Kufuatia upungufu wa madarasa na madawati katika shule ya Msingi Kingo'ngo iliyopo kata ya Saranga Manispaa ya Ubungo unaopelekea wanafunzi wengi kukaa chini, Manispaa itaanza mara moja ujenzi wa vyumba 8 vya madarasa na kutengeneza madawati 300 kwa gharama ya shilingi milioni 160 ikiwa ni hatua ya kutatua changamoto hiyo.
Shule hiyo yenye wanafunzi 2505, kwa sasa ina madarasa 10 Kati ya hayo madarasa 3 ni mabovu ambapo kutokana na uchache huo wanafunzi wengi wanakaa chini na wengine wanasomea nje.
Manispaa imefikia uamuzi wa kujenga miundombinu hiyo ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Mhe. Rais Dkt John Pombe Magufuli alilolitoa leo Januari 18, 2021 akiwa Mjini bukoba la kutaka madarasa yajengwe na kutengeneza madawati kwa haraka ili wanafunzi wasikae chini wala kusomea nje
Mhe Rais ametoa agizo hilo kufuatia taarifa iliyotolewa na mwananchi na kusambazwa kwenye mitandao wa kijamii ikionesha wanafunzi wengi wakisoma darasa moja wakiwa wamekaa chini na uwepo wa baadhi ya madarasa mabovu.
Akiongea na wananchi wa king'ongo Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe. Kisare Makori amewahakikishia wananchi hao kuwa ujenzi wa madarasa hayo utaanza mara moja ili kuhakikisha tatizo la wanafunzi kukaa chini linatatuliwa kwa kiasi kikubwa.
Kibamba Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa