Mkurugenzi msaidizi wa Idara ya Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe TAMISEMI Dkt. Paul Chawote ameipongeza Manispaa ya Ubungo kwa ujenzi wenye viwango wa hospitali ya Wilaya na kuwasisitiza kumaliza mradi huo Kwa wakati
Dkt. Chawote ametoa pongezi hizo wakati alipotembelea na kukagua ujenzi wa hospitali hiyo inayojengwa kata ya kimara mtaa wa baruti leo januari 9, 2020 na kueleza kuwa ziara hiyo inalenga kuona utekelezaji wa shughuli mbalimbali za afya ikiwemo ujenzi miundombinu.
"Kwa mujibu wa taarifa, mradi huu ulipaswa kukamilika mwezi desemba 2020, tumieni vizuri muda wa nyongeza mliopewa kukamilisha mradi ili wananchi waanze kupata huduma kwani hilo ndilo lengo la serikali" amesisitiza Dkt Chawote
Pamoja na kujenga kwa ubora stahiki kwa maana ya thamani ya fedha lakini pia zingatieni marekebisho niliyowaelekeza Kwani ni ya msingi Kwa majengo ya Hospitali ameagiza Dkt Chawote.
Mkurugenzi msaidizi idara ya afya, ustawi wa jamii na lishe Dkt Paul Chawote (aliyenyoosha mkono) akitoa maelekezo kwa uongozi wa Manispaa ya Ubungo na mjenzi wa mradi wa hospitali leo januari 5,2021 alipotembelea mradi huo.
Nae Mkurugenzi wa Manispaa Ubungo Beatrice Dominic ameahidi kuongeza kasi ili mradi ukamilike kwa wakati na uanze kutumika
"Mradi umechelewa kidogo kutokana na changamoto ya upatikanaji wa vifaa vya Ujenzi hususani Mabati na sementi lakini kwa sasa changamoto hizo zimetatuliwa " ameeleza Beatrice
Beatrice ameendelea kueleza kuwa , Utekelezaji wa Mradi Kwa sasa upo asilimia 60 Ila tunategemea asilimia ya kutekelezaji itaongezeka kwani kasi ya ujenzi ni kubwa kwa sasa.
Mradi ulikadiriwa kutumia shilingi bilioni 1.82 kwa awamu ya kwanza ambapo jumla shilingi bilioni 1.5 ni fedha kutoka serikali kuu na shilingi 250 milioni ni mchango wa halmashauri katika mradi huo.
Kibamba Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa