• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
Ubungo Municipal Council
Ubungo Municipal Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Malengo na dhamira
    • Maadili ya Msingi
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Elimu Sekondari
      • Agriculture, Livestock and Fisheries
      • Industry,Trade and Investments
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure, Rural and Urban Development
      • Pre-Primary and Primary Education
      • Human Resources Management and administration
      • Health, Social Welfare and Nutrition Services
      • Communit Development
    • Vitengo
      • Legal Services
      • Ukaguzi wa ndani
      • TEHAMA
      • Procument Management
      • Government Communication
      • Finance and Accounts
      • Sports, Culture and Arts
      • Waste Management and Sanitation
      • Natural Resources and Environment Conservation
    • Sheria ndogo ndogo za Manispaa
      • Sheria ndogo ndogo za Manispaa
      • Other Laws
  • Fursa za Uwekezaji
    • Ufugaji
    • Kilimo
    • Masoko
    • Vituo vya Basi
    • Viwanda
  • Huduma zetu
    • Afya
      • iCHF
      • Lishe
      • Social welfare
    • Elimu
      • Pre and Primary Education
      • Elimu Sekondari
    • Biashara
      • Ushuru wa Huduma
      • Usajili wa Tax
      • Leseni za Biashara
      • Ushuru wa Hoteli
    • Ujasiliamali
      • Ten Percent Loans
    • Kilimo
    • Uvuvi
    • Ufugaji
      • UJUWA
  • Madiwani
    • Orodha za Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za kudumu
    • Ratiba za vikao vya kisheria
    • Ratiba ya Kumuona Meya
  • Miradi
    • Miradi iliyopangwa
    • Miradi endelevu
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Fomu za Maombi
    • Ripoti
    • Sheria
    • Bronchures
    • Zabuni iliyotangazwa
    • Mpango Mkakati
    • Newsletter
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Hotuba

BARAZA LA BIASHARA WILAYA YA UBUNGO LAZINDULIWA RASMI

Posted on: February 15th, 2021

Mkuu wa wilaya ya Ubungo ambaye pia ni Mwenyekiti wa baraza la biashara la Wilaya hiyo  Mhe. Kisare Makori leo februari 15, 2021 amezindua baraza hilo lililojumuisha wajumbe kutoka sekta za umma na sekta binafsi  ikiwa ni chombo cha kisheria cha kusimamia masuala ya biashara zao wilayani hilo.

Akizungumza kwenye kikao cha uzinduzi wa baraza hilo mwenyekiti huyo alieleza kuwa ukuaji wa uchumi unategemea zaidi biashara zinazoendeshwa na sekta binafsi kwa kulipa kodi, kutoa ajira na masuala mbalimbali ya ustawi wa jamii na Taifa kwa ujumla hivyo baraza hilo litasaidia kutengeneza mazingira bora ya kibiashara ili kuleta faida kwa wafanyabiashara na serikali.

Mwenyekiti aliendelea kueleza kuwa kupitia baraza hilo  wajumbe wa sekta binafsi na sekta za umma  kujengeana  uelewa wa mapoja kuhusu masuala mbalimbali yanayohusu uendeshaji wa biashara, ikiwemo sheria na kanuni zinazosimamia biashara pamoja na kuainisha fursa zilizopo na namna ya kuzitumia kwa lengo la kukuza uchumi.

Akisoma taarifa fupi kuhusu baraza la biashara mwakilishi kutoka baraza la biashara la Taifa (TNBC)  Willy Magehema ameeleza kuwa uanzishwaji wa baraza hilo ni wa kisheria kupita  waraka wa Rais Na.1 wa mwaka 2001 likiwa na lengo la kuunda jukwaa la majadiliano kati ya Sekta za Umma na Binafsi ili kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji.

Wajumbe wa baraza la biashara la wilaya  ya Ubungo  wakifuatilia mjadala 

"Baraza hili ni chombo halali cha kisheria cha  kuchambua changamoto zinazokwamisha biashara katika wilaya yenu na kuzijadili kwa pamoja na hatimaye kujenga uelewa wa pamoja kuhusu uendeshaji wa biashara unaoleta manufaa kwa pande zote mbili katika harakati za kukuza uchumi" alifafanua Magehema.

 Magehema amesisitiza kuwa ameeleza baraza  lina wajibu mkubwa wa kutengeneza mazingira bora ya kufanya biashara na kuwekeza, kuibua fursa za uwekezaji na  kuzindua fursa hizo kupitia makongamano ya uwekezaji pamoja na kuandaa midahalo mahususi.


Aidha Magehema,   alitumia nafasi hiyo kutoa rai kwa wajumbe wa baraza hilo  kubuni , kushauri na kuboresha mazingira   ya kibiashara ili kukaribisha wawekezaji katika maeneo ya wilaya ya Ubungo.

Kwa upande wake mwenyekiti wa wafanyabiashara sekta binafsi (TCCIA) Clement Bocco  amesema kuwa kuzinduliwa kwa  baraza hilo ni fursa nzuri kwa wafanyabiashara  kwani litatumika kutuunganisha na sekta za umma na hatimaye kuzungumza lugha moja katika kuhakikisha wafanyabiashara anakuwa na mazingira bora kufanyia biashara na serikali kukusanya Lodi bila malalamiko.

Bocco anaamini kuwa "Ubungo ni wilaya mpya, inakua, tunategeme kwa pamoja tutahakikisha tunatumia fursa zilizopo ili kukuza biashara zenu kwa kuboresha utoaji wa huduma na  kutoa /kuzalisha ajira nyingi"


Taarifa

  • KIBALI CHA KUANZA KUTOZA USHURU WA KUSHUSHA NA KUPAKIA MIZIGO July 17, 2023
  • KUKANUSHA TAARIFA YA UWEPO WA HARAFU MBAYA STENDI YA MABASI MAGUFULI July 06, 2023
  • MATOKEO YA SENSA YA WATU NA MAKAZI 2022 Ubungo September 06, 2023
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI NAFASI YA DEREVA NA KATIBU MAHSUSI July 21, 2022
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • KATA YA UBUNGO YAKABIDHI MKOPO WA TSH. 122,800,000/= KWA VIKUNDI SITA VYA ASILIMIA 10

    May 02, 2025
  • KAMPENI YA KATAA UCHAFU, SAFISHA, PENDESHA UBUNGO YAZINDULIWA, MITAA SAFI NA MICHAFU KUPEWA ZAWADI

    May 03, 2025
  • FANYENI KAZI, MSIJALI MASILAHI BINAFSI" ~ CHALAMILA

    May 01, 2025
  • HUDUMA YA KUJIFUNGUA KWA UPASUAJI YAANZA RASMI KITUO CHA AFYA GOBA,WANANCHI WAKARIBISHWA

    April 30, 2025
  • Tazama zote

Video

KIWANJA CHAKO KINA HATI? | UMEKUWA UKISUMBULIWA NA MIGOGORO YA ARDHI? | KARIBU KWENYE ARDHI CLINIC
More Videos

Viunganishi vya haraka

  • Leseni za biashara
  • Ushuru wa Hoteli
  • Kibali cha ujenzi
  • Sheria ndogondogo
  • Malengo na Dira
  • Muundo wa Uongozi
  • zabuni

Viunganishi linganifu

  • The National Examinations Council of Tanzania
  • TAMISEMI
  • Ministry of Education
  • President office State House
  • National Council for Technical Education
  • Ministry of Finace and Planning

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya wanaoingia

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Luguruni Area, Morogoro Road

    Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam

    Telephone: +255 22 2926341

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: md@ubungomc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa