KANUNI ZA MAADILI YA MSINGI MANISPAA YA UBUNGO
Utekelezaji wa Mpango Mkakati wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo unaongozwa na maadili ya msingi ambayo hujumuisha kile ambacho Halmashauri inakithamini zaidi kama vile wafanyakazi wote wanapaswa kuzingatia utekelezaji Maadili ya msingi ambayo yanayoongoza mpango mkakati.
MAADILI YA MSINGI:
I. Uwazi: Halmashauri inafanya kazi ili kuhakikisha kuwa kuna upatikanaji wa taarifa kwa Umma ya namna inavyofanya kazi zake za kila siku, Halmashauri inakusudia kuitumikia jamii kwa uwezo wake kwa kuzingatia uwazi.
II. Uaminifu na Maadili: Halmashauri itahakikisha wafanyakazi wanafanya kazi kwa usahihi, kwa njia ya uaminifu, haki, na uwajibikaji ili kujenga mahusiano ya kweli na yenye nguvu miongoni mwa wafanyakazi, wadau, na wateja kwa sifa ya kuaminika katika Halmashauri, pia kwa manufaa na maslahi ya kila mtu.
III. Uvumbuzi: Halmshauri inalenga kuwa mstari wa mbele miongoni mwa Halmashauri zingine katika utoaji wa huduma za kijamii. Wafanyakazi wanahimizwa kubadilika kutikokana na mazingira kuja na mawazo ya ubunifu ili kukabiliana na changamoto za kijamii na kuimarisha fursa zilizopo za utoaji wa huduma bora kwa kijamii na ufanisi katika Halmshauri.
IV.Uwajibikaji: Halmashuri inalenga kuzingatia viwango vya utaalamu mahali pa kazi, Uwajibikaji ni kipengele muhimu cha utendaji kazi katika Halmashauri. Wafanyakazi wanakumbushwa kuwa wameajiliwa kwa kigezo cha taaluma walizosomea wanatakiwa kuwajibika katika halmashauri kwa kutoa huduma bora za kijamii na kiuchumi kwa ufanisi kwa kutumia rasilimali zilizopo kwa ajili ya maendeleo endelevu.
V. Mtazamo wa jamii: Halmashauri inajidhatiti kukidhi mahitaji muhimu ya jamii. hii linafanyika kwa kutoa kipaumbele katika kubainsha mahitaji yao na hivyo kutoa huduma kulingana na mahitaji katika ngazi zote na kwa kiwango.
VI. Matokeo chanya: Halmashauri inajitahidi kuzalisha matokeo chanya yanayokubalika katika jamii il kuweza kuleta mabadiliko ya mazuri ya kimaendeleo.
VII. Ushirikiano: Halmashauri inahimiza kufanya kazi kwa kushirikiana na washirika mbalimbali wa maendeleo kutoka sekta binafsi na za umma katika utoaji wa huduma za jamii kwa ufanisi.
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa