo, kuimarisha usalama wa chakula na kuongeza upatikanaji wa malighafi za viwanda vya ndani.

Sambamba na hayo Msafiri ameeleza kuwa mbolea zitakazohusika kwenye ruzuku ni mbolea za kupandia na kukuzia zikiwemo DAP, UREA, SA, CAN, NPKs, NITRABO na aina zingine kulingana na mahitaji ya soko.

Kwa upande wake Kaimu Meneja wa TFRA kanda ya Mashariki Ndg. Alla Mariki ametoa wito kwa wakulima kujisajili kwenye mfumo wa mbolea za ruzuku, ili kuiwezesha Serikali kupunguza mianya ya rushwa  na mfumo huo utatumia program maalum ya Kidijitali kusajili wakulima, wasambazaji/wazalishaji, mawakala pamoja na kuratibu usambazaji wa mbolea kwa wakulima na malipo ya mbolea ya ruzuku.

Aidha, Mariki amewataka wakulima kuacha kuuza mbolea za ruzuku kwani kufanya hivyo ni kinyume na taratibu za muongozo wa mbolea za ruzuku Nchini.

Nae Afisa wa TAKUKURU Wilaya ya Ubungo Ndg. Peter Mtema ameitaka Manispaa hiyo kuhakikisha elimu ya mbolea ya ruzuku inazidi kutolewa ili kuwezesha wakulima wengi kuweza kujisajili kwenye mfumo, Kutafuta wakala wa usambazaji wa mbolea ya ruzuku ndani ya Manispaa hiyo.













Announcements

  • KIBALI CHA KUANZA KUTOZA USHURU WA KUSHUSHA NA KUPAKIA MIZIGO July 17, 2023
  • KUKANUSHA TAARIFA YA UWEPO WA HARAFU MBAYA STENDI YA MABASI MAGUFULI July 06, 2023
  • MATOKEO YA SENSA YA WATU NA MAKAZI 2022 Ubungo September 06, 2023
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI NAFASI YA DEREVA NA KATIBU MAHSUSI July 21, 2022
  • View All

Latest News

  • NI LAZIMA UJENZI WA UKUTA UANZE NA KUKAMILIKA" DC MSANDO

    May 12, 2025
  • CHALAMILA AZINDUA BIASHARA SAA 24 UBUNGO

    May 09, 2025
  • KATA YA UBUNGO YAKABIDHI MKOPO WA TSH. 122,800,000/= KWA VIKUNDI SITA VYA ASILIMIA 10

    May 02, 2025
  • KAMPENI YA KATAA UCHAFU, SAFISHA, PENDESHA UBUNGO YAZINDULIWA, MITAA SAFI NA MICHAFU KUPEWA ZAWADI

    May 03, 2025
  • View All

Video

KIWANJA CHAKO KINA HATI? | UMEKUWA UKISUMBULIWA NA MIGOGORO YA ARDHI? | KARIBU KWENYE ARDHI CLINIC
More Videos

Quick Links

  • Leseni za biashara
  • Ushuru wa Hoteli
  • Kibali cha ujenzi
  • Sheria ndogondogo
  • Malengo na Dira
  • Muundo wa Uongozi
  • zabuni

Related Links

  • The National Examinations Council of Tanzania
  • TAMISEMI
  • Ministry of Education
  • President office State House
  • National Council for Technical Education
  • Ministry of Finace and Planning

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Contact Us

    Luguruni Area, Morogoro Road

    Postal Address: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam

    Telephone: +255 22 2926341

    Mobile:

    Email: md@ubungomc.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • Site Map

Copyright ©2017Ubungo Municipal Council All rights reserved.