• Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
Ubungo Municipal Council
Ubungo Municipal Council

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Ubungo Municipal Council

  • Home
  • About US
    • History
    • Mission and Vision
    • Core Values
  • Administration
    • Structure
    • Departments
      • Secondary Education
      • Agriculture, Livestock and Fisheries
      • Industry,Trade and Investments
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure, Rural and Urban Development
      • Pre-Primary and Primary Education
      • Human Resources Management and administration
      • Health, Social Welfare and Nutrition Services
      • Communit Development
    • Units
      • Legal Services
      • Internal Audit
      • ICT
      • Procument Management
      • Government Communication
      • Finance and Accounts
      • Sports, Culture and Arts
      • Waste Management and Sanitation
      • Natural Resources and Environment Conservation
    • Municipal By Laws
      • Municipal By Laws
      • Other Laws
  • Opportunities
    • Livestock
    • Agriculture
    • Markets
    • Bus Terminal
    • Industries
  • Services
    • Health
      • iCHF
      • Nutrition
      • Social welfare
    • Education
      • Pre and Primary Education
      • Secondary Education
    • Business
      • Service levy
      • Tax Registration
      • Business Licence
      • Hotel Levy
    • Enterpreneurship
      • Ten Percent Loans
    • Agriculture
    • Fishing
    • Livestock
      • UJUWA
  • Councilors
    • Councilors list
    • Council Committee
    • Council legal meeting
    • Meyor's schudule
  • Projects
    • Planned Projects
    • On going Projects
    • Completed projects
  • Publications
    • Guidelines
    • Application Forms
    • Reports
    • Acts
    • Bronchures
    • Tender Advert
    • Strategic Plan
    • Newsletter
  • Media Center
    • Photo Gallery
    • Video Gallery
    • Press Release
    • Speeches

WATOA HUDUMA ZA AFYA NGAZI YA JAMII 30 WAJENGEWA UWEZO

Posted on: July 14th, 2025

Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo kupitia Idara ya Afya, Ustawi wa jamii na Lishe imewajengea uwezo watoa huduma ngazi ya jamii wapya 30 ili kufanikisha azma ya Mpango Jumuishi wa wahudumu hao kuendeleza afua jumuishi za Afya, Lishe na Ustawi wa Jamii.

Hayo yamebainishwa na Mratibu wa huduma ngazi ya jamii Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo Bi. Shubira Bachuba  ambapo amewataka kuendelea na majukumu yao ya msingi ikiwa ni pamoja na kuhamasisha wananchi kujitokeza katika vituo vya kutolewa hiduma za afya kwa wakati.

"Watoa huduma ngazi ya jamii ni wahamasishaji katika ngazi ya jamii, kwahiyo wanapokutana na changamoto wao kazi yao ni kutoa rufaa kama hilo eneo hawezi kulifanyia kazi, Wasitoe huduma kama Madaktari au wauguzi" -Amesema Bi. Bachuba

Akizungumza wakati wa mafunzo hayo, Afisa Lishe wa Manispaa ya Ubungo Bi. Beatrice Mossile amesema kuwa lishe bora inaanzia kipindi mama anapokuwa mjamzito na mtoto anapofikisha miezi 6 - 24 ili kupunguza utapiamlo kwa watoto.

Bi. Mossile amesema kuwa, lishe bora inaanzia kipindi mama anapokua mjamzito kwasababu mtoto anaanza kupata chakula kupitia milo anayokula mama yake hivyo ni vyema kuzingata ulaji sahihi ili kumjenga mtoto tangu akiwa tumboni.

Akiongelea kuhusu elimu ya lishe na upungufu wa damu kwa Kina mama wajawazito Afisa lishe amesema kuwa vyakula vyenye asili ya mimea na wanyama ni muhimu kuvizingatia ikiwemo pia matumizi sahihi ya dawa za kuongeza damu wanazopewa kliniki ili kumuwezesha kujifungua mtoto mwenye afya bora.

Aidha amewasisitiza watoa huduma za afya ngazi ya jamii kuielimisha jamii juu ya umuhimu wa maziwa ya mama pekee kwa kipindi cha miezi sita kwani yanajitosheleza na yanavirutubisho vyote  anavyopaswa kuvipata mtoto.

Aidha amewaeleza watoa huduma kuelimisha jamii kuwa maziwa ya mama asilimia70 ni majimaji hivyo ile dhana ya maziwa mepesi na kuona watoto hawashibi waiondoe kwani kumuanzishia chakula mbadala katika kipindi cha miezi 6 kunaathari kubwa kwa mtoto.

"Maziwa ya Mama ni Kinga tiba, sio gharama na yanajitosheleza. Chakula mbadala kwa mtoto chini ya miezi 6 kunaweza kupelekea  kupata magonjwa sugu kama kisukari na presha"

Announcements

  • KIBALI CHA KUANZA KUTOZA USHURU WA KUSHUSHA NA KUPAKIA MIZIGO July 17, 2023
  • KUKANUSHA TAARIFA YA UWEPO WA HARAFU MBAYA STENDI YA MABASI MAGUFULI July 06, 2023
  • MATOKEO YA SENSA YA WATU NA MAKAZI 2022 Ubungo September 06, 2023
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI NAFASI YA DEREVA NA KATIBU MAHSUSI July 21, 2022
  • View All

Latest News

  • WATOA HUDUMA ZA AFYA NGAZI YA JAMII 30 WAJENGEWA UWEZO

    July 14, 2025
  • MAKABURI 29 YA UFI UBUNGO KISIWANI YAHAMISHWA KUPISHA UPANUZI WA BARABARA.

    July 10, 2025
  • UBUNGO TAYARI TUPO KATIKA MAONESHO YA 49 YA KITAIFA YA BIASHARA 7'7, MNAKARIBISHWA

    June 30, 2025
  • SERIKALI YAZINDUA MADAWATI YA HUDUMA ZA USTAWI WA JAMII KATIKA VITUO VYA USAFIRISHAJI.

    June 30, 2025
  • View All

Video

KIWANJA CHAKO KINA HATI? | UMEKUWA UKISUMBULIWA NA MIGOGORO YA ARDHI? | KARIBU KWENYE ARDHI CLINIC
More Videos

Quick Links

  • Leseni za biashara
  • Ushuru wa Hoteli
  • Kibali cha ujenzi
  • Sheria ndogondogo
  • Malengo na Dira
  • Muundo wa Uongozi
  • zabuni

Related Links

  • The National Examinations Council of Tanzania
  • TAMISEMI
  • Ministry of Education
  • President office State House
  • National Council for Technical Education
  • Ministry of Finace and Planning

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Contact Us

    Luguruni Area, Morogoro Road

    Postal Address: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam

    Telephone: +255 22 2926341

    Mobile:

    Email: md@ubungomc.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • Site Map

Copyright ©2017Ubungo Municipal Council All rights reserved.