Shirika lisilo la kiserikali la Lawyers Environment action Team (LEAT)limetoa mafunzo kwa wadau na wataalam kutoka katika Wilaya zilizopo mkoa wa dar es salaam kuhusu haki za kimazingira kwa wanawake,vijana,wasichana na jamii kwa ujumla kupitia kuwezesha jamii katika masuala ya kisheria.
Lengo la mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo na kuwawezesha wakazi wa jiji la dar es salaam kuelewa na kutimiza wajibu wao ili kuishi katika mazingira safi na salama.
Aidha malengo mahususi yakiwa ni kuongeza ufahamu wa wakazi wa dar es salaam juu ya haki za kijamii na kiuchumi kwa wanawake , vijana, wasichana na watoto na jamii na pia kuongeza uungwaji mkono wa wadau juu ya mahitaji na vipaumbele vya jamii ziishizo jiji la dar es salaam hususani katika kufikia haki za kimazingira.
Pia wakufunzi kutoka shirika la lawyers Environment (LEAT) waliendelea kusisitiza juu ya uthubutu na kuhakikisha sheria zilizowekwa kuhusu utunzaji wa mazingira zinazingatiwa na itasaidia mazingira kuwa safi na salama.
Sambamba na hayo LEAT iliunda timu ya watu saba kutoka katika kila wilaya kwaajili ya kufuatilia halu mazingira na kutoa mapendekezo juu ya nini kifanyike kuboresha usimamizi wa mazingira.
Kibamba Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa