I. SERVICE LEVY
Kodi hii ni matokeo ya Sheria ya fedha namba 9 ya 1982 kifungu cha 6 (1)(U).
Kodi hii hulipwa na makampuni, taasisi na biashara mbalimbali zilizosajiliwaVAT. Kutokana na mauzo ghafi kwa kiwango kisichozidi asilimia 0.3.
Kwa kawaida kodi hii hukusanywa mara nne kwa mwaka kila baada ya miezimitatu na utaratibu wa malipo ni kama ifuatavyo:-
· Mlipakodi Atatakiwa awasilishe hesabu ya mauzo yake katika Ofisi zaHalmashauri, ambapo atawakabidhi wataalamu wa kutoza kodi hiyo ambao baada yakuzidisha na hiyo asilimia 0.3 atalipa kiasi kinachopatikana.
Mfano mfanyabiashara ameuza kiasi cha Shs. Milioni moja kwa miezi mitatu,i.e. 1,000,000/= itazidishwa na asilimia 0.3 ambazo ni:- 1,000,000 x 0.3 kiasikinachopatikana yaani Shs. 3,000/= ndizo anazopaswa kulipa, na katika ulipaji,mlipa kodi anajaza fomu maalumu ambazo zinapatikana katika Ofisi za Halmashaurina kuambatanisha na mauzo yake na baada ya kufanya malipo anapewa risiti ambayoanapaswa kuiweka tika kumbukumbu zake kwa ajili ya ukaguzi n.k.
Aina ya Makosa yatakayosababisha kutozwa faini/adhabu:-
· Mtu yoyote anayetakiwa kulipa kodi akishindwa kuwasilisha hesabu zakekama inavyotakiwa kwa mujibu wa Sheria ndogo na inapobainika kuwa amefanyamakundi.
· Kodi ambayo haijalipwa kwa wakati kama ilivyoelezwa kwenye Sheriandogo itatozwa na riba ya faini ya asilimia kumi na tano (15%) kwa mwezina zitatakiwa kulipwa pamoja na kodi inayodaiwa.
· Mtu yoyote ambaye bila sababu za msingi atashindwa:-
(a) kuwasilisha nyaraka, maelezo au taarifa inayotakiwa kuwasilishwakwa Halmashauri katika muda uliowekwa.
(b) Kutunza kumbukumbu, kitabu au hesabu.
(c) Kuonyesha kumbukumbu yoyote au nyaraka kwa ajili ya uchunguzi.
Mtu yeyote bila sababu za msingi:-
(a) Akifanya hesabu za uongo kwa kupunguza au kutoa hesabu zisizokuwasahihi.
(b) Akitoa taarifa isiyokuwa sahihi kuhusu jambo lolote linalowezakuathiri jukumu lake au la mtu mwingine la kulipa kodi.
(c) Akiandaa au kutengenezewa vitabu vya uongo vya Mahesabu aukumbukumbu.
(d) Atamzuia au atajaribu kumzuia Afisa Muidhiniwa kutekeleza majukumuyake aliyopewa kwa mujibu wa Sheria ndogo atakuwa anatenda kosa.
Mtu yeyote atakayevunja masharti ya Sheria ndogo hizi atakuwa anatenda kosana atawajibika kulipa faini isiyozidi shilingi elfu hamsini (50,000/=) au kifungocha miezi isiyozidi (12) kumi na mbili jela au adhabu zote mbili kwa pamoja.
NB: Pamoja na adhabu atakayotozwa mkosaji kwenye kif.Na. 17 (1). Pia atawajibika kulipa gharama nyingine za Halmashauri.
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa