Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini( TARURA) Wilaya ya Ubungo tarehe 14.1.2021 wamewasilisha rasimu ya bajeti kwa Mwaka wa fedha 2022/2023 yenye thamani ya bilioni 3.2 kwaajili ya kuboresha mtandao wa barabara wenye kilomita 574.56
Akiwasilisha rasimu ya bajeti kwenye kikao maalum Cha kupitisha Rasimu ya bajeti ya matengenezo na ujenzi wa BARABARA kwa Mwaka wa fedha 2022/2023, Meneja wa TARURA Wilaya hiyo Ndg.Musa Z.Mzimbiri alisema kuwa matengenezo ya Barabara yatajikita kwenye Maeneo korofi ,Maeneo maalum,Vivuko na matengenezo ya kawaida
Aidha Mussa alisema mtandao huo wa barabara unaolenga kuboresha huduma za kijamii ,kiuchumi na kiufundi kwa wananchi utazingatia vipaumbele vya kuhakikisha Maeneo yote yanafikika wakati wote kwa kutengeneza muunganiko wa usafiri wa barabara Kati ya mitaa na Kata
Pia Mussa amefafanua kuwa kiwango Cha rasimali fedha kwa mujibu wa mahitaji halisi ya matengenezo ni karibu Bil 17.1 lakini bajeti iliyopangwa ni bilioni 3.2 hali inayopelekea kutotengeneza barabara zote kwa wakati mmoja katika kipindi husika
Akipongeza baada ya kupokea tarifa hiyo Mwenyekiti wa kikao ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mheshimiwa Kheri ameipongeza TARURA kwa utendaji kazi wa kuhakikisha barabara za mitaa zinapitika ukizingatia barabara nyingi zinachangamoto
Aidha Wajumbe wa kamati hiyo wakichangia rasimu hiyo kwa nyakati tofauti tofauti wamepongeza utendaji kazi wa TARURA na kuwaomba mpango huo utekelezeke kwa asilimia 100 ili kuondoka kero ya ubovu wa barabara kwaajili ya kuchochea maendeleo
Aidha kwa Mtandao wa barabara za vijijini na mijini ( TARURA) Manispaa ya Ubungo una urefu wa jumla ya Km 574.56 ambapo km 221.44 barabara ya makusanyo (collector) km 353.12 ni barabara za mlisho (feeder) na km 0 ni barabara za Jamii (community)
Sehemu kubwa ya mtandao wa barabara 91.67% ni tabaka la udongo na kiasi kidogo Cha changarawe na barabara zilizo na tabaka la lami na zege ni km 47.84 sawa na asilimia 8.33
Kibamba Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa