• Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
Ubungo Municipal Council
Ubungo Municipal Council

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Ubungo Municipal Council

  • Home
  • About US
    • History
    • Mission and Vision
    • Core Values
  • Administration
    • Structure
    • Departments
      • Secondary Education
      • Agriculture, Livestock and Fisheries
      • Industry,Trade and Investments
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure, Rural and Urban Development
      • Pre-Primary and Primary Education
      • Human Resources Management and administration
      • Health, Social Welfare and Nutrition Services
      • Communit Development
    • Units
      • Legal Services
      • Internal Audit
      • ICT
      • Procument Management
      • Government Communication
      • Finance and Accounts
      • Sports, Culture and Arts
      • Waste Management and Sanitation
      • Natural Resources and Environment Conservation
    • Municipal By Laws
      • Municipal By Laws
      • Other Laws
  • Opportunities
    • Livestock
    • Agriculture
    • Markets
    • Bus Terminal
    • Industries
  • Services
    • Health
      • iCHF
      • Nutrition
      • Social welfare
    • Education
      • Pre and Primary Education
      • Secondary Education
    • Business
      • Service levy
      • Tax Registration
      • Business Licence
      • Hotel Levy
    • Enterpreneurship
      • Ten Percent Loans
    • Agriculture
    • Fishing
    • Livestock
      • UJUWA
  • Councilors
    • Councilors list
    • Council Committee
    • Council legal meeting
    • Meyor's schudule
  • Projects
    • Planned Projects
    • On going Projects
    • Completed projects
  • Publications
    • Guidelines
    • Application Forms
    • Reports
    • Acts
    • Bronchures
    • Tender Advert
    • Strategic Plan
    • Newsletter
  • Media Center
    • Photo Gallery
    • Video Gallery
    • Press Release
    • Speeches

WAJAWAZITO KITUO CHA AFYA MBEZI, WAPATIWA ELIMU YA UPUNGUFU WA DAMU.

Posted on: December 12th, 2023

Manispaa ya Ubungo kupitia Kitengo cha Lishe  tarehe 12/12/2023 imetoa elimu ya kukabiliana na changamoto ya upungufu wa damu kwa wajawazito ndani ya Kituo cha afya cha Mbezi lengo ikiwa ni kuwawezesha kuepukana na madhara yanayosababishwa na upungufu wa damu kwa wajawazito.

Akielezea madhara ya upungufu wa damu  Afisa Lishe wa Manispaa hiyo Onesmo Mwaisyungu ameeleza kuwa upungufu wa damu kwa wajawazito unapelekea kuzaa watoto wenye uzito pungufu, upungufu wa maumbile yaani kuwa na kichwa kikubwa, mdomo sungura, mgongo wazi na kupelekea vifo kwa watoto hao lakini pia wajawazito hao hupoteza damu nyingi wakati wa kujifungua.

Onesmo ameendelea kueleza kuwa, kutokana na madhara hayo Manispaa imeamua kuandaa programu ya kutembelea vituo vya kutolea huduma za afya na kufundisha wajawazito namna bora ya kutengeneza juisi za kuongeza damu ikiwemo juice ya beetroot, rozela na tembele.


Aidha, Onesmo ameeleza kuwa beetroot ina faida zaidi ya 19 ikiwemo madini chuma, inawezesha kutozeeka mapema, inaimarisha ngozi na inapunguza presha ya kupanda na ameeleza kuwa juisi hiyo inashauliwa kunywa glasi mbili tu kwa siku na kwa matokeo mazuri zinapaswa kunywa asubuhi kabla ya kula kitu chochote huku akisisitiza kwa wenye changamoto ya figo hawaruhusiwi kunywa juisi hiyo.


Sambamba na hayo Onesmo ameeleza kuwa wakati wa kutengeneza juisi hizo ni vizuri kuchanganya na pasheni au chungwa au limao au apple au zabibu lakini pia kuongeza na karoti kwenye juisi ya beetroot na zisizidi siku mbili tangu siku ya kutengenezwa na kuhifadhiwa kwenye friji kwa ajili ya matumizi.


Nae Afisa lishe Zulfa Mshitiri akielezea dalili za upungufu wa damu kwa wajawazito hao amesema ni uchovu uliopitiliza, kuishiwa nguvu, kuishiwa pumzi, kupauka ngozi, matatizo ya nywele na kucha na kuvimba miguu, mikono na uso.

Zulfa amewataka wajawazito hao kuwahi kituo cha kutolea huduma za afya mara waonapo dalili hizo huku akiwasisitiza kuhudhuria kliniki ya mama wajawazito, kula vyakula vyenye wingi wa madini chuma na vitamini C lakini pia kunywa dawa za virutubishi ili kuwawezesha kuepukana na madhara ya upungufu wa damu.












Announcements

  • KIBALI CHA KUANZA KUTOZA USHURU WA KUSHUSHA NA KUPAKIA MIZIGO July 17, 2023
  • KUKANUSHA TAARIFA YA UWEPO WA HARAFU MBAYA STENDI YA MABASI MAGUFULI July 06, 2023
  • MATOKEO YA SENSA YA WATU NA MAKAZI 2022 Ubungo September 06, 2023
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI NAFASI YA DEREVA NA KATIBU MAHSUSI July 21, 2022
  • View All

Latest News

  • NI LAZIMA UJENZI WA UKUTA UANZE NA KUKAMILIKA" DC MSANDO

    May 12, 2025
  • CHALAMILA AZINDUA BIASHARA SAA 24 UBUNGO

    May 09, 2025
  • KATA YA UBUNGO YAKABIDHI MKOPO WA TSH. 122,800,000/= KWA VIKUNDI SITA VYA ASILIMIA 10

    May 02, 2025
  • KAMPENI YA KATAA UCHAFU, SAFISHA, PENDESHA UBUNGO YAZINDULIWA, MITAA SAFI NA MICHAFU KUPEWA ZAWADI

    May 03, 2025
  • View All

Video

KIWANJA CHAKO KINA HATI? | UMEKUWA UKISUMBULIWA NA MIGOGORO YA ARDHI? | KARIBU KWENYE ARDHI CLINIC
More Videos

Quick Links

  • Leseni za biashara
  • Ushuru wa Hoteli
  • Kibali cha ujenzi
  • Sheria ndogondogo
  • Malengo na Dira
  • Muundo wa Uongozi
  • zabuni

Related Links

  • The National Examinations Council of Tanzania
  • TAMISEMI
  • Ministry of Education
  • President office State House
  • National Council for Technical Education
  • Ministry of Finace and Planning

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Contact Us

    Luguruni Area, Morogoro Road

    Postal Address: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam

    Telephone: +255 22 2926341

    Mobile:

    Email: md@ubungomc.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • Site Map

Copyright ©2017Ubungo Municipal Council All rights reserved.