• Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
Ubungo Municipal Council
Ubungo Municipal Council

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Ubungo Municipal Council

  • Home
  • About US
    • History
    • Mission and Vision
    • Core Values
  • Administration
    • Structure
    • Departments
      • Secondary Education
      • Agriculture, Livestock and Fisheries
      • Industry,Trade and Investments
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure, Rural and Urban Development
      • Pre-Primary and Primary Education
      • Human Resources Management and administration
      • Health, Social Welfare and Nutrition Services
      • Communit Development
    • Units
      • Legal Services
      • Internal Audit
      • ICT
      • Procument Management
      • Government Communication
      • Finance and Accounts
      • Sports, Culture and Arts
      • Waste Management and Sanitation
      • Natural Resources and Environment Conservation
    • Municipal By Laws
      • Municipal By Laws
      • Other Laws
  • Opportunities
    • Livestock
    • Agriculture
    • Markets
    • Bus Terminal
    • Industries
  • Services
    • Health
      • iCHF
      • Nutrition
      • Social welfare
    • Education
      • Pre and Primary Education
      • Secondary Education
    • Business
      • Service levy
      • Tax Registration
      • Business Licence
      • Hotel Levy
    • Enterpreneurship
      • Ten Percent Loans
    • Agriculture
    • Fishing
    • Livestock
      • UJUWA
  • Councilors
    • Councilors list
    • Council Committee
    • Council legal meeting
    • Meyor's schudule
  • Projects
    • Planned Projects
    • On going Projects
    • Completed projects
  • Publications
    • Guidelines
    • Application Forms
    • Reports
    • Acts
    • Bronchures
    • Tender Advert
    • Strategic Plan
    • Newsletter
  • Media Center
    • Photo Gallery
    • Video Gallery
    • Press Release
    • Speeches

VIONGOZI UBUNGO WAJENGEWA UELEWA KUHUSU MFUMOWA ANWANI ZA MAKAZI

Posted on: February 22nd, 2022

 

Viongozi wa Wilaya ya Ubungo wakiwemo Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama, Madiwani na Wataalam wa Manispaa ya Ubungo wamejengewa uwezo kuhusu mfumo wa anwani za makazi  lengo ikiwa ni kuwa na uelewa wa pamoja katika kulitekeleza zoezi hilo muhimu.

Akiongea wakati wa kufungua mafunzo hayo yaliyotolewa leo Februari 22, 2022 kwa viongozi hao, Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mheshimiwa Kheri James ameeleza kuwa mafunzo hayo ni mwendelezo wa utoaji wa elimu kuhusu zoezi hilo kwa viongozi wa ngazi mbalimbali ambao ndio wasimamizi wakuu wa zoezi.

Tumeitana hapa ikiwa ni utekelezaji wa azima ya Serikali ya kujengeana uwezo kama viongozi tunaowajibika kusimamia zoezi la mfumo wa  anwani za makazi ili kila mtu ajue wajibu wake katika zoezi hili ambalo litatekelezwa kwa muda mfupi yaani kama “operational” tunatamani zoezi hili lifanyike kwa ufanisi na kwa haraka ikiwezekana tuwe wa kwanza kumaliza.

Aidha, Mhe James amewaeleza Madiwani kwa nafasi zao wanawajibu mkubwa sana katika kuhamasisha wananchi kushiriki katika zoezi hilo kwa kutoa ushirikiano  wa kutoa taarifa zinazohitajika wakati wa wakusanya taarifa hizo wakifika kwenye nyumba zao kwa ajili ya kuwekwa kwenye mfumo. 

“Tambueni kuwa kufanikisha zoezi hili la mfumo wa anwani ni kufanikisha zoezi la Sensa linalotarajia kufanyika mwaka huu ambapo mazoezi hayo yote yanatekelezwa kwa mujibu wa sheria” alisisitiza Mhe. James”

Akiongea wakati wa kutoa mafunzo hayo, Mratibu wa zoezi hilo JOHN ILOMO alieleza kuwa katika uundaji wa anwani za makazi unahusisha nambari za nyumba, postkodi na  majina ya barabara na kusistiza kuwa utoaji wa majina hayo uzingatie historia ya eneo pamoja na matamshi yanayokubalika na mtaa husika, huku majina yenye itikadi za kidini, kikabila na kisiasa yakikatazwa kabisa kutumika.

Ilomo amesema kuwa utoaji wa  anwani za makazi kwa maeneo yasiyopangika namba zitatolewa bila kufuata mtiririko tofauti na zile zilizopangika ambapo utoaji wa anwani wake utazingatia utaratibu wa namba shufwa kwa upande kulia na namba witiri kwa upande wa kushoto wa barabara.

Pia ameendelea kuwaeleza viongozi hao kuwa maeneo hatarishi au yasiyorasmi kama hifadhi ya barabara, mkondo wa maji au chini ya nguzo ya umeme sheria imekataza kutoa anwani za makazi hivyo taarifa zao hazitaingizwa kwenye mfumo huu.

Kwa upande wao Madiwani wameipongeza serikali kwa kuandaa mafunzo hayo ambayo yamewapa fursa ya kujua nini cha kuwaeleza wananchi namna ya kushiriki kwenye zoezi hilo muhimu la kitaifa ili likamilke kwa wakati na hatimaye malengo ya serilaki yatimie ikiwemo la kuongeza wigo wa ajira kwa njia ya mtandao, kuwezesha ukusanyaji wa mapato, kusaidia zoezi la sensa kwa wepesi na kupanga vizuri mipango ya maendeleo halisi inayotekelezeka Nchi nzima.

Announcements

  • KIBALI CHA KUANZA KUTOZA USHURU WA KUSHUSHA NA KUPAKIA MIZIGO July 17, 2023
  • KUKANUSHA TAARIFA YA UWEPO WA HARAFU MBAYA STENDI YA MABASI MAGUFULI July 06, 2023
  • MATOKEO YA SENSA YA WATU NA MAKAZI 2022 Ubungo September 06, 2023
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI NAFASI YA DEREVA NA KATIBU MAHSUSI July 21, 2022
  • View All

Latest News

  • NI LAZIMA UJENZI WA UKUTA UANZE NA KUKAMILIKA" DC MSANDO

    May 12, 2025
  • CHALAMILA AZINDUA BIASHARA SAA 24 UBUNGO

    May 09, 2025
  • KATA YA UBUNGO YAKABIDHI MKOPO WA TSH. 122,800,000/= KWA VIKUNDI SITA VYA ASILIMIA 10

    May 02, 2025
  • KAMPENI YA KATAA UCHAFU, SAFISHA, PENDESHA UBUNGO YAZINDULIWA, MITAA SAFI NA MICHAFU KUPEWA ZAWADI

    May 03, 2025
  • View All

Video

KIWANJA CHAKO KINA HATI? | UMEKUWA UKISUMBULIWA NA MIGOGORO YA ARDHI? | KARIBU KWENYE ARDHI CLINIC
More Videos

Quick Links

  • Leseni za biashara
  • Ushuru wa Hoteli
  • Kibali cha ujenzi
  • Sheria ndogondogo
  • Malengo na Dira
  • Muundo wa Uongozi
  • zabuni

Related Links

  • The National Examinations Council of Tanzania
  • TAMISEMI
  • Ministry of Education
  • President office State House
  • National Council for Technical Education
  • Ministry of Finace and Planning

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Contact Us

    Luguruni Area, Morogoro Road

    Postal Address: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam

    Telephone: +255 22 2926341

    Mobile:

    Email: md@ubungomc.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • Site Map

Copyright ©2017Ubungo Municipal Council All rights reserved.